Mzozo kati ya Canada na India una zidi kukua huku mahusiano kati yao yakizidi kuzorota huku kila upande ukifukuza Wanadiplomasia na kunyima Visa raia

PakiJinja

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,652
15,770
Kuna mzozo unaendelea kati ya Canada na India. Mzozo huu ulianza baada ya kiongozi wa Sikh, Hardeep Singh Nijjar, kuuawa mnamo Juni 2023 huko British Columbia. Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, alitangaza kuwa kuna ushahidi wa kuaminika kwamba mawakala wa serikali ya India walihusika na mauaji hayo. Kwa sababu hii, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedhoofika sana. India inaamini kuwa Canada inashindwa kukabiliana na waandamanaji wa Sikh ambao wanataka eneo lao huru.

India imechukua hatua kadhaa dhidi ya Canada. Hatua hizi ni pamoja na kuwafukuza wanadiplomasia 41 wa Canada na kupiga marufuku visa kwa raia wa Canada. Kwa upande wake, Canada pia imefukuza mwanadiplomasia mmoja wa India. Mazungumzo ya biashara kati ya nchi hizo mbili yamekwama. Kwa kuongezea, biashara kati ya nchi hizo mbili inaweza kupungua.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedhoofika sana. Wizara ya Mambo ya Nje ya India ililaani matamshi ya Trudeau kama "yasiyokuwa na maana na yenye motisha". Kwa sasa, hakuna upande wowote unaoonekana kuwa unashinda katika mzozo huu.

Raia wa nchi zote mbili wameathiriwa vibaya na mzozo huu. India ina jamii kubwa zaidi ya watu wenye asili ya Kihindi nje ya nchi yao, ambayo ina karibu watu milioni 1.4. Kuhusu Canada, karibu watu 770,000 waliripoti Sikhism kama dini yao katika sensa ya mwaka 2021.

India iliwafukuza wanadiplomasia 41 wa Canada, wakati Canada iliwafukuza wanadiplomasia mmoja wa India. Mzozo huu umesababisha hasara za kiuchumi kwa nchi hizo mbili. Biashara kati ya nchi hizo mbili inaweza kupungua kutokana na mzozo huu. Hata hivyo, mzozo huu unaweza kuwafanya washirika wa Magharibi wa Canada kuwa na wasiwasi juu ya kuadhibu India kutokana na mvutano wake wa kijiografia na China.
 
Sasa India nani anaenda?
Wahindi wamejaa Canada kuliko wa Canada India.
Lro hii Canada ikiamua kuwatimua Wahindi mbona itakuwa kilio?
 
Ngoja NAMI nianzishe mzozo na shabiki wa timu inayobebwa sana Tz
 
Ukitimua wahindi Canada unatimua labour force kubwa ambayo wameipata kwa bei rahisi.

Ukiangalia maofisini wamejaa wahindi tena wale cream.
Idadi ya watu wenye asili ya India nchini Canada ni 1,858,755, ambayo ni sawa na 5.1% ya idadi ya watu nchini humo.

Kwa upande mwingine, kuna takriban 771,790 wanaofuata U-Sikhism nchini Canada, ambayo ni takriban 2.1% ya idadi ya watu nchini humo.
Hawa wahindi wanaoamini Sikhism wanatokea jimbo la Punjab ambalo linapambana kujitenga kutoka India ma kuanzisha taifa lao.
 
Ukitimua wahindi Canada unatimua labour force kubwa ambayo wameipata kwa bei rahisi.

Ukiangalia maofisini wamejaa wahindi tena wale cream.
Msimu huu wa masomo pekee wanafunzi zaidi ya 225,000 kutoka India walitakiwa kwenda Canada kwa ajili ya masomo, lakini restrictoons zilizowekwa na Canada zimepelekea Mawakala wa kutafutia wanafunzi vyuo waanze kutafutia na kuwaelekeza wanafunzi hao nchi nyingine.

Canada inatarajia kupoteza karibu US$ millioni 300+, kwa kupoteza idadi ya wanafunzi waliotakiwa ku join mwaka huu, pia, mbali ya ada, wanafunzi hao pia hutumia huduma mbalimbali nchini humo kama vile tax, vyakula, apartments n.k

Pia upande wa India itapelekea kuzidisha uhasama na uadui kati ya wahindi wa Sikh na Wahindu.

Kutoaminiani miongoni mwa Wahindi wanaoishi nchi ya India kumezidi kukua tangu Narendra Modi kuingia madarakani, kwani hata ukiangalia ndani ya Marekani kumekuwa na mwamko mkubwa sana wahindi wanaoamini katika Hindu kuungana pamoja ndani ya US na kutengeneza kitu kinaitwa Hindu Nationalism ndani ya US.

Huko India pamoja na PM Modi kukemea mara kadhaa ubaguzi wa kidini na kukanusha kujihusha nao, lakini amekua akijulikana kwa kampeni na matamshi yake kui promo Hinduism over other relogions. Imekishikanisha Chama chake na Hinduism, akasikika akinadi kuwa Hinduism siyo dini bali ni mfumo wa maisha kwa Wahindi.

Kwasasa ni kama vile Hinduization ya taifa la India imeshakamilika. Hali hii imezidi kuamsha sintofahamu kwa makundi tofauti ya kidini nchini India.
 
Mizozo kila upande wa Dunia

Huku Jf pia tuna zozana... ni mwendo wa mizozo ila tuna amini itaisha
Wangetuwekea na magemu umu jamii forum ya kuonyesha ugomvi yenye pande mbili kinzani. Pangekuwa hapatoshi ugomvi na malumbano no sehemu ya maisha ya wanadamu
 
Kwanini wafukuzane, waamshe vifaru na mizinga. Midege ya vita mwisho itaota kutu, wayatumie nasi tufurahi, tumuone kanjubhai anapigana.
 
Back
Top Bottom