Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Watanzania tuache siasa kwenye mambo ya msingi Tanzania ni ye2 wote c ya jk, au WARIOBA ni ya watanzania kwa ujumla chamsingi ni kutatua kero sugu zinazotukabili watanzania wa hari ya kawaida. Tukijipanga vizuri na kuweka itikadi zetu za vyama pembeni tutatengeneza katiba bora na yenye kumpa nafuu mlalahoi
 
Acha utoto unaposema mipasho unamaanisha nini... utu uzima pia ni kuwa mstaarabu kwa kila neno unalotamka!

Nimekupata karibu Jf.Inaonekana unaelewa Kiswahili barabara!

Kwa uelewa wangu Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba imekaa kimipasho ,maana nilitegemea azungumze
kama Raisi wa JMT na si Mwenyekiti wa CCM.
 
Japokuwa namheshimu sana Nyerere na natambua mchango wake kwenye Taifa hili; Yeye ndiye katuachia confusion yote hii.

Mimi nadhani Nyerere pia hakua tayari kuingia vyma vingi bali kwakujua yatakayotokea mbele ya safari alitu pre-empt na kutuanzishia vyama vinavyo fanana na upinzani lakini si vya upinzani in their operation.

Sasa ndiyo tunatafuta vyama vya upinzani kweli na demokrasia ya vyama vingi.

Well angekuwepo angetupa sababu ya kutuingiza kwenye hii confusion pengine nia ilikuwa njema labda alitaka guided demokrasia.....Hii ni labda lakini kwa macho yangu yaliyojaa maruweruwe basi successors wake ama hawakumwelewa na hivyo kawaacha wahawajui vision yake au hawakuwa pamoja naye tangu mwanzo.


Kimoja tu ni kuwa we are in a deep confusion; shukrani kwa incubent president amekuwa accomodative!

Vita baridi Kati ya USSR na USA ilimtisha Nyerere wakati huo Tanganyika ilikuwa Nchi ya Kijamaa Ndio Maana aliasisi Muungano kwa nia ya kujikinga na Ubepari kuja kuweka kambi Zanzibar . Lakini lengo la Nyerere lilikuwa Muungano kuboreshwa kulingana na wakati ili baadae Uzae Serikari moja imara. Sasa imekuwa kinyume Zanzibar wamewageuza Bara ndondocha(mabwege)hawajalipa gharama za muungano kwa Miaka 47 hv ! Muungano upo full magumashi pesa nyingi inatumika kubembeleza muungano,wajanja wananeemeka na Bajeti wizara ya muungano pesa inaliwa kero zipo pale pale yaani Kero za Muungano na mladi wa wajanja wachache hivyo hawataki kusikia mabadiliko kwani watakosa Ulaji.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Marekani kuna Muungano wa Nchi 52 Hakuna kero za muungano wala Wizara ya muungano . Hata zile Nchi ndogo hazina Utitiri wa wabunge na viongozi Kama ilivyokuwa zanzibar ! Muungano wetu umepindisha Nia ya Nyerere na malengo yake sasa muungano umekuwa Zigo kwa Tanganyika haipumui inalea Nchi mbili kwa Gharama kubwa . Muungano umegeuka Kuwa njia ya kuifirisi Tanganyika , sasa hatuna budi kuamka na kukataa mambo ya Ajabu juu ya muungano ikishindikana basi Kila mtu aishi kwake kisha tuendelee kuwadai chetu
 
mimo chaguo langu na wanaotutakia nemá ndani ta taifa letu tuchague mfumo wa serikali mbili kwani changamoto zake zinazungumzika. Tusikubali kudanganywa na watu wanaopewa fedha na wazungu kwani lengo kao ní kuturudisha kwenye. Ukoloni. Tuwakatae kama. Raid mugabe alivyo simama.
acha ufala weye m'burulaaa
 
JK katufungua wengi maana tulichanganyikiwa baada ya Warioba kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba kwa hiyo na wewe unapaswa kuwa mwelewa katika jambo hili muhimu lea mstakabali wa nchi yetu na watu wake ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mungu obstojí Tanzania Mungu mbariki JK na umzidishie hekima na busara zaidi
 
Serikali mbili msimamo wananchi wenzangu tusikubali kuhadaika na waru waliopewa mabilioni na mataifa ta wazungu lea lengo lao ní kuvuruga umoja na mshikamano tulionao ndani ya Taifa letu. Endapo tutawapatia fursa ya serikali tátu jana watakavyo tutapekekea dámu kumwagika kama mataifa mengine na dhambi Guo itatugharimu hadí ahera. NARUDIA SERIIKALI MBILI MSIMAMO WA WATU WENYE NIA NJEMA NA TANZANIA YA JULIUS KAMVARAGE NYERERE NA ABEID KARUME WAASISI WETU. MUNGU MBARIKI KIKWETE MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Serikali mbili msimamo wananchi wenzangu tusikubali kuhadaika na waru waliopewa mabilioni na mataifa ta wazungu lea lengo lao ní kuvuruga umoja na mshikamano tulionao ndani ya Taifa letu. Endapo tutawapatia fursa ya serikali tátu jana watakavyo tutapekekea dámu kumwagika kama mataifa mengine na dhambi Guo itatugharimu hadí ahera. NARUDIA SERIIKALI MBILI MSIMAMO WA WATU WENYE NIA NJEMA NA TANZANIA YA JULIUS KAMVARAGE NYERERE NA ABEID KARUME WAASISI WETU. MUNGU MBARIKI KIKWETE MUNGU IBARIKI TANZANIA

Kaka umetumwaaa, unaleta siasa za ccm tena za zama zile walipokuwa wanawadanganya wananchi kuwa upinzani ukichaguliwa watamwaga damu??? Acha campain
 
Katiba mpya ya zanzibar ndio inayotutaka tuwe na tanganyika yetu sababu Inatamka znz kama nchi huru.
kwahiyo hatuwezi kuwa na serikali mbili kwenye nchi mbili bado ukasema huo ni muungano.
na kwakuwa znz wanataka muungano huku wakitaka znz iwe nchi kamili basi serikali tatu ndio jibu muafaka
 
Nadhani waasisi wa Muungano walikua na ajenda zao ... Ila kiundani huwezi kuwa na Muungano wa dola mbili , kimsingi katiba ya Zanziba inatakiwa kubadilishwa ili Zanzibar isitambulike kama ni nchi pia Tanganyika isitambulike kuwa ni nchi , halafu iwepo serikali ya Muungano , kwa maana nyingine ni serikali moja yenye majimbo mawili..
 
Back
Top Bottom