Kuna mtu anayeweza kuandika juu ya urais wa Magufuli kwa usahihi?

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
9,806
14,891
Baada ya kifo chake kumezuka makundi makubwa mawili yanayo kinzana. Moja ni wale wanaoamini kuwa alikuwa shujaa wa kipekee na ameifanyia nchi yetu makubwa. Kundi la pili wanamuona kama rais mbovu kuwahi kutokea, dikteta, fisadi, mkabila, katili nk.

Kwa maelezo hayo naweza kusema kuwa ni rais aliyekuwa controversial. Je kuna anayeweza kuandika kitabu juu ya urais wake kwa usahihi na ukakubalika?
 
Mimi kaniongezea nyama kwenye kitabu change cha ujasiriamali kwamba kumbe Sera ambazo hazina muelekeo ,hata km una elimu nzuri na mtaji huwezi kutobia 'policy uncertainty' in other words use of un guided policy, has negative effect to business growth or success
 
Baada ya kifo chake kumezuka makundi makubwa mawili yanayo kinzana. Moja ni wale wanaoamini kuwa alikuwa shujaa wa kipekee na ameifanyia nchi yetu makubwa. Kundi la pili wanamuona kama rais mbovu kuwahi kutokea, dikteta, fisadi, mkabila, katili nk.

Kwa maelezo hayo naweza kusema kuwa ni rais aliyekuwa controversial. Je kuna anayeweza kuandika kitabu juu ya urais wake kwa usahihi na ukakubalika?

IMG-20210410-WA0065.jpg

IMG-20210410-WA0069.jpg

IMG-20210410-WA0089.jpg
 
Kwani huoni namna watu wanavyoandika kwa usahihi juu ya Uonezi na Upigaji uliofanyika? Ama wewe unataka usahihi upi au kipindi cha hayo yakitokea ulikuwa kipofu na kiziwi?
 
Baada ya kifo chake kumezuka makundi makubwa mawili yanayo kinzana. Moja ni wale wanaoamini kuwa alikuwa shujaa wa kipekee na ameifanyia nchi yetu makubwa. Kundi la pili wanamuona kama rais mbovu kuwahi kutokea, dikteta, fisadi, mkabila, katili nk.

Kwa maelezo hayo naweza kusema kuwa ni rais aliyekuwa controversial. Je kuna anayeweza kuandika kitabu juu ya urais wake kwa usahihi na ukakubalika?
Ndugu, ulichokiwasilisha ni oversize kwa akili za JF iliyojaa mashabiki.
Kuna kiongozi wakati wa kuaga alisema JPM ataishi miaka mingi kwenye mioyo ya watanzania, we can see now. Kaiteka mijadala na siasa za nchi na itaendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu.

Kuna msemo unasema, legends never die.
 
Mimi naamini kwa mazingira tuliyopitia kama nchi kuanzia mwaka 2015, wengi wetu hatutokuja kupenda atokee Rais mwingine nchini mwenye hulka kama za Magufuli!

haki ya nani yule mzee angeendelea kuitawala nchi hii, ingefikia wakati watu wangeamua tu kugawana fito aisee! Aliteua vichaa na wendawazimu kuwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi! Aliteua wezi, wanafiki, makada, ndugu zake nk. Kushika nafasi nyeti!

Alitisha watu mchana kweupe! Na wengine wakapotea, wakauwawa! Na hata wengine kama akina Tundu Lissu, wakanusurika kifo! Aliruhusu hadharani polisi kuua watuhumiwa huku akiwa hajui madhara ya kufanya hivyo!

Mungi ni mwema sana kwa kutusikia kilio chetu na hivyo kutuondolea udikteta ulio anza kutamalaki kwa kasi nchini mwetu.
 
Ndiyo,mimi naweza.Magufuli alikuwa ni populist aliejificha kwenye kichaka cha siasa za propaganda ili kuonekana kuwa ni mchapa kazi wakati alikuwa ni fisadi mkubwa,mwizi,na mzembe kupindukia katika kulinda rasilimali za umma na ukweli huu unaungwa mkono na ripoti iliyotoka ya CAG.

Hiyo ndiyo summary ya kitabu changu.
 
Ndugu, ulichokiwasilisha ni oversize kwa akili za JF iliyojaa mashabiki.
Kuna kiongozi wakati wa kuaga alisema JPM ataishi miaka mingi kwenye mioyo ya watanzania, we can see now. Kaiteka mijadala na siasa za nchi na itaendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu.

Kuna msemo unasema, legends never die.
Ataendelea kuishi both +ve & -ve way. Kwa mazuri ya awamu hii tunashukuru. Lakini pia kwa mabaya ya awamu hii tumejifunza mengi kama taifa
 
Ataendelea kuishi kwenye moyo wako tu, usiwasemee watu wengine wana mioyo yao, yaani kama mimi hakuna hata chembe ya nafasi kwenye moyo wangu naweza kuweka kitu kama hicho, viko vitu vingi vinahutaji nafasi kwenye moyo wangu siwezi kuweka jiwe
 
unaongea kitu gani wewe? Hata Idd Amin, Hitla, Musolin bado wanaishi kwenye mioyo ya watu kwa maana kwamba bado wanakumbukwa. Hatukumbuki waliotenda mema tu, hata waliofanya fyongo tutawakumbuka, so sidhani kama utaweza kujifanya eti usimkumbuke Magufuli. Kwa mazuri or otherwise utamkumbuka tu!
 
Ana mazuri yake na mabaya yake.

Mazuri--ujenzi wa reli,bwawa la umeme, kupunguza ujambazi,ujenzi wa madaraja na barabara,kuisha mgao wa umeme, kupunguza ujangiri,kupambana na madawa ya kulevya,usambazaji maji na umeme vijijini nk.

Mabaya-kukandamiiza demokrasia,kukandamiza uhuru wa habari, kutengeneza viongozi waoga na wanafki,miradi isiyo kuwa na lazima Kama ununuzi wa ndege,uwanja wa ndege Chato,kutokujibu au kufanya uchunguzi wa kupotea Azory Gwanda,Ben saa nane,kupigwa risasi Tundu Lissu.

Ukisema JPM kafanya yote mabaya ni kosa na kusema kafanya yote mazuri nalo ni kosa.
 
Back
Top Bottom