Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!

Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!

Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!

Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege

Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!

Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!

WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
 
Niliotesha karanga ekari 2, zilivyokomaa zikafukuliwa na kunguru. Sikuvuna hata kilo moja. Halafu hawaogopi Watu. Ukiwafukuza Wengine wanatua nyuma yako
Jaman kumbe wamefikia hatua ya kula pembejeo!? Huko buza wanaiba sana chupi zilizoanikwa hasa zile tandabui kama barakoa! Wanazichukua wakizani utumbo
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika.

Mabaki ya chakula hua nawawekea sehemu maalum na wakishaniona naelekea hiyo sehemu wanakuja kwa kelele kali hua natafsiri wanafurahi na kuitana, wanabeba na kula kwenye nyumba zao,

Watu wengine wanaona kero makelele yao nikagundua kinachowasumbua ni kiu cha maji.
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika...
Kwahiyo wawatekee maji ya mgao
 
Kweli kabsa wanakula vifaranga vyangu hatari! Ufugaji umekua tabu na huu ujobless wangu nashindwa zana za kuwazuia kabsa! Ukiamuua kuwafungia tu vifaranga wasitoke nje, ukuuaji wao ni wa shida sana! Siwatofautishi na Magu kabsa.
Pole sana ndiyo maana mayai ya kenyeji yamepanda bei
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija...
Wazo la kuwashughulikia kunguru weusi limenivuta nisome.Baada ya kusoma historia ya uongo kuhusu kunguru hao nasimama hapa hapa mbele siendi.
 
Wanakula mayai ya Ndege wa Asili na kupelekea kupotea kwa asilimia kubwa ya Ndege wa Asili.

Hili ni Janga kubwa.
Umeongea kitu muhimu sana mkuu, ni lazima tulinde uasili wetu ndio maana kuingia NZ au Australia wapo makini mno, kuanzia uhamiaji haramu mpaka vitu vya kuathiri uasili wao,pendekezo hizi borders zetu tuunde chombo kimoja cha kuratibu sio sasa kila mtu anafanya kazi independent,

utafiti wa kunguru hawa ulishafanyika miaka kibao nyuma huku na mpaka kukawa na mitego eti wategwe na zawadi kutolewa hasa kwa kiota chenye mayai!pale makumbusho ya taifa watu wakala pesa tu,tuingize eagles 🦅 ambao ni natural enemy wa kunguru,

Hawa watakomesha kabisa tatizo hili, hawa kunguru wametupotezea mno ndege wetu wa asili, Dar vitonga sasa ni adimu mno, shore hamna kabisa
 
Imeongea kitu muhimu sana mkuu, ni lazima tulinde uasili wetu ndio maana kuingia NZ au Australia wapo makini mno, kuanzia uhamiaji haramu mpaka vitu vya kuathiri uasili wao,pendekezo hizi borders zetu tuunde chombo kimoja cha kuratibu sio sasa kila mtu anafanya kazi independent, utafiti wa kunguru hawa ulishafanyika miaka kibao nyuma huku na mpaka kukawa na mitego eti wategwe na zawadi kutolewa hasa kwa kiota chenye mayai!pale makumbusho ya taifa watu wakala pesa tu,tuingize eagles 🦅 ambao ni natural enemy w kunguru, hawa watakomesha kabisa tatizo hili, hawa kunguru wametupotezea mno ndege wetu wa asili, Dar vitonga sasa ni adimu mno, shore hamna kabisa
Eewaah jambo la msingi umenikumbusha
 
Wazo la kuwashughulikia kunguru weusi limenivuta nisome.Baada ya kusoma historia ya uongo kuhusu kunguru hao nasimama hapa hapa mbele siendi.
Hoja kwa hoja lete ukweli wa kunguru mweusi mkuu, lengo kumtokomeza maana anapokula vifaranga habagui vifaranga kwa vyama!
Kero ni kwa wote
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika...
Daah umefanya jambo ambalo jamaa mmoja aliwahi fanya kule Yombo dovya miaka ya nyuma sana mpaka wakawa wanamwita kwa Kunguru maana aliweka sehemu ya maji na chakula na alikua kama amewafundisha awazagai hovyo wala kwenda sehemu ingine na pia nilishangaa kuona hawaogopi watu kabisaa...
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!

Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!

Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!

Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege

Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!

Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!

WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
Hili nalo nendeni mkalitizame
 
Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika...
Nilikuwa napiga stor na jamaa zangu wa arusha nikawaambia jinsi hawa kunguru wanavofungua koki ya maji na kuyaacha yamwagike, kila mtu aliniona ni muongo!

Lakini huwezi amini, baada tu ya kuwasimulia pale pale nikapata wazo la kuvunja ule mshikio wa koki uwe mdogo hivo watashidwa kuushika, mpaka leo hawafungui tena.

Zamani bomba ilibidi liwe linafunikwa na ndoo kwa juu.hawa kunguru hapa dodoma ni shida sana!
 
Wanafungua kwa midomo yao, mngekua mmewawekea chombo chao cha maji wangeacha,

Kiu ni kibaya sana unajua wao chakula wanapata kwa urahisi tu tatizo hua ni maji hasa kipindi hiki cha ukame.
 
Back
Top Bottom