Kuna wimbi la biashara ya ukahaba kwenye vyuo vikuu kupitia Instagram

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,580
10,818
Wakuu, naamini mmeakuwa na weekend njema, na mmeianza Jumatatu vyema. Back to me it was boring baada ya kukutana na hiki kisanga.

For the last six months nimekuwa mtu wa kusafiri safiri kidogo ndani ya hii Tz. Napenda sana kampani hasa maeneo ninayotembelea, hii imenifanya kujuana na watu tofauti tofauti maeneo ninayokwenda.

Kuna kipindi nilikuwa Mwanza ninaowajua pale wakawa nje ya Mwanza, baada ya siku mbili nikashindwa kuvumilia katika pitapita mtandaoni nikasaka page moja ya Instagram ya kichoko sana.

Kuna namba nikachukua nikapiga haikupokelewa nikatuma ujumbe Whatsapp ukajibiwa, zile automatic reply ukielezea huduma inayotolewa! Nikatakiwa kutuma Tsh 5000/= ili kuendelea na huduma.

Nikafanya hivyo ikachukua kama masaa 2 nilivyoona kimya nikatuma msg kukumbushia. Duh! Nikatumiwa picha kama 15 za wadada tofauti tofauti katika mapozi tofauti tofauti then nikatakiwa nichague mmoja ili nitumiwe namba.

Nilivyotumiwa namba nikapewa na maelezo nini nitakachotakiwa kufanya wakati nawasiliana na mrembo husika - it was restricted kuhoji maswali mengi.

Anyway nilijaribu kufuata masharti, nikatuma ujumbe kwa mrembo ila intention yangu haikuwa kula mzigo! Just kampani, nilivyomweleza akasema nimwambie nitamlipa bei gani kwa hiyo kampani as hawezi kuja kukaa bure.

Yule main connector alishasema hao warembo huduma yao haizidi 50k means naweza nikabagain na niliyemchagua na kama ni kudinyana nitaamua kama yeye ndio atafute sehemu au mimi mwenyewe.

Sikupenda aje hotel niliyokuwepo ili nisipate tamaa yakufanya ambacho hakikuwa in my plans.

Baada ya mazungumzo akahitaji nauli ili anifuate, nikamtumia 10k alivyokuja, nikamwambia mimi lengo langu ni kampani yake tu so anywe ale atakacho. Katika stori za hapa na pale nikagundua alikuwa Mwanachuo Mwaka wa pili, hakutumia kilevi. Mwisho nikamwachia 20k akarudi kwake maeneo ya Nyegezi.

Huu ukawa ndio mtindo nikienda mkoa wowote natuma tu message kwa main connector natuma 5k, natumiwa picha nachagua. Mahali nilipoenda mara nyingi ni Arusha ambapo pia Wanachuo nimekutana nao wachache(2) kulinganisha na maeneo mengine kama Dodoma, Iringa, Mwanza na Mbeya.

Huyu mtu wa Insta ana connection mikoa karibia yote Lindi tu, ndio alinipa mtu aliyekuwa Mtwara siku meet nae.

Na niliokutana nao ni mara chache sana nilikuwa nashiriki tendo.

Kisa cha Weekend kilichonifanya nilete huu Uzi.

Nilikuwa Dodoma, na pale kuna Dada wa kimeru Ambaye namjua nje ya connection ya mtu wa Instagram, nirafiki wa muda, na tumeshakutana hapo Dom mara kadhaa kabla hajamaliza Chuo (kamaliza this Year). Ni mtu nimemsapoti in many areas.

Last Friday akaniambia bado hajaondoka Dodoma kurudi Meru kwao as kuna mambo anafanya hapo town! Nikajua ndio kampani yangu sasa, na alikubali angenijoin jioni baada ya kumaliza mambo yake! Imefika saa 12jioni.

Nikapiga simu hakupokea, nikatuma ujumbe wa sehemu niliyopo as akiwa karibu na simu yake atanijibu. Ikafika Saa Moja kimya! Nikajaribu kupiga tena haikupokelewa.

Nikaamua kuachana nae, Nikaona isiwe shida nikaingia Whatsapp kwa Mtu wa Instagram nikatuma buku tano, ndani ya dakika 10 nitatumiwa picha za warembo waliopo nilitumia picha 9. Moja wapo ni ya yule mmeru ambaye hajapokea simu yangu.

Duh ilikujiridhisha nikamchagua yeye! Nikapewa namba, namba tofauti na ile anayotumia siku zote.
Na mimi nikatumia namba nyingine ambayo haijui, kama kawaida nikatuma ujumbe! Hapo inakaribia saa 2 usiku. Huyu nikasema ngoja nibagain nae kabisa, huwa wanauliza "Kulala au shorttime?

Nikamwambia kulala akataja 80k, guest juu yake. Nikamwambia niko Hotelini kuja yeye nitamlipaje? Tuka bargain hadi 50k. Akataka nauli, nikamwambia kuna boda najuana naye hapa namwagiza akufuate, tukakubaliana hivyo!!

Nikaona ananipigia kwenye simu yangu ya kawaida sasa na namba yake ya siku zote, alikuwa ananipa excuse yakushindwa kuja na akaomba msamaha kushindwa kupokea simu as alikuwa busy! So tusingeweza kuonana kwa madai kuna mambo yamem'bana Usiku ule akaniahidi tungeonana Jumamosi.

Kwenye saa tatu na robo boda alishaifanya kazi yake vyema kabisa, kuniletea! Alivyoniona alishtuka sana! Wala sikutaka mambo yawe mengi, nikamtaka aagize kinywaji akagoma kabisa anaomba aondoke tu, hapo tuko kwenye bar ya ile Hotel, anyway tukaenda ndani kwa ajili ya kuzungumza.

Akapata ujasiri wakunielezea scenario nzima japo uongo ulikuwa mwingi. Aliniahidi kuacha huo mchezo wakujiuza as usiku ule ule alimwomba yule mtu wa Insta amtoe kabisa kwenye connections zake.

Wanachuo wengi wanafanya hii biashara wengine sio kwa kukosa pesa, ni tamaa. Japo wengine wanafanya kwasababu ya umaskini.

Kwa hapa Dar sijui kiwango chao ila kwa Mwanza, Iringa, Dodoma, Mbeya na Kilimanjaro wapo sana in this worse business.

Take care!
 
Huwa nabisha kwamba malaya wanaojiuza ni wanachuo, hiyo hutumika kama njia ya kuvutia wateja. Nani auzwe kwa kuitwa mamantilie au msusi. Ila nilishaona wadangaji wawili chuo, jamaa yangu ndio alinihakikishia wanauza na alishawaona Riverside. Hapo ndio somehow nikakubali kwamba baadhi wanauza ila sio kwa wingi kama inavyosemekana mitandaoni
 
Huwa nabisha kwamba malaya wanaojiuza ni wanachuo, hiyo hutumika kama njia ya kuvutia wateja. Nani auzwe kwa kuitwa mamantilie au msusi. Ila nilishaona wadangaji wawili chuo, jamaa yangu ndio alinihakikishia wanauza na alishawaona Riverside. Hapo ndio somehow nikakubali kwamba baadhi wanauza ila sio kwa wingi kama inavyosemekana mitandaoni
Wanafanya kwa siri ila ndio kama hivyo.
Kuna wimbi la Wasichana wakimaliza vyuo hawarudi makwao na hawana boom na maisha yanaenda.
Wanajifanya kuishi kwa maisha ya kuuza Online vitu vidogo vidogo
 
Back
Top Bottom