Mr. Bigman
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 2,560
- 1,299
Wakuu, nimekuwa nawaza mara kwa mara kuhusu jamii hii ya Kunguru ambao wamezagaa sasa karibu eneo lote la Pwani ya Tanzania,kuanzia Tanga hadi Mtwara. Jambo moja ninalolijua ni kwamba hawana asili ya Afrika. Wametokea India. One theory inasema walitua pwani ya Tz baada ya ku stow away ktk meli kubwa za kibiashara zilizofika Tz kutoka bara Hindi.
Nyingine inasema waliletwa Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Sheikh Amani Abeid Karume alipofanya Ziara ya India in the late 60's. Alipewa zawadi ya kunguru kadhaa ili waje wazaliane as a control measure ktk mashamba ya karafuu kwani ndege hawa hula viwavi wanaoharibu zao la karafuu. Wakuu, maicologist na wanamazingira mliopo humu,hebu tujadili kama kuna faida na hasara za uwepo wa ndege hawa katika pwani ya Tz.
Inasemekana wamewatimua aina ya ndege wengine wa asili katika miji yetu ya pwani, kwa ama kuwala wao wenyewe, makinda/vifaranga au mayai yao. Lakini pia ni maarufu kwa kukwapua sidiria , chupi, nepi na leso zinapokuwa zimeanikwa uani baada ya kufuliwa.
Pia inasemekana wanakula uchafu jalalani hivyo wanaweza kutumika katika kazi za kusafisha mazingira ya miji. Lakini pia kwa nini wanaishi miji ya pwani tu? Je Dodoma, Arusha na Mwanza wanaonekana?
Nawasilisha