Kusadikika: Nchi inayowapoteza wazalendo na kuwalinda mafisadi

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,893
3,200
Asalaam Aleykum wapenzi wana JF wenzangu.

Kati ya vitabu vigumu kabisa kuvielewa ni pamoja na vitabu vya Hayati Shaaban Robert na Mkerewe mmoja aliyekuwa anaitwa Euphrase Kezilahabi (kwa sasa marehemu).

Hawa wanaume sijui walikuwa wanafikiri kwa kutumia mechanisms zipi maana vitabu vyao vingi ni vigumu kuvielewa. Na sababu ya kuandika kwa mafumbo, bila shaka zinaeleweka.

Leo, nimejikuta nakikumbuka kitabu cha KUSADIKIKA ambacho kimeandikwa na Hayati Shaaban Robert, kikielezea namna ambavyo uonevu na ukosefu wa haki ulikuwa umetamalaki katika nchi ya WASADIKIKA.

Na kwa sababu hiyo hali ilikuwa imezoeleka katika nchi hiyo, ilifikia hatua WASADIKIKA wengi wakawa Wapumbavu sana kiasi kwamba walishindwa hata kujua wanachokitaka katika maisha yao. Na kwa bahati mbaya zaidi wengi wao walikuwa waoga na kama tunavyofahamu uoga huambukiza.

Viongozi wa Wasadikika kwa kuchukulia upumbavu na uoga wa WASADIKIKA, walikuwa wanajinufaisha wao tu na ndugu zao wa karibu au marafiki zao.

Wale ambao walionekana kutaka kuwaamusha wenzao kwa kupinga yanayoendelea, walifunguliwa kesi za uhaini, kufungwa, kupotezwa kusikojulikana na hata kuuawa.

Hivyo, Kusadikika ikawa nchi ya hovyo kabisa kuwahi kutokea duniani, ambako hawakuwa tena na uhakika na kesho yao.

Cha kusikitisha sana, watu wabaya na waliokuwa wanawanyonya wanyonge, walikuwa wanalindwa sana na hata kupandishwa vyeo.


Basi bhana kusadikika ikawa kusadikika
 
Nchi ya Kusadikika ndiyo hii Tanzania yetu bila shaka. Maana mwandishi amepita mulemule.

Na mpaka muda huu unaweza kuta hicho kitabu wameshakiondoa kwa hila kwenye mitaala yetu. Maana watawala wetu hawataki kabisa kuambiwa ukweli.

Muda wote wanataka kusifiwa tu kama yule Mfalme Juha.
 
Nchi ya Kusadikika ndiyo hii Tanzania yetu bila shaka. Maana mwandishi amepita mulemule.

Na mpaka muda huu unaweza kuta hicho kitabu wameshakiondoa kwa hila kwenye mitaala yetu. Maana watawala wetu hawataki kabisa kuambiwa ukweli.

Muda wote wanataka kusifiwa tu kama yule Mfalme Juha.
Sifa huwa zinawalevya sana watawala.
Tate Mkuu itabidi na sisi tuanze kusifia labda tutatafutiwa kacheo Mkuu.
Maana sasa hivi ili upate uteuzi, basi sifa ya kwanza ni ujue kusifia hata pasipo na sababu za kusifia
 
Back
Top Bottom