Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Baada ya Uchaguzi huru na haki huko Gambia, upinzani umeibuka Washindi chini ya Umoja wa vyama pinzani ukiongozwa na Adamu Burrow!
Rais aliyekuwa madarakani Yahya Jammeh kwanza alikubali matokeo na kumtumia salamu za pongezi Burrow kitendo kilichopongezwa na Jumuia za Kimataifa.
Vituko vilianza baada ya Jammeh kubatilisha kauli yake kwamba Uchaguzi haukuwa huru na haki hivo hawezi kukabidhi madaraka!!!
Uamuzi wa Yahya Jammeh unafanana kabisa na kilichotokea Zanzibar mwaka jana 2015 pale ambapo Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) chini ya Jecha Salim Jecha ilipobatilisha matokeo baada ya CUF chini ya UKAWA kuibuka na ushindi mnono kwene viti vya Wawakilishi ndani ya BMZ!
Kinachoshangaza ni kwamba Jumuia ya Kimataifa ikiwemo Jumuia ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi(ECOWAS) imeanza mchakato wa kumshauri Jammeh akabidhi madaraka kwa amani la sivyo Gambia itawekewa vikwazo vya Kiuchumi!
Swali ni kwanini hatua kama hizo hazikuchukuliwa kwa Zanzibar na Serikali ya Tanzania Bara ilhali mazingira yalikuwa yaleyake kama ilivyo Gambia? Kuna nini kilikosekana hapo? Tujadili.