Kuna wimbi kubwa la wamiliki wa Trekta hizi Hybrid kuziuza miezi michache baada ya kuzitumia au kuzikopa

Chivundu

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
7,201
5,370
Tuambiane ukweli, kwanini watu wengi wanaziuza Trekta hizi za kisasa, Mahindra, Swalaj, Tafe, New Holland TT75, miezi michache baada ya kuzitumia?

Zamani mtu akinunua trekta tegemea umuone nayo miaka kibao.
 
Tuambiane ukweli, kwanini watu wengi wanaziuza Trekta hizi za kisasa, Mahindra, Swalaj, Tafe, New Holland TT75, miezi michache baada ya kuzitumia?
Zamani mtu akinunua trekta tegemea umuone nayo miaka kibao.
Kwa haraka haraka. Hizi trekta za kisasa hazitaki janja janja kama zilivyokuwa trekta za miaka hiyo. Kila kitu ufanye kama walivyoelekeza waundaji wa trekta husika. Sasa kuzitunza kama producer mwenyewe anavyo taka, sisi huku wamiliki hatutaki maana tunaona ni gharama. Majibu yake hujitokeza baada ya muda mfupi tu.
 
Unataka John Deere uipelekeshe kama Massey Ferguson ya miaka ya 80?

Trekta za kisasa ni mitambo inayohitaji uhalisia wa service na spare genuine.

Wabongo tunapenda janja janja ndiyo maana baadhi ya brand za kisasa hazidumu kwa sababu ya kutozingatia utaratibu wa service, uendeshaji, aina ya oil na spare husika.

Kuna haya John Deere yaliletwa na serikali Toka USA kutumika huku Kambi za JKT katika kilimo. Mengi yalianza kufa mpka wakaletwa watu USA Toka John Deere kutoa seminar kwa madereva/operators na mafundi ndipo yakafufuka.
 
Back
Top Bottom