Kuna umuhimu wa mimi kupiga kura tena?

Kupiga kura ni muhimu, USIACHE. Kuacha kupiga kura ni kuhalalisha wapiga kura wenzako wakuchagulie kiongozi wako mia kwa mia. Sasa jiulize, je yule mlevi anayesumbua kila usiku mtaani akipigana na mkewe ndio mwenye hekima ya kukuchagulia wewe kiongozi wako? Hapana. Je yule kibaka mvuta bangi aliyeshindikana, baada ya kuhongwa tshirt, ndiye mwenye busara kuliko wewe ya kujua mgombea yupi anafaa kuwa kiongozi? Hapana.

Kupiga kura ni hatua ya kwanza katika kuhakikisha tunapata viongozi wazuri. Lakini tusiishie hapo. Tunatakiwa tudai kuwe na uchaguzi ulio huru na wa haki. Yaani mgombea ambaye anakubalika na wengi ndio mwisho wa siku anatangazwa kuwa mshindi. Tunatakiwa kudai sheria za uchaguzi ziboreshwe ili wagombea wote watendewe haki. Mfano pawepo na ukomo wa matumizi ya pesa kwenye kampeni za uchaguzi na kila mgombea atueleze hizo pesa amezitoa wapi. Hii itazuia watu wenye pesa ambao hawakubaliki kutumia udhaifu wa watu maskini kuwarubuni wakati wa uchaguzi.

Aidha, Kwa ujumla wetu tunatakiwa kuishinikiza Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kila mwananchi apate fursa ya kupambanua kwa uhuru kabisa ni mgombea yupi anayefaa na haki itendeke kura yake ihesabike. Kuna mapungufu mengi katika chaguzi zetu lakini NEC inayafumbia macho kwa makusudi kabisa. Mapungufu haya yakiondolewa CCM haitakuwa inashinda kwa kiulani kama ilivyo sasa. Kwa kuwa viongozi wa NEC wanateuliwa na rais basi wameamua kula ngumu. Tunatakiwa tudai kuwe na Tume ya Uchaguzi iliyo huru na itakayoshirikisha wadau wote.

Mapungufu yako mengi nitataja kadha. Mfano NEC bado inang'ang'ania kwamba kura lazima zihesabiwe ndani ya majengo/majumba ya serikali kama vile mashuleni na kwenye zahanati. Kwa mijini hi ni sawa lakini huko vijijini huu ni usumbufu mkubwa. Utakuta kwenye kituo kimoja kumeandikishwa wapiga kura elfu mbili au zaidi ambao wametapakaa katika kila kona ya kijiji. Sasa mwananchi wa kijijini akitaka kupiga kura ni lazima atembee umbali mrefu wengine hata kilomita kumi na zaidi. Hii inakatisha tamaa. CCM kwa vile wana pesa wanakodi malori kusafirisha wapiga kura wao siku ya uchaguzi (Biharamulo). Nchi zingine za Afrika ambazo ni maskini kama sisi wameshaachana na huu mtindo. Kwa mfano Ghana wanapiga kura msimu ambao sio wa mvua na kura zinahesabiwa chini ya mti kwa uwazi kabisa mbele ya kadamnasi. Hivyo kila Kitongoji kinakuwa na kituo chake cha kupiga kura na wanaojitokeza kupiga kura ni asilimia kubwa.

NEC vilevile imekataa kujihusisha na kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura. Utawezaje kuwa na mpango unaotumia mabilioni ya fedha wakati wanaohusishwa na huo mpango ni mambumbumbu kuhusu mpango wenyewe? Mgombea anapanda jukwaani anatishia na kusema wapinzani hawajashika dola hivyo mkiwachagua serikali haitaleta maendeleo na wao wanaamini. NEC iko kimya. Mabalozi na Madiwani wanapita mtaani kukusanya shahada za wapiga kura in exchange na vocha za mbolea (Mbeya Vijijini). Mabalozi wa nyumba kumikumi wanajua wapinzani ni akina nani na wanajua ni shahada zipi za kukusanya. Wanakamatwa red-handed (Busanda) wanapelekwa polisi, NEC wanasema hilo haliwahusu ni kosa la jinai, wanakataa kutoa ushirikiano, kesi zinafutwa kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha. Madhehebu ya kidini (TUCTA wako mbioni) wameliona hilo ombwe lililotengenezwa na NEC na sasa wametoa waraka unaotoa elimu ya kiraia, huu ni mwanzo mzuri sana. Kingunge ingefaa aelekeza nguvu zake katika kuikarapia NEC kutotimiza wajibu wake mpaka imefikia pahali inaanza kuingiliwa kazi yake.

