Kuolewa SIO bahati...USIBAHATISHE!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,821
59,420
Hua nashangazwa sana na kauli isemayo "kuolewa ni bahati" toka kwa wanaume na hata wanawake. Kauli hii hua inatoka kwa watu wanaoamini kwamba kwa kuolewa, mwanamke anakua amefanyiwa FAVOUR, AMESAIDIWA au AMEPEWA ZAWADI kana kwamba mwanamke pekee ndie anaefaidika na hiyo ndoa. Na hiyo bahati yenyewe inayotokana na kuolewa huko sio kupata mume ambae anastahili kuitwa mume bali ni kupata mahali pa kulala, chakula na mavazi. Wengine hua wanafika mbali kiasi cha kuwauliza wenzi wao moja kwa moja "unalalamika nini wakati unakula, unalala na unavaa vizuri?" pale mwanamke anapoonyesha kutoridhisha na namna mahusiano yao ndani ndoa yanavyoenda mf. mume kutokua mwaminifu, kutokuwepo nyumbani muda wa kutosha, kulewa sana, kumdharau mkewe n.k .

Ina maana wanawake wanaolewa ili wale, walale na wavae? Walipokua kwa wazazi wao au wakijitegemea waliishi bila kula, kuvaa na kulala ndani ya nyumba?

Kinachonisikitisha ni kuwa baadhi ya wanawake wanaunga mkono mawazo haya. Wanakubali kuchukuliwa kama watu wanaopewa msaada kwa kuolewa.

Binafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati". Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.

Kuoa/kuolewa sio bahati hivyo usibahatishe.
 
Unasema kweli. Lakini tatizo la wanawake walio wengi hawataki kujishughulisha kama wanaume wanavyo jishughulisha.
Ndio maana watu kama hao huwa wanauza miili yao. na wakipata mwanaume japo wa kuwafanya wale WANAONA BAHATI.
Lakini kwa mwanamke mwenye fikra komavu hawezi kuona kuwa kuolewa ni bahati.
 
KBinafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati".Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake.
Kazi kweli kweli.

Mtoa mada anasema; Kuolewa haoni kama ni bahati, afu pale pale anasema bahati ipo kama umepata mtu ambae anaelewa nini mana ya ndoa.

Binafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati". Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.

Kuoa/kuolewa sio bahati hivyo usibahatishe.

Hapo penye red panaonesha kuwa kuolewa ni bahati. Mengine nimekubali lakini umejipinga tena mwenyewe na kukubali kuolewa ni bahati
 
Unasema kweli. Lakini tatizo la wanawake walio wengi hawataki kujishughulisha kama wanaume wanavyo jishughulisha.
Ndio maana watu kama hao huwa wanauza miili yao. na wakipata mwanaume japo wa kuwafanya wale WANAONA BAHATI.
Lakini kwa mwanamke mwenye fikra komavu hawezi kuona kuwa kuolewa ni bahati.

Na wanaume wanaosema hivyo je?
 
Kazi kweli kweli.

Mtoa mada anasema; Kuolewa haoni kama ni bahati, afu pale pale anasema bahati ipo kama umepata mtu ambae anaelewa nini mana ya ndoa.

Jaribu kuwa muelewa, nilichosema ni kwamba kitendo cha kuolewa tu pekee(na mtu yeyote yule) sio bahati, bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa maana ya mahusiano yake (mwenye heshima, kujali, mwaminifu n.k).
 
Freeman,

Mwanaume anaweza akawa yeyote kati ya uliowataja lakini akawa anakupenda kwa dhati.

sidhani kwani attention yake itakuwa huko... atanispoil saa ngapi wakati muda mwingi atakuwa nawaza mengine kama hataniabuse?

Mume anatakiwa awe na akili timamu 24/7, so mlevi na teja wanahusika hapa. Mume anatakiwa aniwaze 24/7, hapa malaya anahusika. Mume anatakiwa a provide, hapa king'asti anahusika. Mume anatakiwa tushauriane na tukosoane kama watu wazima na sio kupelekesha mke kama mtoto au gari bovu, hapa abuser anahusika.

Ama kweli kuolewa rahisi ila kupata mume kazi.
 
Huo msemo watu wengine wanautumia vibaya, lakini ukweli ni kwamba ....neno kuolewa/kuoa ni bahati.....halimaanishi kuwa mtu huyu amepata bahati ya kuolewa kwa maana ya kupata mtu wa kumsaidia,.... bali mtu wa kusaidiana naye katika mipango ya maisha. Nasema hivi, kwa sababu baadhi ya wanawake wanaolewa tayari wakiwa wanajiweza kiuchumi na kwa mantiki hii anapata mwenza wa kusaidiana katika maisha na sio mtu wa kumtoa kimaisha. Ndio maana kuna msemo mwingine unaosema.....kuzaliwa na kufa ni lazima, ila kuoa/kuolewa sio lazima kwa maana kwamba mtu anaweza kuishi hata kama hajaoa/kuolewa. Waliopata bahati ya kuoa/kuolewa ni wale waliopata wenza wanaoweza kukaa pamoja na kupanga maisha pamoja na tabia zao zinaendana. Kwa wale wanandoa ambao ni kero kwa wenzao, watambue kuwa hawajapata bahati ya kuoa/kuolewa.
 
nikweli usemayo,lakini tatizo la vijana wengi wasasa hawaangalii sifa za msingi pindi wanapotafuta mwenzi pamoja nakwamba c bahati lakini na hayo yanachangia kwa ndoa nyingi kutodumu.
 
nikweli usemayo,lakini tatizo la vijana wengi wasasa hawaangalii sifa za msingi pindi wanapotafuta mwenzi pamoja nakwamba c bahati lakini na hayo yanachangia kwa ndoa nyingi kutodumu.

Kukurupuka ndio kosa kubwa ambalo mtu anaweza kufanya kwenye haya mambo. Ukikosea hatua tu imekula kwako.
 
Back
Top Bottom