Hajakufungua bali amekuteka kifikra just stand on your own good feetMwanzon nilikuwa nashabikia serikali 3, bila kujua kiundan ila JK kanifungua kwa nini tunataka serikali 2.
Hakuna katiba mpya tena pale. Ninachokiona mimi ni watu wenye nia njema na Tanzania watafunga virago na kuondoka Dodoma.
Kufunga virago kwa Wajumbe ndicho JK na Chama chake wanachokitaka na watafurahi kuona hilo linafanikiwa .
Na hii itakuwa dhambi kubwa kwa UKAWA na wengineo wote kwa kula pesa za walipa Kodi na mwisho kususia kazi waliyotumwa.
Nawashauri kusimamia kidete kufufuka kwa Tanganyika kupitia Muundo wa Nchi mbili Serikali Tatu .
Kinyume na hapo kuwe na Muaafaka wa Nchi moja Serikali Moja na Na hili linafaa kuafikiwa na Wajumbe wote kabla ya kuanza Kujadili Rasimu Nzima ,maana kiuhalisia hakuna mantiki ya kujadili Rasimu kama Muundo wa Serikali haufahamiki/unaleta mgogoro.
Historia siku zote ndiyo inayomuhukumu mtu nilimsikiliza rais wakati anatoa hotuba na kutanabaisha kuwa serikali tatu ni gharama kuliko mbili na viongozi waliouasisi muungano waliona mbili ndio suluhu swali linakuja kama kwale serikali mbili ndio suluhisho nini kwa nini matatizo mpaka leo hayajatatuliwa mpaka sasa mwaka wa 50 huu na kadri tunavyokwenda serikali mbili ipo kwenye deni kubwa ambalo halilipiki zaidi ya nchi wahisani kufanya chochote wanachotaka kutokana na deni wanalotudai.
Swali la pili kama kweli sio unafiki kusema tunawaenzi waasisi nakumbuka hotuba moja ya mwalimu julius nyerere aliwahi waasa viongozi na kuwaambia rasilimali tulizokuwa nazo mfano madini na vinginevyo haviozi kwa hiyo viachwe mpaka nchi yetu tanzania itakaposomesha vijana wake na kuwa na wataalamu wa kutosha kuweza kusimamia na kuzitumia rasilimali za nchi ipasavyo je kama kweli hamkimbii kivuli chenu kwa nini katika hili hamkumuenzi mwali mkaanza kujimilikisha rasilimali za nchi kama za kwenu ? Uko wapi uzalendo hapa mnaouzungumzia zaidi ya uhafidhina .
Na ikumbukumbukwe kwamba enzi ya chama kimoja ccm walikuwa hawataki kabisaa kusikia nchi imeingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwalimu akaitisha kura ya maoni watu wengi wakakataa vyama vingi wachache wakakubali vyama vingi lakini kutokana na upeo na maarifa aliyokuwa nayo mwl nyerere na kuangalia wakati uliopo akayachukua maoni ya watu wachache na kukubali nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi huyo ndio kiongozi aliyetumia busara hekma na maono kuepusha shari ambayo ingewezatokea mabeleni kutoka na wakati uliopo.
Hoja inakuja kwamba serikali tatu kwa wakati huu tuliopo haiepukiki kama ni gharama hata hii tulionayo sasa kila kichwa cha mtanzania kilicho hai kinadaiwa laki tano anaekataa haya aje na hoja ni kwanini muundo wa serikali mbili bado umeliingiza taifa katika deni kubwa ambalo halilipiki na kama litalipwa mtuambie ni nani atakaezilipa ni heri kuishi na mchawi kuliko kuishi na mnafki .