Sasa NEC wanatuambia hawajui kwanini asilimia 40% (mpaka 60% kwenye chaguzi ndogo) ya waliojiandikisha hawapigi kura. Wamepanga kuleta kampuni ya kigeni ije ifanye utafiti. Hawa wazungu wasiojua siasa za Tanzania waende huko vijijini wakapokelewe na haohao mabalozi wa nyumba kumikumi waonyeshwe ni akina nani wakuwahoji. Majibu ya huo utafiti tayari wengine tunayajua. Tunaendelea kupoteza kodi zetu kwa mambo ya kifisadi yasioyokuwa na tija kwetu. Hamtoi elimu ya uraia halafu mnashangaa kwanini watu hawapigi kura? Hivi ni vichekesho.

Ndugu Chrispin sina lengo la kukukatisha tamaa ila naona ni muhimu kueleza hali halisi ikoje maana wengi hawaifahamu. Lakini cha msingi ni kwamba tunatakiwa tuongeze nguvu na sio kukata tamaa. Haya mazuri tunayoyataka hututaletewa kwenye kisahani, inabidi tuwe ngangari. Kwani huwezi kudai haki haitendeki wakati umejitoa kwenye mchakato wenyewe ambao unaiminya hiyo haki. Tupige kura, tuhamasishe wengine nao waende kupiga kura, ambao hawajajiandikisha tuwahimize wakajiandikishe, tuelemishe wasiofahamu ni nini elimu ya uraia na mwisho tudai tume huru na sheria za uchaguzi zinazotoa haki ili yule wengi wetu tunayemtaka ndiye mwisho wa siku awe kiongozi wetu.

Umenena kuongeza ni kuharibu tutafakari hizi bold zikifanyiwa kazi anachotaka chrispin kitakuwa
 
I suggest uache kupiga kura uangalie njia nyingine nyingi za kujiongezea kipato!

Nakushukuru mdau kwa point yako nzuri, haiwezekani kila siku nikawa looser halafu niendelee kuhangaika na kupiga kura.
 
Piga kura my pal.
Every vote counts, hata kama jamaa hatashinda..

Inauma sana, unampigia kura mtu anayeamini anakufaa. Na mazingira yanaonyesha atapata ushindi wa kishindo. Badala yake linashinda lijitu jingine, halina jipya.
 
mi nakushauri usipige kura. Imagine unapanga foleni siku nzima unaungua na jua eti unapiga kura, then akishinda ukliyemoigia anakupa tena headache ya kukaa hapa JF na kulalamika juu ya ufisadi, njaa, elimu mbovu , uchumi mbaya, shida kbao, what for. I will nebver vote again, and i dont care, nasaka feza tu ndo kilichobaki ili nirekebishe mambo yangu.

Umevaa viatu vyangu mkuu.
 
Kupiga kura ni muhimu, USIACHE. Kuacha kupiga kura ni kuhalalisha wapiga kura wenzako wakuchagulie kiongozi wako mia kwa mia. Sasa jiulize, je yule mlevi anayesumbua kila usiku mtaani akipigana na mkewe ndio mwenye hekima ya kukuchagulia wewe kiongozi wako? Hapana. Je yule kibaka mvuta bangi aliyeshindikana, baada ya kuhongwa tshirt, ndiye mwenye busara kuliko wewe ya kujua mgombea yupi anafaa kuwa kiongozi? Hapana.

Aidha, Kwa ujumla wetu tunatakiwa kuishinikiza Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kila mwananchi apate fursa ya kupambanua kwa uhuru kabisa ni mgombea yupi anayefaa na haki itendeke kura yake ihesabike. Kuna mapungufu mengi katika chaguzi zetu lakini NEC inayafumbia macho kwa makusudi kabisa. Mapungufu haya yakiondolewa CCM haitakuwa inashinda kwa kiulani kama ilivyo sasa. Kwa kuwa viongozi wa NEC wanateuliwa na rais basi wameamua kula ngumu. Tunatakiwa tudai kuwe na Tume ya Uchaguzi iliyo huru na itakayoshirikisha wadau wote.

