Kuna mama ananitaka kwa udi na uvumba nifanyeje?

Ukback255

Senior Member
Aug 31, 2016
174
276
Wakuu salamu,

Nimeona niilete hii kuna mama alifanikisha mimi kupata scholarship ya kusoma second degree nje ya nchi.

Ni mama msichana lakini yupo na miaka 37 wakati mimi nikiwa na miaka 28 kibaya zaidi kaolewa but sijawai jua mume wake kwa sababu sijawai muona.

Sasa hivi ananitaka kimapenzi kabisa alikuwa ni Mkurugenzi pale kitengo changu cha kazi. Alifanikisha kuniunganisha nikapata scholarship ya kwenda kusomeshwa nje degree ya pili na taasisi miliyokuwa nafanyia kazi siwezi itaja.

Lakina cha kushangaza alikuwa akinipa dollar 2,000 kila baada ya miezi 6 pembeni ya ile scholarship yangu na taasisi ya kazi.

Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa muda mrefu tokea nitoke nyumbani lakini mpaka sasa ni kuniambia ananipenda tu. Masomo nimemaliza na nimeamua kuzama ugaibuni maana naogopa hata kurudi nyumbani.

Wakuu mnishauri nifanyeje maana nimeshindwa kabisa nifanyeje huyu mama ananisumbua kweli ushauri wenu wakuu.

Nimeshindwa kutoa maelezo ya kutosha kwa sababu ya usalama wangu zaidi.
 
Kama ana mumewe kula mzigo ila mkapime kwanza maana ukimwi upo, pia ukae ukijua kwamba mke wa mtu sumu hivyo siku ikifika ujue na wewe unaliwa utulie mambo yaishe
 
Ugumu uko wapi hapa? Mbona hiyo tofauti ya umri wenu si kubwa kiasi hicho? labda useme hakuvutii. Kama hakuvutii mwambie ukweli kwamba humtaki badala ya kuendelea kumzuga kwa kipindi kirefu sasa.

Mkuu haya mambo ni magumu sana
 
ommba ukimbizi huko. sema Nyumbani utanyanyaswa kingono na kijinsia. kwani anavyosema anakupenda huwa unamjibu nini? iga kisa cha yosefu na mke wa potifa.
 
Kama ana mumewe kula mzigo ila mkapime kwanza maana ukimwi upo, pia ukae ukijua kwamba mke wa mtu sumu hivyo siku ikifika ujue na wewe unaliwa utulie mambo yaishe
Haaaaaah mkuu anaogopa vitu vya watu wazima huyo
 
Back
Top Bottom