Kuongezeka kwa mvutano kati ya India na Canada kunaonyesha unafiki wa Marekani wa wenzi unaojali faida

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111454756432.jpg


Mwezi Juni mwaka huu, kiongozi maarufu wa jamii ya Masingasinga Hardeep Singh Nijjar ambaye pia ni raia wa Canada, aliuliwa kwa kupigwa risasi nchini humo. Hivi karibuni, Canada imeituhumu India kuhusika na mauaji hayo, na kumfukuza nchini humo balozi wa India. Katika kujibu hatua hiyo, India nayo ilitangaza mara moja kuwa imemfukuza balozi wa Canada nchini humo, huku ikipinga tuhuma zilizotolewa na Canada na kusema kuwa hazina maana na za uchochezi,

Katika miaka ya kaibuni, mvutano kati ya India na Canada umejikita Zaidi katika jamii ya Singasinga, ambayo inapinga serikali ya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na kutaka haki ya jamii ya Singasinga. Jamii hiyo ni kundi dogo nchini India likiwa na jumla ya watu Zaidi kidogo ya milioni 20. Nchini Canada, ambayo ni moja ya makazi makubwa ya Masingasinga duniani, jamii hiyo ina ushawishi mkubwa wa kisiasa, biashara na uchumi. Kuibuka tena kwa harakati za kujitenga za Khalistan katika miaka ya karibuni kumekuwa sababu kubwa ya mvutano kati ya India na Canada, na kuathiri vibaya uhusiano wa pande mbili hizo. Mvutano huu unaoendelea sasa kati ya nchi hizo umeuweka uhusiano kati ya India na Canada katika hali tete Zaidi.



Wafuatiliaji kwa kawaida wanaamini kuwa kutokutana kwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na mwenzake wa India Narendra Modi wakati wa mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika New Delhi, India, ni ishara ya hatari ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Sasa, nchi hizo zimezidi kutupiana lawama na kufukuza mabalozi, na hivyo kuonyesha wazi hali tete ya kile kinachoitwa mfumo wa wenza unaojali faida unaoongozwa na Marekani.

Nchi za Magharibi zinadai kuwa watetezi wa haki za binadamu, na mara nyingi kukosoa nchi nyingine katika masuala yao yanayohusiana na haki za binadamu. Sifa zake kwa kile kinachoitwa ‘demokrasia’ ya India kimsingi zinatokana na maslahi ya siasa za kijiografia na nia yake ya kuijumuisha India kwenye mwenzi wake wa kuipinga China. Nchi za Magharibi zinafahamu vizuri tofauti iliyopo kati ya kile kinachoitwa ‘demokrasia’ ya India na demokrasia katika nchi zao, na watu wengi katika nchi za Magharibi hawaungi mkono sera za kidini na za makabila madogo ya nchini India.

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti katika Taasisi ya Mkakati wa Kitaifa ya Chuo Kikuu cha Tsinghua, Qian Feng, anasema nchi za Magharibi, hususan Marekani, katika miaka ya karibuni zimekuwa zikipeperusha bendera ya manufaa ya pamoja ya uhuru na demokrasia, zikijaribu kuendeleza ushirikiano wa kina na India ili kuizuia China. Nchi hizo ziko tayari kufunbia macho kile wanachofikiri kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu nchini India na kuwanyima haki watu wa makabila madogo, hatua inayoweka wazi unafiki wa wenzi wan chi za Magharibi na India katika kile kinachoitwa manufaa ya pamoja.

Mtafiti katika Taasisi ya Elimu ya Kimataifa ya mjini Shanghai, Zhao Gancheng anasema, kama nchi za Magharibi kwa dhati zinaichukulia India kama nchi ya kidemokrasia kama nchi zao, bado ni swali ambalo halijapata majibu. Lakini ukweli ni kwamba, nchi za Magharibi zinaihitaji India, hivyo zinatumia fursa iliyopo kutimiza ajenda zao.

Kama mwenzi muhimu wa Magharibi na mashirika wa muda mrefu wa Marekani, Canada imechukua nafasi kubwa kwa Marekani kuanzisha kile kinachoitwa kanuni zenye msingi wa utaratibu wa kimataifa na kuboresha Mkakati wa India na Pasific.

Kwa sasa, India na Canada zote zimefukuza maofisa wa ngazi za juu kutoka kila nchi, na kama uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuzorota, Marekani inaweza kujiingiza kwa haraka kwa madai ya ‘kupatanisha,’ kwani, Marekani kuingilia masuala ya Canada, ni kazi rahisi na iliyozoeleka.
 
Back
Top Bottom