Kuna nini uwanja wa Ndege Kilimanjaro?

SonGod emo

Member
Apr 5, 2012
17
12
Tarehe 02 Julai nilikuwepo eneo la uwanja wa ndege kia nikiwa na shughuli zangu binafsi majira ya saa 1430. Ilitua ndege kubwa aina ya ya Airbus iliyovuta hisia za watu wengi sana wakiwemo wafanyakazi wa uwanja huo.

Nilijivuta karibu na kutaka kujua ni kina nani wako na ndege hiyo nilipouliza niliambiwa ni mtoto wa mfalme wa Dubai amekuja kwa ajili ya kwenda kuwinda kwenye kambi yao iliyoko Loliondo.

Kama tunavyojua taratibu za kitaifa au kimataifa mtu yeyote anaeingia nchi yoyote ile awe mwenyeji au mgeni ni lazima akaguliwe na Immigration pamoja na Customs yaani wakiwemo Tra cha kushangaza watu hao wilishuka kwenye Airbus na mizigo yao na kuingia kwenye ndege ingine tayari kwa safari ya loliondo nilipouliza ni kwa nini? Nilijibiwa huyo ndo mfalme ameshamwaga pesa kila kona kwenye idara zote je?

Nchi kama Kenya watu wanaweza kufanya upuuzi huuuu kweli? Sishangai kuona wanyama wakisafirishwa kwenda nje ya nchi pamoja na udongo kwa ajili ya kuoteshea maua ua mfalme wa Dxb ni kutokana na KIA imekuwa kama lango la uhaini, uharamia kwa sababu ya njaaa za viongozi wachache wasiokuwa na uchungu wa nchi yao.

Nawasilisha wandugu.
 
Labda wanamfanyia hivi Riz akienda Dubai, hivyo nao wakija kwetu wanategemea watoto wa Mfalme wafanyiwe hivyo hivyo - reciprocal arrangement!
 
Umeshasema ni mtoto wa mfalme,achekiwe nini? Halafu wewe umeacha kazi zako ukaenda airport kutafuta nini? Si uanafiki tu huo
 
Ni aibu sana kwa taifa alafu polisi wanakuambia usalama umeimarishwa upuuuzi mtupu
 
hee...wanasema karibu kwenye himaya ya kifalme kumbe tayari hii sio ya kwetu tena
 
Yani mpaka leo kuna watu wanakwenda kutembea airport halafu mnasema tanzania ya sasa sio ya zamani.
 
Umeshasema ni mtoto wa mfalme, achekiwe nini? Halafu wewe umeacha kazi zako ukaenda airport kutafuta nini? Si uanafiki tu huo
Hujui unachobishia wewe.

Nenda Lololiondo kipindi waarabu hawa waharibifu wanawinda ndipo utajuwa hakuna uongozi makini katika nchi hii. Uwindaji wao hauchagui aina wala umri wa mnyama.

Sasa hivi ukifanya game drive maeneo ya Lobo wanyama wakiona gari wanakimbia sababu ya waarabu hawa. Mzee Mwinyi naye alitukaanga katika hili.
 
Ni tayari msimu wa uwindaji umeshaanza toka 1.7.2012, kwa wanaoishi Arusha wanajua. Huyu kijana huwa akija anatanguliwa mbele na warembo wa kifaransa ambao wanaangusha hela huku wakimpepea. Kwa maana hiyo hakuna anaeweza kumfanyia ukaguzi wowote, maana anakuwa alishatuma watangulizi mapema.
 
huyu ni mfalme wa nchi kutoka kwao na nikiongozi kweli anaweza kuja hapa nchini bila serikali kujua? Uenda ujui taratibu na serikali inavyofanya kazi
 
Mambo haya yapo!! Polisi + usalama =wapo kulinda maslah ya matajiri wachache na chama chao. Wewe unayebisha nadhani unahusika
 
Hao waarabu si ndio wale waliochoma maboma yote ya wamasai na ng'ombe zao na bado wanaendela kuchoma?

Leo hii mmsai aliyeishi na wanyama hao tangu kuumbwa kwa ardhi haruhusiwi hata kupitisha ng'ombe vinginevyo wanapigwa risasi na maboma yanaendelea kuchomwa, halafu wanaondoka na wanyama aina 100 mpaka nembo ya taifa letu, kitoweo chao ni wanyama wa Tanzania yaani TWIGA naye anabebwa kwa kiasi wanachotaka, wewe majebere aka CCM huruhusiwi kuwinda Loliondo yote huo sio wizi au unataka mamayo akwambie
 
Nimeshawahi kuishuhudia pia mimi kipindi cha nyuma ivi .......dege la emirates lilitua pale.. wakashuka waarabu kadhaa pale pale wakapanda emirate nyigine ndogo kidogo, kuuliza nikaambiwa wana mbuga yao Loliondo...

Sasa cha ajabu, watu hupanga foleni kupewa hela kipindi waarabu hao wanapobadilisha ndege (kwa maana kutoka kubwa kwenda ndogo), hiyo siku watu walitoka maeneo yao ya kazi na kwenda kujipanga mstari na kukinga mikono... Vichwa viliondoka na dola mia mia... Kama mtu wa kawaida anaondoka na hela izo......je mataita?
 
Back
Top Bottom