Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Serikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!
Naona umeshachukua card ya CCM hivi ni namba ngapi?
 
Huwezi ukaunganisha vipande vya kamba viwili then ukiulizwa unasema una kamba mbili;kwa kifupi hatuna Muungano wa namna hiyo ila tuna poteza wakati kwa sababu hatutaki kuukubali ukweli licha ya kuwa tunaujua ukweli ni upi na uongo ni upi.
 
Serikali 3 ili kuwapa fursa Wazanzibar wafanye yao kwa uhuru zaidi, pia ili watanganyika watambulike rasmi
 
Serikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!
Haki za Muungano na wajibu wa Nchi shiriki alizozitaja Warioba unaziweka wapi?
 
Serikali mbili ila baadhi ya twiga tuwapeleke msitu wa Ngezi na Jozani ili kubalance maliasili za wanyama.

na kwa kuwa Zenji hakuna kiwanja kikubwa cha kutua madege yanayoiba twiga nadhani watabaki salama zaidi
 
Cha kwanza Tanzania ni nchi huru inayo jiamuliya mambo yake yenywewe na katika hili swala la muungano kuna suluhisho moja tu ambayo litawaridhisha wote watanganyika na wazanzibari na muundo huo ni huu.

Tunakuwa na mataifa huru mawili ndani ya serekali moja maana yake ni hii, Tunakuwa na nchi huru mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibari zitakazo ongozwa na mawaziri wakuu wawili watakao wachagua na wabunge ndani ya mabunge husika yaani ya kila nnchi lakini hizi nchi mbili zote zitakuwa zinaongozwa na raisi mmoja ambayo atachaguliwa na watanzania woote ili kuimarisha umoja wa kitaifa.

Mawawaziri wakuu ndo viongozi wa nnchi husika na wote watakuwa chini ya rahisi wa tanzania na huyu rahisi wa tanzania atatawala nnchi yoote kwa ujumla na hayo ndo mawazo yangu mnaruhusiwa kuboresha na kukosoa pia.

MUNGU WABARIKI WANAOTAKA KUBARIKIWA.......EEMEN
 
Cha kwanza Tanzania ni nchi huru inayo jiamuliya mambo yake yenywewe na katika hili swala la muungano kuna suluhisho moja tu ambayo litawaridhisha wote watanganyika na wazanzibari na muundo huo ni huu
Tunakuwa na mataifa huru mawili ndani ya serekali moja maana yake ni hii, Tunakuwa na nchi huru mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibari zitakazo na ongozwa na waziri wakuu watakao wachagua na wabunge ndani ya bunge lakini hizi nchi mbili zote zitakuwa zinaongozwa na raisi mmoja ambayo atachaguliwa na watanzania woote ili kuimarisha uumoja wa kitaifa
Na mambo mengine ya kiutawala yataendelea kawaida ila wawaziri wakuu ndo viongozi wa nnchi husika na rahisi ndo atatawala nnchi yoote kwa ujumla hayo ndo mawazo yangu mnaruhusiwa kuboresha na kukosoa pia, MUNGU WABARIKI WANAOTAKA KUBARIKIWA.......EEMEN

Fanya editing kwanza ndo utoe post yako mkuu,hapo tutachangia.
 
Cha kwanza Tanzania ni nchi huru inayo jiamuliya mambo yake yenywewe na katika hili swala la muungano kuna suluhisho moja tu ambayo litawaridhisha wote watanganyika na wazanzibari na muundo huo ni huu.

Tunakuwa na mataifa huru mawili ndani ya serekali moja maana yake ni hii, Tunakuwa na nchi huru mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibari zitakazo ongozwa na mawaziri wakuu wawili watakao wachagua na wabunge ndani ya mabunge husika yaani ya kila nnchi lakini hizi nchi mbili zote zitakuwa zinaongozwa na raisi mmoja ambayo atachaguliwa na watanzania woote ili kuimarisha umoja wa kitaifa.

Mawawaziri wakuu ndo viongozi wa nnchi husika na wote watakuwa chini ya rahisi wa tanzania na huyu rahisi wa tanzania atatawala nnchi yoote kwa ujumla na hayo ndo mawazo yangu mnaruhusiwa kuboresha na kukosoa pia.

MUNGU WABARIKI WANAOTAKA KUBARIKIWA.......EEMEN

Hilo linaweza kuwa suluhisho na rasimu inalega hilo lakini wasiwasi wa JK na wahafidhina wenzake ni kuwa Watanganyika hamuutaki muungano hivyo mkipewa nchi yenu mtauvunja, hivyo mbaki mkilalama maisha yenu.
 
nafikiri inaleta mantiki, na inawezekana suluhisho likawepo kwenye mweelekeo wa namna hiyo
 
3 ndio jibu. Wanaosema kuhusu mapatp watuambie hii ya muungabo wa sasa inamiliki ardhi ipi na mapato inapataje?( kama ipo)
 
Duniani kote, na hata uwalete wataalamu washauri wa aina gani, swala tata kama hili la kwetu la kubishania idadi ya watu wanaopendekeza serikali tatu, au mbili huamuliwa kwa kura ya maoni pekee. Na ndio ushirikishwaji wa wananchi kwenyewe huko. Sasa sijui viongozi wetu hawalioni hilo au wamepofushwa na ibilisi mpaka machafuko yatokee kwanza ndio wapatanishi waje kutueleza kwamba muarobaini wa haya mabishano ni kura ya maoni? Viongozi wetu hamuoni hili jamani? mnaogopa nini kuwauliza wananchi wanavyotaka kuongozwa? Au nyie ndio mnaojua zaidi ni vipi wananchi wanatakiwa kuongozwa kuliko wao? Mbona jambo dogo sana hili? Viongozi mnawaogopa wananchi wenu?
 