Mapungufu yako mengi nitataja kadha. Mfano NEC bado inang'ang'ania kwamba kura lazima zihesabiwe ndani ya majengo/majumba ya serikali kama vile mashuleni na kwenye zahanati. Kwa mijini hi ni sawa lakini huko vijijini huu ni usumbufu mkubwa. Utakuta kwenye kituo kimoja kumeandikishwa wapiga kura elfu mbili au zaidi ambao wametapakaa katika kila kona ya kijiji. Sasa mwananchi wa kijijini akitaka kupiga kura ni lazima atembee umbali mrefu wengine hata kilomita kumi na zaidi. Hii inakatisha tamaa. CCM kwa vile wana pesa wanakodi malori kusafirisha wapiga kura wao siku ya uchaguzi (Biharamulo). Nchi zingine za Afrika ambazo ni maskini kama sisi wameshaachana na huu mtindo. Kwa mfano Ghana wanapiga kura msimu ambao sio wa mvua na kura zinahesabiwa chini ya mti kwa uwazi kabisa mbele ya kadamnasi. Hivyo kila Kitongoji kinakuwa na kituo chake cha kupiga kura na wanaojitokeza kupiga kura ni asilimia kubwa.

NEC vilevile imekataa kujihusisha na kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura. Utawezaje kuwa na mpango unaotumia mabilioni ya fedha wakati wanaohusishwa na huo mpango ni mambumbumbu kuhusu mpango wenyewe? Mgombea anapanda jukwaani anatishia na kusema wapinzani hawajashika dola hivyo mkiwachagua serikali haitaleta maendeleo na wao wanaamini. NEC iko kimya. Mabalozi na Madiwani wanapita mtaani kukusanya shahada za wapiga kura in exchange na vocha za mbolea (Mbeya Vijijini). Mabalozi wa nyumba kumikumi wanajua wapinzani ni akina nani na wanajua ni shahada zipi za kukusanya. Wanakamatwa red-handed (Busanda) wanapelekwa polisi, NEC wanasema hilo haliwahusu ni kosa la jinai, wanakataa kutoa ushirikiano, kesi zinafutwa kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha. Madhehebu ya kidini (TUCTA wako mbioni) wameliona hilo ombwe lililotengenezwa na NEC na sasa wametoa waraka unaotoa elimu ya kiraia, huu ni mwanzo mzuri sana. Kingunge ingefaa aelekeza nguvu zake katika kuikarapia NEC kutotimiza wajibu wake mpaka imefikia pahali inaanza kuingiliwa kazi yake.

Sasa NEC wanatuambia hawajui kwanini asilimia 40% (mpaka 60% kwenye chaguzi ndogo) ya waliojiandikisha hawapigi kura. Wamepanga kuleta kampuni ya kigeni ije ifanye utafiti. Hawa wazungu wasiojua siasa za Tanzania waende huko vijijini wakapokelewe na haohao mabalozi wa nyumba kumikumi waonyeshwe ni akina nani wakuwahoji. Majibu ya huo utafiti tayari wengine tunayajua. Tunaendelea kupoteza kodi zetu kwa mambo ya kifisadi yasioyokuwa na tija kwetu. Hamtoi elimu ya uraia halafu mnashangaa kwanini watu hawapigi kura? Hivi ni vichekesho.

Ndugu Chrispin sina lengo la kukukatisha tamaa ila naona ni muhimu kueleza hali halisi ikoje maana wengi hawaifahamu. Lakini cha msingi ni kwamba tunatakiwa tuongeze nguvu na sio kukata tamaa. Haya mazuri tunayoyataka hututaletewa kwenye kisahani, inabidi tuwe ngangari. Kwani huwezi kudai haki haitendeki wakati umejitoa kwenye mchakato wenyewe ambao unaiminya hiyo haki. Tupige kura, tuhamasishe wengine nao waende kupiga kura, ambao hawajajiandikisha tuwahimize wakajiandikishe, tuelemishe wasiofahamu ni nini elimu ya uraia na mwisho tudai tume huru na sheria za uchaguzi zinazotoa haki ili yule wengi wetu tunayemtaka ndiye mwisho wa siku awe kiongozi wetu.

