Kuna Mchezo Unachezwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwa nini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'?

Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza.

Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Ukialikwa kucheza utacheza au utabakia kutazama? Au utajaribu kutaka mchezo ubadilishwe ili wengi waufurahie kwa kufuata kanuni, na mirindimo yenye kuendana na uzuri wa mchezo wenyewe?

Ndugu zangu, kuna mchezo unachezwa, na wapo wenye kupenda kucheza mchezo huo!



MMM
 
MMM,
Mbona leo umekuja kivingine umekuja kwa vina tata!

Tudokeze basi mchezo gani unachezwa na nani wanacheza!
 
MMM tukiwaacha wacheze hautatudhuru mchezo huo,na tukitaka tucheze je tutacheza kama wao au tutacheza kwa kufuata tune na melody ya mlio wa mchezo.au tuwaache tu wacheze lakini najiuliza nini hatima yake?

Au tukitaka kuwafunza kucheza kwa kufuata kanuni za kucheza mchezo huo watakuwa tayari kupokea maelekezo ya kucheza? Any way tuujadili mchezo wenyewe
 
Mchezo unaopendwa na watu ni halali kuchezwa na watu!

Mchezo wa watu wote kwanini ukae pembeni wewe si mtu??

Mchezo mzuri kanuni zake huandaliwi kabla ya kucheza!

Kucheza bila kufuata kanuni ni kuharibu utamu wa mchezo wenyewe!

Huwezi kupenda huu mchezo hadi ucheze kwanza

Hairuhusiwi kubadili kanuni kabla ya kucheza, sharti uwe uwanjani ndio utabadili kanuni.
 
Yes mchezo wenyewe ni katiba. Kila mtu anaitaka lakini wananchi walio wengi including wapinzani wamegoma kucheza mpaka kanuni zifuatwe. CCM wanatulazimisha tuingie tucheze lakini bila kanuni hamna raha ya mchezo.

Ni wazi upinzani wamekataa kabisa kuingia kucheza; wamekaa pembeni, sijajua wanachi wameamu nini hasa. Je wamekaa pembeni tu au wanampango wakuingia na kuvuruga mchezo mzima ili tuanze upya kwa taratibu/kufuata kanuni?

Au watakubali kucheza kama wanavyoshauriwa na CCM bila kufuata kanuni?
 
Back
Top Bottom