Kuna Mchezo Unachezwa!

ni kweli kuna mchezo unachezwa...na ni kweli sio kila mchezaji anaujua muziki wenyewe...ni kucheza kwa kufata mkumbo kwa kwenda mbele...kanuni kuu ni moja, mtumikie kafiri upate rizki yako...so wachezaji wale utawaona wanatoka majasho na hata midomo inarusha mate ukidhani wanatetea na kuucheza mchezo kwa upendo wa kweli...la hashaa...wakitoka pembeni kupumzika kidogo ukiwauliza walikuwa wanacheza nini, watakwambia sisi tunacheza tu ndo watakavyo wakubwa...si ndo kamanda mkuu atakavo hivi tuchezeeee tuuu!!! mbaya zaidi, wanadhani watz wote wanawakubali na kuwaona wanacheza vyema,..kumbe ni hasira zimejaa huku nje ya huo mchezo na ole wao subira ituishe...na hivi inavyozidi kutuisha...naona na wao wameanza kuona tishio la mchezo wao mchafu...ila kwa vile nidhamu ya woga, wanaogopa waende kwa watu au wabaki mchezoni kumfurfahisha kamanda mkuuu.....ole na pole zao nyingiiiiii
 
Kwenye mchezo wowote ili timu ishinde inabidi uingie ndani ya dimba na ucheze kwa moyo wako wote... Ule mtindo wa kuwa nje ya dimba na kupiga kelele ...Piga mbele... Toa pasi... Piga ngwara ..haitosaidia kushinda mchezo, kwani kama mchezaji unatakiwa kutumia akili (kama unayo) na pia kumsikiliza kocha na sio wale walioamua kuwa nje na kuishia kupiga kelele.....

Raha ya ngoma ingia ndani ucheze... Na pia kumbuka ukiingia ndani kucheza basi ucheze kweli na sio uingie ndani kwa nia ya kuangalia kiuno cha mwenzako bila kufuata mirindimo ya ngoma... Kama hujui kucheza basi hata mwangalie jirani yako alicheza vipi au anacheza vipi...

 
yes mchezo wenyewe ni katiba. Kila mtu anaitaka lakini wananchi walio wengi including wapinzani wamegoma kucheza mpaka kanuni zifuatwe. Ccm wanatulazimisha tuingie tucheze lakini bila kanuni hamna raha ya mchezo. Ni wazi upinzani wamekataa kabisa kuingia kucheza; wamekaa pembeni, sijajua wanachi wameamu nini hasa. Je wamekaa pembeni tu au wanampango wakuingia na kuvuruga mchezo mzima ili tuanze upya kwa taratibu/kufuata kanuni? Au watakubali kucheza kama wanavyoshauriwa na ccm bila kufuata kanuni?


asante sana mkuu, maana nilishaanza kukatishwa tamaa na wachangiaji wa mwanzoni maana ile "the great thinkers" haionekani kabisa, ushauri wangu kwao "" sio lazima uchangie kila hoja , hujui tulia utajifunza kutoka kwa great thinkers wa kiukweli, ndipo utakuwa umepata pa kuanzia, jf ilikuwa kitu makini sana mpaka kuwa tishio lakini sasa naona KAMA harufu za kishule shule vile, sijui, na samahani sana kwa wale watakaokwazika, huo ni mtazamo wangu.
 
Maandamano vyuo vikuu,Fujo za wmachinga mbeya, hekaheka za Arusha ni sisimu ndo wanazifanya na wanalijua hilo na hili la katiba wanataka kuleta upumbavu sasa ninachosema ni kwamba hawata fanikiwa....Tanzania ni nchi ya amani tutapata katiba yetu kwa njia ya amani....Wanatingisha kiberiti tu hivi mnafikiri kuna mtu muoga kama kikwete?....uoga wa huyu kiongozi wa wanafiki ndo utakao tufikisha kwenye mapinduzi ya kweli kwa sababu anapenda kumfurahisha kila mtu....na nimtu ambaye hufanya maamuzi bila kufikiria athari zake....na ndo faida tunayokwenda kuipata kupitia udhaifu wa huyu Bwana....Tusikate tamaa.....wala hatutagomba....kama Mwl Jk alivyoweza kuichua nchi bila fujo kutoka mikononi mwa mkoloni ndivyo hivyo cdm watakavyo hichukua nchi hii mikononi mwa haya mazimwi,makupe,mambwa mwitu yanayo jivika vinywa vya wanakondoo.
 
Nahisi mchezo wenyewe ni wabunge wa CCM kuburuzwa katika mswada wa katiba mpya. Siku watakapokuwa sio wabunge ndio watajua walichotaka kupitisha hakikuwa kizuri
 
Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwanini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'?

Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza.

Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Ukialikwa kucheza utacheza au utabakia kutazama? Au utajaribu kutaka mchezo ubadilishwe ili wengi waufurahie kwa kufuata kanuni, na mirindimo yenye kuendana na uzuri wa mchezo wenyewe?

Ndugu zangu, kuna mchezo unachezwa, na wapo wenye kupenda kucheza mchezo huo!



MMM

Kuna mchezo mchafu unachezwa? Lol! Bila shaka huo utakuwa ni ucameron tu! Ha!ha!ha!
 
Na mchezo huo umehamia hata kwa wototo hasa wale wa vyuoni, mchezo ambao unaweza kucheza bila kujijua kuwa umeucheza. Mchezo ambao wenye kuuimba hawataki wasanii wengine wauimbe. wengine wanataka waucheze mpaka wafe ka kuku atamiaye na kufia juu ya mayai ya kuku.
Mchezooo jamani khatari!
HUJUI KAMA UNACHEZA MCHEZO WA SIASA WEWE!
 
