Kunguru weusi a.k.a Kunguru wa Zanzibar

Mr. Bigman

JF-Expert Member
May 7, 2011
2,562
1,299
Wakuu, nimekuwa nawaza mara kwa mara kuhusu jamii hii ya Kunguru ambao wamezagaa sasa karibu eneo lote la Pwani ya Tanzania,kuanzia Tanga hadi Mtwara. Jambo moja ninalolijua ni kwamba hawana asili ya Afrika. Wametokea India. One theory inasema walitua pwani ya Tz baada ya ku stow away ktk meli kubwa za kibiashara zilizofika Tz kutoka bara Hindi.

Nyingine inasema waliletwa Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Sheikh Amani Abeid Karume alipofanya Ziara ya India in the late 60's. Alipewa zawadi ya kunguru kadhaa ili waje wazaliane as a control measure ktk mashamba ya karafuu kwani ndege hawa hula viwavi wanaoharibu zao la karafuu. Wakuu, maicologist na wanamazingira mliopo humu,hebu tujadili kama kuna faida na hasara za uwepo wa ndege hawa katika pwani ya Tz.

Inasemekana wamewatimua aina ya ndege wengine wa asili katika miji yetu ya pwani, kwa ama kuwala wao wenyewe, makinda/vifaranga au mayai yao. Lakini pia ni maarufu kwa kukwapua sidiria , chupi, nepi na leso zinapokuwa zimeanikwa uani baada ya kufuliwa.

Pia inasemekana wanakula uchafu jalalani hivyo wanaweza kutumika katika kazi za kusafisha mazingira ya miji. Lakini pia kwa nini wanaishi miji ya pwani tu? Je Dodoma, Arusha na Mwanza wanaonekana?

Nawasilisha
 
inabidi ufahamu kwanza kunguru hafugiki...........

niliwahi kusikia waliletwa mjini kama scavenger........
 
ninachojua kunguru hawa ni wezi ile mbaya, wanaiba hata chujio za chai, yaani hawana maana na hawaogopi watu
 
Nilisikia kuna mradi wa kuwaangamiza hao kunguru hapo Dsm. Sijui zoezi limeishia wapi!
 
Katika vyote madhara makubwa waliyoleta hawa kunguru weusi ni lile la kutikomeza ndege wa asili ya pwani. Karibu dsm yote kwa sasa haina tena ndege wa asili baada ya hawa kunguru kuletwa. Serikali inabidi ifanye juhudi za makusudi kuwatokomeza hawa kunguru weusi.
 
Hawajaletwa, wakuja hao.
 
Hawajaletwa, wakuja hao.

Hao kunguru waliletwa. Kuna kipindi kilirushwa na itv kuelezea uwepo wao, ni muda umepita sasa lakini nakumbuka walisema hao kunguru waliletwa Zanzibar ili waje wale uchafu, huko walikotolewa kati ya India au Uarabuni walikuwa wanakula taka, walivyofika zenji wakaanza kula misosi badala ya taka, wakaasi na kuangua na kuongezeka wakasambaa ukanda wa pwani, ukaja mpango wa kuwaua na kila kunguru mmoja atakayeuliwa ni Tshs 50/- sijui kama bado hii kazi inaendelea
 
Wakuu, nimekuwa nawaza mara kwa mara kuhusu jamii hii ya Kunguru ambao wamezagaa sasa karibu eneo lote la Pwani ya Tanzania,kuanzia Tanga hadi Mtwara. Jambo moja ninalolijua ni kwamba hawana asili ya Afrika. Wametokea India. One theory inasema walitua pwani ya Tz baada ya ku stow away ktk meli kubwa za kibiashara zilizofika Tz kutoka bara Hindi. Nyingine inasema waliletwa Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Sheikh Amani Abeid Karume alipofanya Ziara ya India in the late 60's. Alipewa zawadi ya kunguru kadhaa ili waje wazaliane as a control measure ktk mashamba ya karafuu kwani ndege hawa hula viwavi wanaoharibu zao la karafuu. Wakuu, maicologist na wanamazingira mliopo humu,hebu tujadili kama kuna faida na hasara za uwepo wa ndege hawa katika pwani ya Tz. Inasemekana wamewatimua aina ya ndege wengine wa asili katika miji yetu ya pwani,kwa ama kuwala wao wenyewe,makinda/vifaranga au mayai yao. Lakini pia ni maarufu kwa kukwapua sidiria , chupi, nepi na leso zinapokuwa zimeanikwa uani baada ya kufuliwa. Pia inasemekana wanakula uchafu jalalani hivyo wanaweza kutumika katika kazi za kusafisha mazingira ya miji. Lakini pia kwa nini wanaishi miji ya pwani tu? Je Dodoma, Arusha na Mwanza wanaonekana? Nawasilisha