Kwa mantiki hiyo ndugu yangu, bila mabadiliko katika tume ya uchaguzi na kuyafanyia marekebisho mapungufu yote, kuna sababu gani ya kupiga kura? Sio wizi huu? Kwanini nipige kura wakati najua fika hata nifanyeje mgombea nayeona anafaa hatashinda?
 
mimi nazani wewe ndio unajua lipi bora
1. kati ya ambaye hujampigia kura na ameshinda je umeona kuna mambo ya maana aliyo fanya.
2 kama kuna mambo ya maana aliyo fanya je huyo uliye mtaka je angeweza kufanya zaidi yake. kama ameweza kufanya zaidi yake itabidi ujutie ila kama hajafanya na ameharibu zaidi nazani inabidi ujivunie sana kwa machaguo yako.

kwa mfano mimi nipo kama wewe hakuna ambaye nilisha wahi kumpigia akashinda ila mpaka sasa hivyi nafarijika kuwa katika haya madudu yanayo fanya na viongozi walio kuwa madarakani mimi sikuwapendekeza wala kushiriki kuwaweka. ingawa naumia ila ningeumia zaidi kama kura yangu ndiyo ingekuwa imechangia kumuweka.

kitendo cha kuacha kupiga kura ni kibaya zaidi kwa mfano uliye mtaka angeshidwa kwa kura moja nazani ungejisika vibaya sana na ungeihukumu hiyo siku kwa kufanya kosa kushiriki kufanya kosa la kihistoria
piga kura kwa unayezani atakuletea maendeleo yako na ya tanzania sio kwa unaye zani atashinda. na kama unayezani atakaye kuletea maendeleo ana possibility ndogo ya kushinda ni jukumu lako kusaidia ili aweze kushinda kwa mfano unaweza kuwashawishi watu kwa nini huyo ni bora zaidi ya huyo mwingine. mpaka hapo utakuwa umefanya majukumu yako yote na hakuna atakaye kulaumu katika kizazi hiki na vyingine vyijavyo ndugu yangu.
 
Mkuu,tupo sawa kabitha..
Mi pia nimeanza kupiga kura 2000,kunzia diwani,mbunge,mpaka rais wote niliwapigia wapinzani,wakakosa....2005 zoezi likawa vilevile,wakakosa......
Sikati tamaa kamwe mkuu,nitaendelea kupiga kura kwa wapinzani km wagombea wao watakuwa wakiniridhisha kwa sera.km sera mbovu, nalala home,lakini ccm nooooooo1

mkuu endelelea kupiga kura,hivi ni vita usirudi nyuma,daima nenda mbele..ukirudi tu umewapa mwanya maadui.
 
Kinachokera ni kupoteza muda wangu bure. Nasimama kwenye foleni kutwa nzima nampigia kura mpiganaji lakini anapigwa mweleka wa kifisadi. Heri angeshindwa kihalali ningeelewa, lakini anashindwa kwa wizi wa kura!
 
mimi nazani wewe ndio unajua lipi bora
1. kati ya ambaye hujampigia kura na ameshinda je umeona kuna mambo ya maana aliyo fanya.
2 kama kuna mambo ya maana aliyo fanya je huyo uliye mtaka je angeweza kufanya zaidi yake. kama ameweza kufanya zaidi yake itabidi ujutie ila kama hajafanya na ameharibu zaidi nazani inabidi ujivunie sana kwa machaguo yako.

kwa mfano mimi nipo kama wewe hakuna ambaye nilisha wahi kumpigia akashinda ila mpaka sasa hivyi nafarijika kuwa katika haya madudu yanayo fanya na viongozi walio kuwa madarakani mimi sikuwapendekeza wala kushiriki kuwaweka. ingawa naumia ila ningeumia zaidi kama kura yangu ndiyo ingekuwa imechangia kumuweka.

kitendo cha kuacha kupiga kura ni kibaya zaidi kwa mfano uliye mtaka angeshidwa kwa kura moja nazani ungejisika vibaya sana na ungeihukumu hiyo siku kwa kufanya kosa kushiriki kufanya kosa la kihistoria
piga kura kwa unayezani atakuletea maendeleo yako na ya tanzania sio kwa unaye zani atashinda. na kama unayezani atakaye kuletea maendeleo ana possibility ndogo ya kushinda ni jukumu lako kusaidia ili aweze kushinda kwa mfano unaweza kuwashawishi watu kwa nini huyo ni bora zaidi ya huyo mwingine. mpaka hapo utakuwa umefanya majukumu yako yote na hakuna atakaye kulaumu katika kizazi hiki na vyingine vyijavyo ndugu yangu.

