Kuota unakula ugali na mboga za majani

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Inamaanisha nini?

Niliota hivi karibuni!

Katika ndoto hiyo, tulikuwa sehemu ambako chakula kilikuwa kinagawiwa kwa utaratibu wa "self service".

Nilisimama kwenye foleni kama wenzangu kuelekea kwenye meza ya vyakula, na nilipofika, vyombo vikawa vimeisha. Ilinibidi mimi, pamoja na waliokuwa nyuma yangu kwenye foleni, kusubiria vyombo vingine vikasafishwe.

Baada ya dakika chache, mhudumu alirejea na vyombo vilivyosafishwa, ila vilikuwa vya plastiki.

Nilijongea mezani na kuchukua sahani na bakuli na kujipakulia ugali mweupe (unga wa sembe) na mboga za majani, na kwenda kukaa nilikopachagua kwa ajili ya kula.

Wachache waliokuwa nyuma yangu kwenye foleni, nao baada ya kuchukua vyakula vyao, walikuja kukaa nilikokuwa nimeketi.

Sikuwa nawafahamu, lakini baadaye, katika kupiga nao stori, nilibaini kuwa mmoja wa vijana nikiyekuwa nikizungukza naye alikuwa Mkenya. Aliniambia baada ya kumwuliza anakotokea.

Nini tafsiri ya hiyo ndoto kwa mrengo wa kiroho?
 
Umetoka kwenye ukoo wa kirasta hakikisha unarudi kundini
 
Back
Top Bottom