Kuna umuhimu wa mimi kupiga kura tena?

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,012
95,359
Wadau naomba Ushauri wenu. Nafikiria kuacha kupiga kura kwa kuwa tangu nianze kupiga kura, sijawahi kumchagua aliyeshinda. Sasa naona kuliko kupiga kura wakati nayempigia kura huwa hashindi, ni kama kupoteza muda wangu bure. Labda ushauri wenu unaweza kunisaidia.

Hebu angalia mlolongo huu:
Mwaka 1995 Nilimpigia Mrema, akashinda Mkapa.(CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia Lipumba akashinda tena Mkapa.(CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia Mbowe akashinda Kikwete.(CCM)

Kwa Upande wa wabunge
Mwaka 1995 Nilimpigia mgombea wa NCCR Mageuzi akashinda Keenja (CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia mgombea wa TLP akashinda Ritha Mlaki (CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia mgombea wa CHADEMA akashinda Ritha Mlaki (CCM)

Sasa niendelee kupiga kura au niache? Nauliza kwa kuwa nina allergy ya kukipigia kura CCM na ninapowapigia wapinzani huwa hawashindi.
 
Kupiga kura ni haki yako . na kwa kila unayemchagua kushindwa basi hapo umeonyesha upinzani kwa yule aliyeshinda. Kwani kama mgombea alishinda kwa let say 56% , next time atajitahidi ashinde kwa kishindo zaiidi.

Bila upinzani hawa wagombea watabweteka.

nakushauri usiache kupiga kura.
 
Demokrasi siyo kamari eti utabahatisha wakati fulani ushinde.You backed a losing horse and lost.Jaribu kuweka perspectives zako kisawasawa na kuona kama kuna uwezekano wa kambi ya upinzani kushinda.In Zenj yes, bara kura yako is not wasted lakini ni "pima joto" kwa chama kilicho madarakani.
 
Vote yako ni wasted vote, yaani wewe ni hoi ile mbaya. Miaka 15 wewe unachagua watu bomu tupu?

Uko jimbo gani nikusaidie kuchagua mtu wa kumpa kura yako 2010?

Ukiendelea na tabia ya kuwa kilaza wa kuchagua watu bomu, hata mke utachagua bomu!

Mimi 2000 nilichemka wote urais na MP. Mwaka 2005 nikajifunza na nikachagua washindi, ila wote wamekuwa bomu, bora ningelilala nisiende kwenye uchaguzi.

Inaniumiza kwamba kura yangu ilisaidia kuleta majitu hovyo hovyo!
 
Afadhali yako kaka, Mie sijawahi kupiga kura Neither CMM nor Upinzania,Ila najipanga mwakani,piga ua Lazima upande wangu itashinda.
Ushauri wangu kwako ni "kukata tamaa ni sawa na kusema Mungu hayupo" Keep trying may be one day upande wako itashinda.
 
Vote yako ni wasted vote, yaani wewe ni hoi ile mbaya. Miaka 15 wewe unachagua watu bomu tupu?

Uko jimbo gani nikusaidie kuchagua mtu wa kumpa kura yako 2010?

Ukiendelea na tabia ya kuwa kilaza wa kuchagua watu bomu, hata mke utachagua bomu!

Mimi 2000 nilichemka wote urais na MP. Mwaka 2005 nikajifunza na nikachagua washindi, ila wote wamekuwa bomu, bora ningelilala nisiende kwenye uchaguzi.

Inaniumiza kwamba kura yangu ilisaidia kuleta majitu hovyo hovyo!

Engineer amefulia hana jipya kabisa zaidi ya kuomba omba hisani kwa wagombea kule Kyela tumemfukuza!
 
Engineer amefulia hana jipya kabisa zaidi ya kuomba omba hisani kwa wagombea kule Kyela tumemfukuza!

Anasubili kupewa laptop kama takrima.
Umesikia na kwa Mwandosya nako kuna kajamaa kameenda kanataka kumng'oa Prof.
 
I suggest uache kupiga kura uangalie njia nyingine nyingi za kujiongezea kipato!
 
