Kupanda kwa Bei ya chakula na dhana ya kufunguliwa kwa Mipaka Nchini

Jay2525

Member
Mar 5, 2014
68
120
1664285739587.png
1664285784409.png


Na Taban J

Kumekuwa na nadharia kuwa, kupanda kwa bei ya mazao ya chakula kumesababishwa na kufunguliwa kwa mipaka. Jambo linalo pelekea mazao ya chakula kubebwa na majirani zetu wa Uganda na Kenya hivyo kusababisha upungufu wa chakula na kupelekea bei ya mazao kupanda. Huku lawama ikibebeshwa serikali kwa kufungua mipaka na kuruhusu biashara ya mazao baina ya taifa letu na mataifa mengine. Nadharia hii ni sahihi japo biashara baina ya Taifa letu na mataifa mengine inafaida kubwa ikilinganishwa na kupanda kwa bei ya mazao.

Ili kufafanua hoja yangu, nipende kujikita kwenye uchambuzi wa kichumi. Kwani biashra ya kimataifa (Intrenational Trades) ni mada muhimu katika sayansi ya uchumi, hivyo ni vema kuangazia kanuni za uchumi (Economic Principles) ili kujenga uelewa wa pamoja

Kanuni za kiuchumi kuhusu biashra ya kimataifa zinaelezwa na manguli wawili wa uchumi yaani Adam Smith na David Ricardo, katika kanuni ya Absolute advantage na comparative advantage. Katika kanuni hizi zote inaelezwa: Kama Taifa (A) linaweza kuzalisha bidhaa (X) kwa gharama kidogo ikilinganishwa na Taifa (B). Huku Taifa (B) likiwa na uwezo wa kuzalisha bizaa (Y) kwa gharama kidogo ikilinganishwa na Taifa (A) . Basi mataifa haya mawili yatanufaika yote kwa Pamoja kwa kufanya biashara. Ikiwa Taifa A atazalisha bidhaa X na kununua bidhaa Y toka taifa B. Wakati Taifa B akizalisha Bidhaa Y akinunua bidhaa X toka taifa A.

Kutokana na jiografia yetu,katika ukandawa nchi za Africa Mashariki Tanzania imekuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha mazao ya chakula kwa gharama nafuu ikilinganishwa na mataifa mengine ya ukanda huu. Hivyo kuna faida kubwa kwa kuzalisha zaidi mazao ya chakula na kuyauza kwa majirani. Huku tukiendelea kunufaika Zaidi kwa kununua bidhaa ambazo sisi tunazalisha kwa gharama kubwa ikilinganishwa na wenzetu wa Afrika Mashariki.

Mfano Mwaka 2021 Tanzania kwa kuzingatia kanuni hizi, ilinunua bidhaa toka Kenya kwa bei nafuu zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 410.88 Ikiwa ni sabuni, madawa (pharmaceuticals), mabati , plastiki na nyinginezo. Huku ikiuza Kenya bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani Milioni 489.84 ikiwa ni nafaka, Mbao, Mafuta ya Kupikia na nyinginezo.

Kwa mfano huo maana yake kama mipaka ya kibiashara ingefungwa, Kenya ingepata uhaba mkubwa wa mazao ya chakula na Misitu huku Tanzania ingepata uhaba mkubwa wa sabuni na madawa. Bidhaa hizi zote zikiwa na umuhimu mkubwa kwa matumizi ya binadamu. Lakini uhaba huu umweza kuwa balanced kwa mataifa baina yetu kufungua mipaka na kuruhusu biashara. Biashara hii imepelekea wakenya kuuza bidhaa zao kwa bei kubwa kidogo nchini Tanzania na kununua baidhaa za chakula kwa gharama nafuu toka Tanzania. Huku kwa upande wa Watanzania wakiuza mazao yao kenya kwa bei kubwa kidogo na kununua sabuni na madawa kwa bei ya punguzo kidogo.

Hivyo kwa kufanya biashara nchi zote zimenufaika kwa kuongeza wigo wa bidhaa zinazoweza kupatikana sokoni. Mwisho wa siku bei haipangwi na serikali bali nguvu ya soko ya demand na supply. Hivyo ni vema vijana kuwekeza kwenye maeneo ambayo kama taifa tunafursa ya kuzalisha kwa gharama nafuu ikilinganishwa na mataifa mengine hivyo kuondokana na swala la kuilaumu serikali kufuatia kufunguliwa kwa mipaka. Kwani kufunguliwa kwa mipaka ni chachu ya kuongeza soko la bidhaa. Mwisho kufunguliwa kwa mipaka tuone ni fursa kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa letu.​
 

Attachments

  • Nafaka.jpg
    Nafaka.jpg
    9.2 KB · Views: 11
  • Bei ya Nafaka.jpg
    Bei ya Nafaka.jpg
    10.2 KB · Views: 11
Back
Top Bottom