Kuna uraibu wa vyakula vya nazi? Chakula cha nazi ni bora sana tofauti na kisicho na nazi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,276
Kuna baadhi ya watu wanapikia nazi kila chakula, yani chakula hawawezi kupika au kula bila kuweka nazi.

Unaweza kukua katika mlo mmoja amepika wala wa nazi, nyama ina nazi, maharage ya nazi na mboza za majani za nazi. Akipika mihogo anaweka nazi, ndizi nazi, makanda nazi n.k.

Huwa nasikia watu hasa wa pwani wanavyosifia chakula cha nazi mpaka wanatokwa udenda nabaki kuduwaa kwa sababu sijawahi kuiona ikiwa kiungo cha maana sana cha chakula.
 
umeuliza kitu ambacho kipo wazi sana. kwetu nazi ni kiungo cha heshima sana.

nikienda kumtembelea bi mkubwa, nikikaa siku 3 anaweza tumia nazi hata 10 kuanzia mboga mpaka wali wenyewe.

mambo hayo yanapatikana sana pwani especially Tanga.
Haukinai?
 
Nyama kuweka nazi ni makosa makubwa, lakini hakuna wali mtamu duniani kama wa nazi.....umkute anayejua kupika. Hakuna mboga tamu kama kisamvu, mrongi ulioungwa na nazi. Ile harufu yake tu kwanza ukiisikia.....roho kwatu kabisa
 
Back
Top Bottom