Kwa Tanzania hakuna muhimu wowote wa kupiga kura ni kupoteza wakani Nec ama tume ya uchaguzi ya taifa (i mean ya CCM ) ndio inayochaguwa nani awe raisi nani awe mbunge kwa matakwa ya CCM kuna majimbo mengine hata kura ya mbunge mwenyewe haionekani. bro usipoteze wakati wako bure kwa usanii wa CCM.
 
kupiga kura ni haki yako ya msingi, na ukumbuke kura yako inaweza kuleta mabadiliko ya kweli
 
Mie sijaamua kama 2010 nipige kura au lah bado sijaona wa kumpigia ,kwa hiyo wewe una hiari ya kupiga kura au kutokupiga ,mradi tu iwe na manufaa kwako
 
Mie sijaamua kama 2010 nipige kura au lah bado sijaona wa kumpigia ,kwa hiyo wewe una hiari ya kupiga kura au kutokupiga ,mradi tu iwe na manufaa kwako

Ndo nyie mnachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza haki zenu na kuacha watu wanawachagua viongozi wabovu wasio na sifa.
 
mi nakushauri usipige kura. Imagine unapanga foleni siku nzima unaungua na jua eti unapiga kura, then akishinda ukliyemoigia anakupa tena headache ya kukaa hapa JF na kulalamika juu ya ufisadi, njaa, elimu mbovu , uchumi mbaya, shida kbao, what for. I will nebver vote again, and i dont care, nasaka feza tu ndo kilichobaki ili nirekebishe mambo yangu.
 
Ndo nyie mnachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza haki zenu na kuacha watu wanawachagua viongozi wabovu wasio na sifa.

Fidel80
kutoka moyoni kila nikiangalia viongozi walioko madarakani hakuna hata mmoja alieniridhisha na utendaji wake wa kazi

Nina sababu zipi za msingi zitakazonifanya nikapange foleni ya kupiga kura kisa cha kufaint katika mstari ni nini??
 
Wadau naomba Ushauri wenu. Nafikiria kuacha kupiga kura kwa kuwa tangu nianze kupiga kura, sijawahi kumchagua aliyeshinda. Sasa naona kuliko kupiga kura wakati nayempigia kura huwa hashindi, ni kama kupoteza muda wangu bure. Labda ushauri wenu unaweza kunisaidia.

Hebu angalia mlolongo huu:
Mwaka 1995 Nilimpigia Mrema, akashinda Mkapa.(CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia Lipumba akashinda tena Mkapa.(CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia Mbowe akashinda Kikwete.(CCM)

Kwa Upande wa wabunge
Mwaka 1995 Nilimpigia mgombea wa NCCR Mageuzi akashinda Keenja (CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia mgombea wa TLP akashinda Ritha Mlaki (CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia mgombea wa CHADEMA akashinda Ritha Mlaki (CCM)

Sasa niendelee kupiga kura au niache? Nauliza kwa kuwa nina allergy ya kukipigia kura CCM na ninapowapigia wapinzani huwa hawashindi.
why should you do that?
HELL NO!
 
Fidel80
kutoka moyoni kila nikiangalia viongozi walioko madarakani hakuna hata mmoja alieniridhisha na utendaji wake wa kazi

Nina sababu zipi za msingi zitakazonifanya nikapange foleni ya kupiga kura kisa cha kufaint katika mstari ni nini??

Ndo hapo elimisha ndugu zako jamaa zake hata mmeo jinsi ya kuchagua viongozi bora waambie wazi huyu tulimchagua chaguzi iliyo pita hajafanya lolote piga kampeni chini kwa chini mpigeni chini chagueni kiongozi bora sio bora kiongozi kwa vile kasimamishwa na CCM.
 
Engineer amefulia hana jipya kabisa zaidi ya kuomba omba hisani kwa wagombea kule Kyela tumemfukuza!
sas masalilo na rafiki yangu fidel, mnanipa hofu kidogo, mimi nilikuwa namuona injia kama mwanamapinduzi. sasa kama ndio hivi labda mnipe ufafanuzi kidogo. japo najua kuwa injinia atajibu soon. na mjadala unaweza kuwa mrefu?
sometime anajionyesha ni mshabiki wa mwakalinga lakini kuna wakati anakuja kama mtu wa kusapoti mtu yeyote ambaye atakuwa against mwakyembe. hivi vipi kuhusu huyu jamaa sikonge? sijui kama mnampata. wanaunity sana na injinia. nahisi atajitokeza hapo kumtetea injinia
 
Engineer amefulia hana jipya kabisa zaidi ya kuomba omba hisani kwa wagombea kule Kyela tumemfukuza!

