Askofu Mwamakula achambua wimbo wa 'mnatuona nyani' na kutoa ushauri kwa watawala

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Hayati Shabaan Robert aliandika 'Kusadikika' na 'Kufikirika' ili kuisema Serikali ya Kikoloni ya Waingereza. Wakoloni hawakumkamata, badala yake aliendelea kufanya kazi katika Serikali ya Kikoloni. Hayati Saadani Kandoro pia aliandika shairi liitwalo 'Siafu Wamekazana', katika shairi hilo wakoloni aliwaita 'nyoka' na Ikulu aliipa jina la 'pangoni' na wapigania uhuru akiwaita siafu. Lakini wakoloni hawakumkamata Kandoro pia.

Hatuwezi kusema wakoloni wa Kiingereza wao hawakujua Kiswahili na hivyo walishindwa pia kuelewa nahau na mbinu za Shaaban Robert na Saadani Kandoro! Kama tutafikiri hivyo basi tutawafanya waonekane kama nyani! Ukweli ni kuwa wakoloni walielewa fika harakati ambazo zilikuwa zinafanywa na watunzi wale.

Ney wa Mitego na Sifa Bujune nao wameimba nyimbo za kuisema serikali yao. Lakini kabla ya hakujacha wakaitwa kuhojiwa, wimbo wa Ney wa Mitego ukapigwa marufuku, na Sifa Bujune akatiwa kolokoloni, akanyimwa hata dhamana!

Hata wakati huu, Askofu hajapata taarifa kama Sifa Bujune ameaçhiwa tangu akamatwe siku ya tarehe 13 Septemba 2023. Hii ina maana ya kuwa anashikiliwa kinyume cha Sheria!

Wakoloni pamoja na manyanyaso yao lakini pia wao hawakupiga marufuku vitabu na mashairi ya wanaharakati. Badala yake, mitambo yao na ofisi zao zilitumiwa na wanaharakati katika zile kazi za fasihi. Wakoloni hawakuwahi kufikiri pia kumkamata Shaaban Robert.

Uchochezi ni makosa yanayopatikana katika nchi ambazo sio za kidemokrasia. Kwa lugha rahisi, sifa ya nchi zilizo na harufu ya udikiteta ni kuwepo kwa hisia na dhana za maneno ya uchochezi ambayo hutumiwa na watawala ili kuwanyamazisha wakosoaji. Watawala katika mifumo ya udikiteta hupenda kusifiwa na watu wote na kila wakati na kila mahali. Hawapendi kabisa kuona au kusikia watu wakiwakosoa au kuwanung'unikia hata katika mambo ya wazi.

Kamanda wa Polisi (RPC) wa Mkoa wa Mbeya anasema Sifa Bujune ameimba uchochezi! Ila tukiuchunguza wimbo wa 'Mnatuona Nyani' na tukiuweka katika midhani tunaona malalamiko ya mwananchi kwa serikali yake. Malalamiko hayo hayana tofauti na malalamiko ya watoto kwa baba yao anayetumia pesa katika masuala ya ulevi badala ya kuwapeleka watoto shule.

Baba anayejitapa kujenga nyumba nzuri na pia kujaza vyakula kwenye mafriji lakini anapuuza afya, elimu na hataki kusikiliza hisia za watoto wake hawezi kukosa kulaumiwa na watoto hao!

Vile vile, kuna mambo ya msingi ambayo kwa maoni ya Sifa Bujune, serikali haijasikiliza hisia zao. Kwa maoni yake, mtu asiposikiliza hisia za watu wengine ni sawa na kuwaona kama nyani kwani nyani hawana hisia kama za binadamu.

Na tangu dunia iumbwe, watawala hawajawahi kupewa mamlaka na Mungu kuchagua lugha ya kutumiwa na watawaliwa katika kukosoa au kulalamikia mifumo ya utawala. Tunaweza pia kuona mifano mingi hata katika Biblia.

Yohana Mbatizaji aliwaita mafarisayo pamoja na wateule (makamishna wa Kodi) wa Mfalme wa Rumi kuwa ni kizazi cha nyoka (Luka 3:7-9), na Yesu Kristo alimuita Mfalme Herode kuwa ni mbweha (Luka 13:32). Nabii Amos aliwaita wake wa watawala wa Israeli ya Kale katika Mji Mkuu wa Samaria kuwa walikuwa ni 'ng'ombe wa Bashani' (Amos 4:1-3).

Ni vizuri tuwakumbusha watu wanaowasaidia watawala pamoja na watawala wenyewe katika Tanzania ya leo kuwa wakianza kukimbizana na wakosoaji kwa kuwakamata na kuwaweka ndani; kuwatesa na pia kuwanyamazisha watu wanaolalamikia kutoridhishwa na utendaji wa serikali yao, hiyo itakuwa ni kuasisi anguko la serikali husika. Hivi ni mfalme au mtawala gani wa dunia aliyewahi kuzima malalamiko ya watu anaowatawala kwa kutumia vyombo vya dola?

Ni matumaini yetu kuwa wahusika watatafakari uchambuzi huu pamoja na ushauri. Kubambika kesi watu, kunyanyasa watu na kufinya haki za watu ndio njia pekee ya uchochezi kwani kwa njia hiyo, idadi ya watu watakaoichukia serikali inazidi kuongezeka kila siku.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 19 Septemba 2023; 6:55 usiku

FB_IMG_1695140225987.jpg
 
Ukoloni ni nini


"Mzee fulani ni mkononi sana" Kauli hii ilisika miaka flani hivi ya 2000 kurudi nyuma.
 
Jiulize swali viongozi wote walioongoza kuanzia 1961 wamekufa maskini ,tafsiri yake ni kuwa wakoloni walikuwa na maadili Sasa geuka Leo baada ya huo Uhuru kila mahali pananuka rushwa imefikia mahalaaa hadi uchawa imekuwa ajenda ,kila waziri lazima awe na mahotel,majumba,na makochokocho mengi ,je saizi tumekosa nini?
 
Ngorongoro ndugu zetu WANAHAMISHWA KWA NGUVU ,mnatuona nyani....

Yaani huu usiwe uchochezi wa kutokamatwa?!!!!!!

Kutetea ujinga hakuwezi kuitwa BUSARA......

#SiempreJMT
 
Hayati Shabaan Robert aliandika 'Kusadikika' na 'Kufikirika' ili kuisema Serikali ya Kikoloni ya Waingereza. Wakoloni hawakumkamata, badala yake aliendelea kufanya kazi katika Serikali ya Kikoloni. Hayati Saadani Kandoro pia aliandika
Watawala wameshikwa pabaya karibu wataanza kukamata na mbwa wanaobweka..
Nje ya mada kidogo
Mwimbaji kwaya na supikha wa jumba bovu nani anaonekana ni mkimbizi
Tuseme za kweli?🤪
 
Ngorongoro ndugu zetu WANAHAMISHWA KWA NGUVU ,mnatuona nyani....

Yaani huu usiwe uchochezi wa kutokamatwa?!!!!!!

Kutetea ujinga hakuwezi kuitwa BUSARA......

#SiempreJMT
Mbona nyumbu wetu humu, hawajarudishwa polini, "nikisema kwenye msafara wa mamba na kenge wamo" wanaoongelewa hapa ni binadamu sio kenge na mamba wa mtoni ni semi tu kuonyesha hisia waambieni wapunguze makasiriko.
 
Back
Top Bottom