MADAI YA UKAWA:-
  1. MADAI YASIYOKUWA NA MAANA

  • Katiba ya znz kuchakachuliwa: hili dai halina maana kwani znz kujiita nchi haimpungumziii mtanzania kitu chochote, rais wa znz kupewa mamla ya kuigawa mikoa ya znz dai hili halina maana kwa vile kwa udongo wa znz yenye mikoa mitano wala hakuna cha kugawa na ukweli wala hakuna chochote shein alichogawa.suala la rais wa znz kuanzisha vikosi vya ulizi ambavyo ni kmkm hoja hii haina maana kwa vile hao jamaa ni wanamgambo wa jiji na kulinda karafuu kwa uchache wa askari hata hapo dar inabidi kutumia askari mbadala hii haina tabu wala hao wanamgambo hawana cha kufanya hii hoja ni hewa.HOJA HIZO HAPO HAZINA EFFECT YEYOTE KWA MTANZANIA ziondolewe au kutoondolewa haziwezi kupunguza uchumi wa mtanzania yeyeto wala kuongeza wala hazina athari na usalama maana usalama uko makini huko znz chini ya mwamunyange.


2. MADAI YENYE HOJA.
  • Watanganyika kutoruhusiwa kumiliki ardhi znz:hili dai lina hoja kidogo Ingawa znz haina ardhi na hata huko ndani ndani ardhi ya znz ni bei juu kuliko ya uswahilini dar, yaani mil 5 ndio unaweza pata kakiwanja znz angali dar kule mbagala mil 3 unapata kiwanja safi kabisa. ILA KWA KUWA KUNA WANAOISHI HUKO KWA MIAKA MINGI NA KUJIKUTA ANAKUWA NA FAMILIA NA WAJUKUU huwezi kubeza hoja hii.Kunyimwa kuchagua viongozi wa kisiasa huko: hili kidogo lina hoja maana ukiwa kisiwani unatibiwa kisiwani,utasoma kisiwani hivyo unavipaumbele vya maisha ukiwa huko ingawa hoja inaweza isiwe na uzito sana.HIZO NDIO HOJA KUU ZA KUELEWEKA KIDOGO KWA UKAWA KUTAKA SERIKALI TATU JE ZINAKIZI MADAI YAO? KWELI SERIKALI 3 NDIO SULUHU?JIBU UNALO WEWE



MADAI YA KUNDI LA TANZANIA KWANZA
  1. MADAI YASIYOKUWA NA MAANA: Waznz kumiliki mashamba tanganyika angali watanganyika wamejikubalishja wenyewe, wame sign kuwa watumwa na wapangaji kwa nini wanahoji waznz kumiliki? huu kwa lugha fupi ni ulimbukeni.Znz haina rasilimali:hii ni hoja ya kijinga kuwahi kutokea maana znz ni ndogo hiihitaji mamia ya majeshi au msurulu wa rasilimali,utalii pekee unaweza yote hayo kwa hesabu za kawaida ,maana wanaweza kuwa wanahitaji polisi 100 na wanajeshi 1000 tu.
  2. MADAI YA MAANA: KUTOKUWA NA AMANI KATIKA ZNZ KUTAKAKOSABABISHA KUYUMBISHA AMANI TANGANYIKA:kutoka na hali ya kisiasa znz, kwa rais kupisha kura za urais kwa mamia huyu ana asilimia 50%.. na huyu ana asilimia 49..% huku chama kimoja kikishinda majimbo yote ya kisiwa kimojawapo na bado kushindwa kuongoza nchi, ukichanganya na ubishi na upinzani wa zppp na asp ,kuchanganya dini katika siasa na kufanya maamuzi ya kisiasa kwa kutumia vifungu vya dini inaweza lete vurugu visiwani, ukijumlisha na askari wote nao wanakuwa na itikadi hiyo hiyo kuna kuwa na uwalakini.HAPO SASA TUAMUE WENYEWE JE TUNATAKA NINI? nieleweke sijasema vita itatokea znz bali historia inaonesha ni nguvu znz kutulia bila external force. asiyembishi atakubaliana nami kuwa hakuna tofauti ya kuonekana kati ya znz na mombasa au znz na somalia na kote hitilafu ni kuchanganya dini na siasa, angali dunia inaenda upande fulani wengine hupendwa kwenda upande waujuo wao.
 
Back
Top Bottom