Masanilo,

Hivi huna dada? Ili uache kumwandama engineer wa bush, inabidi nitongoze dada yako. Si unaona Malafyale hasemi tena baada ya engineer kushinda pale kwa mtoto wao?

Nyie mmekimbia nchi shauri ya shida na kutuachia sisi wanyonge tuendelee kuteseka. Mwakani nimejiandaa, sichagui tena mijitu ya hovyo hovyo.

Wacha niwake kikao cha vijana saa tisa tukapange mikakati ya 2010.

Weekend njema.
 
Wadau naomba Ushauri wenu. Nafikiria kuacha kupiga kura kwa kuwa tangu nianze kupiga kura, sijawahi kumchagua aliyeshinda. Sasa naona kuliko kupiga kura wakati nayempigia kura huwa hashindi, ni kama kupoteza muda wangu bure. Labda ushauri wenu unaweza kunisaidia.

Hebu angalia mlolongo huu:
Mwaka 1995 Nilimpigia Mrema, akashinda Mkapa.(CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia Lipumba akashinda tena Mkapa.(CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia Mbowe akashinda Kikwete.(CCM)

Kwa Upande wa wabunge
Mwaka 1995 Nilimpigia mgombea wa NCCR Mageuzi akashinda Keenja (CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia mgombea wa TLP akashinda Ritha Mlaki (CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia mgombea wa CHADEMA akashinda Ritha Mlaki (CCM)

Sasa niendelee kupiga kura au niache? Nauliza kwa kuwa nina allergy ya kukipigia kura CCM na ninapowapigia wapinzani huwa hawashindi.

Kupiga kura ni muhimu, USIACHE. Kuacha kupiga kura ni kuhalalisha wapiga kura wenzako wakuchagulie kiongozi wako mia kwa mia. Sasa jiulize, je yule mlevi anayesumbua kila usiku mtaani akipigana na mkewe ndio mwenye hekima ya kukuchagulia wewe kiongozi wako? Hapana. Je yule kibaka mvuta bangi aliyeshindikana, baada ya kuhongwa tshirt, ndiye mwenye busara kuliko wewe ya kujua mgombea yupi anafaa kuwa kiongozi? Hapana.

Kupiga kura ni hatua ya kwanza katika kuhakikisha tunapata viongozi wazuri. Lakini tusiishie hapo. Tunatakiwa tudai kuwe na uchaguzi ulio huru na wa haki. Yaani mgombea ambaye anakubalika na wengi ndio mwisho wa siku anatangazwa kuwa mshindi. Tunatakiwa kudai sheria za uchaguzi ziboreshwe ili wagombea wote watendewe haki. Mfano pawepo na ukomo wa matumizi ya pesa kwenye kampeni za uchaguzi na kila mgombea atueleze hizo pesa amezitoa wapi. Hii itazuia watu wenye pesa ambao hawakubaliki kutumia udhaifu wa watu maskini kuwarubuni wakati wa uchaguzi.

Aidha, Kwa ujumla wetu tunatakiwa kuishinikiza Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kila mwananchi apate fursa ya kupambanua kwa uhuru kabisa ni mgombea yupi anayefaa na haki itendeke kura yake ihesabike. Kuna mapungufu mengi katika chaguzi zetu lakini NEC inayafumbia macho kwa makusudi kabisa. Mapungufu haya yakiondolewa CCM haitakuwa inashinda kwa kiulani kama ilivyo sasa. Kwa kuwa viongozi wa NEC wanateuliwa na rais basi wameamua kula ngumu. Tunatakiwa tudai kuwe na Tume ya Uchaguzi iliyo huru na itakayoshirikisha wadau wote.