1.Walioshinda hakuna hata moja la maana walilofanya zaidi ya kuongeza kero
2. Hakuna jema alilofanya kwa hiyo naamini hakustahili kuchaguliwa. Niliyempigia kura angefanya mazuri zaidi ya aliyeshinda kiwiziwizi.
 
Mie mwakani kura yangu ninampa Kingunge Ngombale Mwiru maana hataki kustaafu ila anataka kufia pale mjengoni.
 
kama walio shinda wameharibu kwanza hongera sana na inabidi ujipongeze sana kwani wewe hujahusika kwenye kuwaweka viongozi wabaya madarakani kwa hiyo hutahukumiwa kwa hilo (ninaposema kuhukumiwa ni naama nafsi yako haita kuhukumu wala laana ya vyizazi vijavyo haita pata uzao wako.

sasa kwenye la kupiga kura usinge piga kura nazani ungekuwa unawajibika katika matatizo kwani kukaa kimya kwako tungejua unamsaport.

huyo mbunge uliye naye siku zote anajua kuwa kuna watu hawamkubali na mmja wao ni wewe kwa hio anafanya hayo kwa wale wanao mkubali ila we sio mmoja wao.

piga kura siku zote usiache haki yako ya msingi mi nakumbuka mwaka 2005 ili nibidi nisafiri usiku mzima ili niende kupigA KURA NAMPAKA SASA NAFARIJIKA KUWA NILIYE MPIGIA HAKUPATA ILA ALIYE SHINDA NA KUFANYA UTUMBO SIO CHAGUA LANGU,.
 
Mkuu una moyo mgumu kama wa kobe! Hongera kwa ujasiri huo.
 
Vote yako ni wasted vote, yaani wewe ni hoi ile mbaya. Miaka 15 wewe unachagua watu bomu tupu?

Uko jimbo gani nikusaidie kuchagua mtu wa kumpa kura yako 2010?

Ukiendelea na tabia ya kuwa kilaza wa kuchagua watu bomu, hata mke utachagua bomu!

Mimi 2000 nilichemka wote urais na MP. Mwaka 2005 nikajifunza na nikachagua washindi, ila wote wamekuwa bomu, bora ningelilala nisiende kwenye uchaguzi.

Inaniumiza kwamba kura yangu ilisaidia kuleta majitu hovyo hovyo!

Niko jimbo la KAWE.
 
Mimi nakushauri uwapigie CCM ama yoyote unayotaka ashindwe kwa kuwa takwimu zako zinonesha wazi kwamba umpigiae kura siku zote hushindwa.
 
Wadau naomba Ushauri wenu. Nafikiria kuacha kupiga kura kwa kuwa tangu nianze kupiga kura, sijawahi kumchagua aliyeshinda. Sasa naona kuliko kupiga kura wakati nayempigia kura huwa hashindi, ni kama kupoteza muda wangu bure. Labda ushauri wenu unaweza kunisaidia.

Hebu angalia mlolongo huu:
Mwaka 1995 Nilimpigia Mrema, akashinda Mkapa.(CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia Lipumba akashinda tena Mkapa.(CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia Mbowe akashinda Kikwete.(CCM)

Kwa Upande wa wabunge
Mwaka 1995 Nilimpigia mgombea wa NCCR Mageuzi akashinda Keenja (CCM)
Mwaka 2000 Nikampigia mgombea wa TLP akashinda Ritha Mlaki (CCM)
Mwaka 2005 Nikampigia mgombea wa CHADEMA akashinda Ritha Mlaki (CCM)

Sasa niendelee kupiga kura au niache? Nauliza kwa kuwa nina allergy ya kukipigia kura CCM na ninapowapigia wapinzani huwa hawashindi.

Mwakani mpigie JK atashinda!
 
Back
Top Bottom