Kuna siku dunia inaweza kuwa bila vita ama mtu yeyote kukosa adui kila aendapo?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,363
6,900
Nilishatafakari kuwa hivi mataifa yote yanaweza kuwa na amani hata siku moja dunia nzima? jibu nililopata ni kuwa haiwezekani kitu kama hicho.

Mtu binafsi unaweza kukaa bila adui popote uendapo hata iwe kanisani?

Amani kitu kizuri katika maisha ya mwanadamu. Binadamu ana hofu nyingi maishani mwake. Hata kama una kidonda au kovu lilisababishwa na kitu, mtu au mnyama amani hutoweka. Kila ukiona linaweza kuwa kama rejea. Ndio maana kila mtu hana amani kutokana na kitu fulani maishani mwake.

Nahisi kila mtu ana kitu kinachomtia hofu, chochote kinachokuondelea amani ni adui.

Swali linakuja kama hiwezi kumkwepa adui huwa unafanyaje ili usishikwe na msongo au sonona (trauma)?
 
Back
Top Bottom