MKJJ bana!! Michezo iko mingi najua wengi hatuijui.This season michezo mikubwa ni miwili tu. Reshuffle the cabinet and, or leave the office by coercion!! Believe me hali ni ngumu pale ndani...
 
Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwanini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'? Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza. kuna mchezo unachezwa na wapo
 
Yes mchezo wenyewe ni katiba. Kila mtu anaitaka lakini wananchi walio wengi including wapinzani wamegoma kucheza mpaka kanuni zifuatwe. CCM wanatulazimisha tuingie tucheze lakini bila kanuni hamna raha ya mchezo. Ni wazi upinzani wamekataa kabisa kuingia kucheza; wamekaa pembeni, sijajua wanachi wameamu nini hasa. Je wamekaa pembeni tu au wanampango wakuingia na kuvuruga mchezo mzima ili tuanze upya kwa taratibu/kufuata kanuni? Au watakubali kucheza kama wanavyoshauriwa na CCM bila kufuata kanuni?

asante mk., huu ni mchezo wetu wa katiba, tumeona mapigo na mashairi haviendi ila ssm wanacheza ili mradi wacheze na ionekane unacheza, cdm na nccr wamejitahidi kubadilisha mapigo ya mziki wakakataliwa ma kutukanwa na kudharauliwa, kisa mapigo yasibadilishwe hata kama haviendi, walio wengi tanzania hii ngoma wanailewa,
wameshauri sana, ngoma kubadilishwa,
wenye hatamu hawataki kisa kitambua kitaigiw amchanga,
sisi tukae pembeni bomu hili litakuja pasuka,
wanajiita wasomi, ndani ya ssm wamekaa,
uweledi wao tunaoji mbona wafaa mipasho,
mtazamo wao ukoja mambo muhimu kupuuzia,
waliowabeza kwa mbwembwe huku kwetu ndo mashujaa,
wanazuoni nguli washauri wao wawaona makapi,
wajiona sheria navifungu wavijua huku twasema hamnazo
siku itafika nasema wote watashangaa
kisu ulichomnolea mtu, kitakuja kukuchinja mwenyewe!
 
Mchezo bila kanunu, si mchezo ni uchizi

Kanuni huweka mwanzo wa mchezo na mwisho wa mchezo.

kanuni huweka mshindi wa mchezo na mshindwa wa mchezo.

mchezo bila kanuni, si mchezo ni uchizi.

Haihitaji kanuni machizi wanapocheza

Wala haitamanishi kuwaona wanavyocheza

ukitamani kucheza, na wewe utakuwa chizi.

usiulize kanuni, kwa mchezo usio ujua

wala usiutamani mchezo usio ujua.

kama twataka cheza, tuanzishe wetu mchezo, tuweke zetu kanuni
machizi wakituona, wataacha wao mchezo, usokowa na kanuni
 
Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwa nini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'?

Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza.

Kuna mchezo unachezw
 
Kwa jinsi kila jambo lilivyo au linavyoelekea kusambaratiki ni ngumu sana to tell umelenga nini.
Vinginevyo Nahisi Mwanakiji unajianda kuingia Studio au unamuandikia mtu mashairi..
 
Inakuwaje wapo watu ambao wanashabikia mchezo ambao wao wenyewe wakiambia wacheze wanagoma? Watu wanaotaka wengine wacheze bila kuuliza na washangilia bila kujua mwisho wa mchezo unatakiwa uweje. Huwezi kumchukua anayecheza Lizombe ukamrushia acheze Mganda! Well, zote ni ngoma lakini steps za Mganda na kuchezacheza kwa lizombe havifanani. Mchezo huu kwa kweli unatugawanya maana wapo wengine ambao wanazungumza kwa umakini utadhani wanajua mchezo ulivyo kumbe na wao wameambiwa tu 'ni mchezo mzuri'! Wanashabikia!

Tusubiri tuone kina nani watacheza na kwanini watacheza!
 
MKJJ,I always don't underestimate their capabilities.Although inawezekana this time wamekuta kuna difficulties kila stage wanayovuka, they are so well kwenye kujipanga, this includes provision of the contingency plan. Lets see; maana kwa sasa naona hata wasiokuwano wanaucheza tu!!!
 
Ni upofu mkubwa wa ufahamu hasa unaosababishwa na unafiki,kujikomba,kugagaa na upwa,mawazo finyu na hata mitindio wa ubongo kwa baadhi ya washabiki wa mchezo wasiouelewa.Haiwezekani kwa mtu mwenye akili timamu kucheza ngoma ambayo imebadilishwa sio ile aliokuwa anacheza kabla kwa staili ile ile,yaani ulikuwa unacheza lizombe ghafla unaletewa mganda we bado umo na staili ile ile ya lizombe,mchezaji makini ni yule anaetambua kuwa ngoma imebadilika sio unacheza tu,na ukiona mwenzio kaacha kucheza unamshangaa na kuanza kumponda kuwa si mchezaji hapana wewe ndio sio mchezaji ni mkorogaji tu,utachezaje staili ya lizombe kwenye mganda na hata hao wanao kushangilia nao hamnazo kama wewe.Hakuna kitu kibaya kama kuwa akili kuambiwa wasukuma wanasema "masala kulangwa" asilimia 100 ya wabunge ccm ni masala kulangwa wanaamini kila wanachoambiwa na kuanza kushabikia kwa nguvu zao zote bila hata kuona athari za kile wanachokishabikia.
 
Back
Top Bottom