Mapungufu yako mengi nitataja kadha. Mfano NEC bado inang'ang'ania kwamba kura lazima zihesabiwe ndani ya majengo/majumba ya serikali kama vile mashuleni na kwenye zahanati. Kwa mijini hi ni sawa lakini huko vijijini huu ni usumbufu mkubwa. Utakuta kwenye kituo kimoja kumeandikishwa wapiga kura elfu mbili au zaidi ambao wametapakaa katika kila kona ya kijiji. Sasa mwananchi wa kijijini akitaka kupiga kura ni lazima atembee umbali mrefu wengine hata kilomita kumi na zaidi. Hii inakatisha tamaa. CCM kwa vile wana pesa wanakodi malori kusafirisha wapiga kura wao siku ya uchaguzi (Biharamulo). Nchi zingine za Afrika ambazo ni maskini kama sisi wameshaachana na huu mtindo. Kwa mfano Ghana wanapiga kura msimu ambao sio wa mvua na kura zinahesabiwa chini ya mti kwa uwazi kabisa mbele ya kadamnasi. Hivyo kila Kitongoji kinakuwa na kituo chake cha kupiga kura na wanaojitokeza kupiga kura ni asilimia kubwa.

NEC vilevile imekataa kujihusisha na kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura. Utawezaje kuwa na mpango unaotumia mabilioni ya fedha wakati wanaohusishwa na huo mpango ni mambumbumbu kuhusu mpango wenyewe? Mgombea anapanda jukwaani anatishia na kusema wapinzani hawajashika dola hivyo mkiwachagua serikali haitaleta maendeleo na wao wanaamini. NEC iko kimya. Mabalozi na Madiwani wanapita mtaani kukusanya shahada za wapiga kura in exchange na vocha za mbolea (Mbeya Vijijini). Mabalozi wa nyumba kumikumi wanajua wapinzani ni akina nani na wanajua ni shahada zipi za kukusanya. Wanakamatwa red-handed (Busanda) wanapelekwa polisi, NEC wanasema hilo haliwahusu ni kosa la jinai, wanakataa kutoa ushirikiano, kesi zinafutwa kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha. Madhehebu ya kidini (TUCTA wako mbioni) wameliona hilo ombwe lililotengenezwa na NEC na sasa wametoa waraka unaotoa elimu ya kiraia, huu ni mwanzo mzuri sana. Kingunge ingefaa aelekeza nguvu zake katika kuikarapia NEC kutotimiza wajibu wake mpaka imefikia pahali inaanza kuingiliwa kazi yake.

Sasa NEC wanatuambia hawajui kwanini asilimia 40% (mpaka 60% kwenye chaguzi ndogo) ya waliojiandikisha hawapigi kura. Wamepanga kuleta kampuni ya kigeni ije ifanye utafiti. Hawa wazungu wasiojua siasa za Tanzania waende huko vijijini wakapokelewe na haohao mabalozi wa nyumba kumikumi waonyeshwe ni akina nani wakuwahoji. Majibu ya huo utafiti tayari wengine tunayajua. Tunaendelea kupoteza kodi zetu kwa mambo ya kifisadi yasioyokuwa na tija kwetu. Hamtoi elimu ya uraia halafu mnashangaa kwanini watu hawapigi kura? Hivi ni vichekesho.

Ndugu Chrispin sina lengo la kukukatisha tamaa ila naona ni muhimu kueleza hali halisi ikoje maana wengi hawaifahamu. Lakini cha msingi ni kwamba tunatakiwa tuongeze nguvu na sio kukata tamaa. Haya mazuri tunayoyataka hututaletewa kwenye kisahani, inabidi tuwe ngangari. Kwani huwezi kudai haki haitendeki wakati umejitoa kwenye mchakato wenyewe ambao unaiminya hiyo haki. Tupige kura, tuhamasishe wengine nao waende kupiga kura, ambao hawajajiandikisha tuwahimize wakajiandikishe, tuelemishe wasiofahamu ni nini elimu ya uraia na mwisho tudai tume huru na sheria za uchaguzi zinazotoa haki ili yule wengi wetu tunayemtaka ndiye mwisho wa siku awe kiongozi wetu.
 
Back
Top Bottom