...Mie pia miaka ya nyuma nimewahi kusoma katika moja ya magazeti nchini kwamba Karume Sr ndiye aliyewaingiza Zenj toka India.
 
Hao kunguru waliletwa. Kuna kipindi kilirushwa na itv kuelezea uwepo wao, ni muda umepita sasa lakini nakumbuka walisema hao kunguru waliletwa Zanzibar ili waje wale uchafu, huko walikotolewa kati ya India au Uarabuni walikuwa wanakula taka, walivyofika zenji wakaanza kula misosi badala ya taka, wakaasi na kuangua na kuongezeka wakasambaa ukanda wa pwani, ukaja mpango wa kuwaua na kila kunguru mmoja atakayeuliwa ni Tshs 50/- sijui kama bado hii kazi inaendelea

Sasa kama walipelekwa Zanzibar, huku bara si wakuja tu. Unanchekesha.
 
hao kunguru hawakuletwa na karume ila waliletwa na wabaniani ambao awali hawakupata njia ya kuteketeza miili ya maiti zao hivyo walilelta ila wale mizoga ya maiti hizo. baada ya kuona mafanikio ni madogo ndipo walipoibua wazo la kuchomana. wabillahi tawfiq
 
Mradi huu upo unaendeshwa na Wildlife Conservation Society of Tanzania, kama kwako wamezidi uwaone watakupa mitego maalum ya kuwanasa...........ofisi zao ziko Mtaa wa Ghana Avenue Mkabala na Ubalozi wa Msumbiji............kwamba wameletwa na nani sio hoja kwa sasa hoja ni kuwaangamiza maana ni kweli ni invasive species ambao wamechase ndege wengi wakiwemo wale wenye mabaka meupe (Pied Crow) Kuhusu kuenea, sasa hivi yasemekana wako zaidi ya Km 600 toka Pwani ya Dsm. Jina halisi kwa kiswahili wanaitwa Kunguru Kaya (Indian House Crow) Waliletwa kama scavenger toka India ambako ndio asili yao, si kwamba Sharif Majid aliwaleta balialishauri wachukuliwe toka India ili kupunguza kadhia ya uchafu..........na Kwa Dar walifika baada ya kuwa wanapanda maboti na meli kubwa kufuata uchafu . Rafiki mkubwa wa Kunguru Kaya ni uchafu au mizoga ndio maana utawakuta wengi sana maeneo yenye uchafu sana (sitaki kusema kwamba Uhindini kunanuka lakini wao hufuata zaidi yale mapochopocho yao ambayo ni aghalabu uswahilini) ambako udhibiti wa uchafu ni mdogo
 
dawa ni kuwala , tufanye utafiti wanaliwaje ili wawe kitoweo maana nyama ya kuku ng'ombe haikamatiki, hata hivyo waziri Kamara aliulizwa jinsi ya kuwatomeza ngedele yeye akajibu dawa ni kuwafanya kitoweo ndio watakwisha.
dawa nyingine ni kwamba kwa kuwa kunguru hawa ni waoga sana mbinu mbadala ni kila mti walalapo unafunga puto wakae wanaelea pale hawawezi kukaa wala kuzaliana wanakaa na wasiwasi hivyo watakimbia wote huku tukiendelea na utafiti wa kuwa!!
 
Nimeipenda, itabidi utuonyeshe mfano. Kunakijiji walikuwa wanasumbuliwa sana na kima, ila walipogundua nyama ya kima ni tamu, wale kima wametoweka hawaonekani tena. Yaani sasa wamezimiss sauti zao!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom