NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
Unaweza ukawa unakula ugali na mboga za majani na ukajiona unakula chakula chenye afya kumbe uhalisia ni kwamba unajiongezea sumu zaidi mwilini.
Sehemu kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya Mto Msimbazi, Mandela road bonde lililoko kituo cha garage, Jangwani, Kigogo sambusa na maeneo ya Tandale na kwingineko
maji yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu, yenye kemikali toka viwandani, yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayotumika kumwagilia mbogamboga hizi wanazokula wakazi wengi wa jiji hili.
Kwa vyovyote vile, maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa cha sumu mbalimbali zinazoingia katika miili ya wakazi wengi wa Dar.
Uchafu unaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde ni mwingi sana, mabetri ya magari na simu yenye tindikali, mizoga ya wanyama, pedi za wanawake, nk nk vyote hivi vimebeba kemikali zenye sumu kali.
Sumu hizi si ajabu ndizo huchangia matatizo kama upungufu wa nguvu za kiume, bawasiri, vidonda vya tumbo, vijana kuwahi kuota mvi, n.k.
Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa