Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,157
Kwa sasa serikali ina wastani wa watumishi 700k, sekta binafsi wenye mikataba ya maana ni kama millioni 1 tu.
Tuseme hivi waajiriwa wenye maslahi angalau hapa nchini ni kama millioni 2 tu.
Wengi ni vibarua, nikimaanisha wengi wana mikataba mifupi .
Idadi ya wasomi inaongezeka kila leo.
Zamani ukiwa na diploma unaonekana msomi, sasa hivi hata wenye bachelor wanakaribia kuondolewa au kujiondoa kwenye kundi la wasomi.
Mtoto anamaliza darasa la 7, form 4, 6 au chuo mzazi alipaswa kumfundisha maisha ya kujitegemea.
Kuna kilimo, biashara au ufundi stadi.
Huyu mtoto baadaye akifika level ya juu ya elimu kama hataajiriwa kwa mkataba wenye maslahi hatakubali kuwa mtumwa kwa kuajiriwa mikataba ya hovyo. Badala yake atatumia kile alichofundishwa na mzazi wake. Ataanza hata kufuga kuku 20 wa mayai kuliko kwenda kufanya vibarua vya kitumwa.
Sasa mtoto humjengi katika msingi wowote unategemea nini ?
Hawa ndio wale wanapita kuzunguka na bahasha Kila siku. Mtu ana shahada ya uhandisi mitambo anakuambia nisaidie hata kazi ya usafi nipate hali ngumu.
Miaka 4 yako ya chuo ni void?
Ungetaka kazi ya usafi si ungeenda VETA upige miezi 3 fresh .
Mimi nimeanza kumfundisha mwanangu kuuza duka weekend na siku za kazi jioni amwagilie bustani ya mbogamboga na kulishia kuku.
Kuna wahitimu wengi wa degree wanafanya kazi za kulipwa 5000/=kwa siku. Huruma