Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,496
- 37,789
Niko Rukwa kwa kazi zangu za uandishi wa habari za mazingira siku 5 Sasa. Hapa naongea toka kijiji cha Kabwe wilaya ya Nkasi.
Hapa Niko Jimbo la Nkasi kaskazini Kwa Mbunge pekee wa kuchaguliwa wa Chama cha demokrasia na maendeleo mh. AIDA KENANI. Nina Jambo nimelishudia Sumbawanga mjini juzi jumatatu acha niliweke hapa.
Kwanza nitoa mfano wa mkoa wa Mbeya unavyoendesha Mambo yake. Mbeya Jiji ina stendi 2 na zote zinafanya kazi, yaani stendi ya zamani ya mjini Kati na Nanenane.
Mbeya ni jiji kubwa na pilika zake ni mara 3 au zaidi Kwa Sumbawanga. Hali hiyo ya stendi mbili imewarahisishia Wananchi kuingia na kutoka Mbeya bila bughudha wala kutumia gharama kubwa.
Lakini Sumbawanga mji mdogo viongozi wa serikali wameona Hilo haliwezekani wamefunga stendi ya mjini Kati hata Kwa mabasi yanayofanya safari ndani ya wilaya ya Sumbawanga na ndani ya mkoa na yote wanataka yaanzie safari Stendi mpya ya Katumba km 14 toka mjini.
Hebu fikiria akili za hawa watendaji. Mwananchi mgonjwa aliyepeapa rufaa kwenda hospitali ya mkoa atoke Matai Makao makuu ya wilaya ya Kalambo km 36 toka Sumbawanga aipite hospitali maana hairuhusiwi kushusha abiria stendi za daladala, aende Katumba km 14, kisha apande bajaj alipe 3000/- arudi tena km 14 kufuata hospitali mjini akimaliza kutibiwa achukue bajaj aende Katumba km 14 apande basi la kwenda Matai apite hapohapo alipokuwa anatibiwa ndo aende Matai. Huu ni uhuni na kusumbua Wananchi. Ni kuwapa gharama na mateso yasiyo na sababu.
Mwaka jana alipokuja Waziri Mkuu Majaliwa alielezwa Jambo hili na Diwani wa CCM na akaamuru stendi zote mbili zitumike kama ilivyo Mbeya, alipoondoka baada ya mwezi wakafunga stendi CCM wakamwambia Waziri ikafunguliwa, alipokuja KM Chongolo akaelezwa akasema Chama kimetoa amri Wananchi wasisumbuliwe.
Ameondolewa Chongolo madarakani miezi michache tu wamefunga stendi ya mjini na safari hii CCM wamekaa kimya naambiwa wananchi wanataka kupeleka Kadi ofisi ya CCM mkoa.
Hivi kama chama mnajinasibu kila siku nyie ndo Wenye serikali maana yake nini kama mkurugenzi mmoja anaweza kuwatetemesha kiasi hiki na mkaufyata? Au na nyie mmeungana naye kutesa wapiga Kura wenu?
Nadhani hamjasahau taabu mliyopata Nkasi kaskazini 2020 Wananchi walipomkataa mgombea wenu na wakalinda Kura wakiwa na chupa zenye petrol tayari kuchoma jengo la mkurugenzi akithubutu kupindua matokeo. Mmesahau Polisi walivyosaidia kupiga mabomu zaidi ya 100 na bado Wananchi hawakuondoka hadi matokeo halali yalipotangazwa?
Wafipa ni wapole, lakini wakikasirika hamuwezi kuwarudisha.
Chelleeni Mwana kulia Oktoba mtalia ninyi.