Kuna hiki kiumbe lakini cha ajabu hapa duniani

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,401
Kuna hiki kiumbe lakini cha ajabu hapa duniani
kiitwacho Mwanaume. Ni cha ajabu kutokana na uwezo
wake wa kubadilika kufuatana na mazingira kilichomo
kwa wakati husika. Hakika hata yule bingwa wa
kujibadili kinyonga haoni ndani. Angalia kwa mfano
mazungumzo ya simu ya kiumbe hiki. Miaka kama kumi nyuma wakati kikifahamika kwa sifa ya 'mchumba wa mtu':

"Sweetheart! Habari za asubuhi"
"Nzuri tu dear, sijui wewe !"
"Aa, mimi hali yangu sio nzuri kabisa"
"Ee nini tena Dear !"
"Nimekumiss mpenzi wangu, halafu usiku mzima wa jana
nakuota tu!"
"Jamani pole sana mpenzi"
" Asante lakini haitoshi darling ! Hivi kwanza leo
nitakuona saa ngapi?"
"Sijui wewe labda unifuate wakati wa lanchi !"
"Ok basi, wife to be endelea na kazi huku ukiendelea
kukumbuka ule wimbo wangu ninaoupenda kukuimbia !"
"Mh? Upi tena huo dear ?"
"Aaah unaniangusha darling ! Si ule wa oh my sweet,
my sugar, let melove you forever, oo yes!, umeukumbuka
?!"
"Alaa! Huo! Basi nimeukumbuka! Bye dear!"
"Bye, nibusu basi"
"Baadaye dear, kuna watu hapa!"
"Ok basi!"



Haya basi miaka kumi na mbili na watoto wanne baadaye
hiki kiumbe mwanaume sasa kina hadhi ya 'mume wa mtu'
na sasa tunakutana nacho kikipiga simu kwa yulee mtu
aliyekuwa mchumba wake miaka kumi na mbili nyuma na
ambaye sasa anakwenda kwa hadhi ya "mkewe". Mazungumzo
yaokwenye simu sasa ni "makavu" kama mtumba wa Manzese
........!
"Hujambo ?"
"Sijambo ! Za kazi ?"
" Safi , hawajambo hao ?"
"Hawajambo tu !"
"Huyu aliyekuwa anaharisha vipi ?"
"Anaendelea vizuri, nimempa enthoromycin naona
inamsaidia"
"Sawa huyo fundi wa TV naye kishafika ?"
"Sijamuona !"
"Sawa, akija muangalie sana asiibe vitu kwenye hiyo
TV !"
"Sawa, sasa Baba nanii...!"
"Unasemaje?"
"Kuhusu ile losheni"
"Umeshaanza! Nimesema nitakununulia! "
"Jamani Baba nanii.....! Mwezi wa pili huu sasa, kila
siku unaniambia hivyo hivyo!"
"Alaa! Tumeshaanza kuhesabiana siku sasa!"
"Basi yaishe ! Mimi nilikuwa nakukumbusha"
"Haya, mimi nitachelewa kurudi nyumbani kidogo kuna
jamaa naenda kumcheki nikitoka kazini !"
"Sawa"
"Baadaye basi"
"Sawa"



Kiumbe kiitwacho mwanaume kinamaliza kuongea na mkewe
na kukata simu.Bila shaka utapata taabu kukubali
kwamba huyo ndiye yule yule aliyekuwa anaongea kwenye
simu ya kwanza miaka kumi na mbili iliyopita. Bila
shaka pia utajiuliza, yako wapi maneno yale 'darling',
sweetheart', mpenzi na wimbo wa 'ooh my sweet my
sugar!' sasa yamekuwa ni bidhaa adimu mdomoni mwa mume
na masikioni kwa mkewe. Lakini ni kweli kwamba maneno
hayo yamekuwa bidhaa adimu kwenye mdomo wa kiumbe hiki,
mume ?
Hebu tusikilize simu hii ya mwisho ya kiumbe huyu
dakika chache tu baada ya kuongea na mkewe anaongea na
simu hii akiwa amevua ile hadhi ya mume na kujivika
mwenyewe bila kushurutishwa na mtu, hadhi ya buzi na
anayeongea naye ni kiumbe mwenye hadhi ya mchuna buzi.
Patamu hapo, babu yangu!
"Haloo, darling!"
"haloo mambo"
"Poa! Unafanya nini sasa hivi darling wangu?!"
"Aaa nipo tu natengeneza nywele zangu!"
"Yees ! Zitengeneze vizuri ule mtindo ninaoupenda,
jioni nitapita hapo nikupeleke ukapate vikuku na
vikopo viwili vitatu!"
"Sawa darling ! Halafu dear, vipi kuhusu vile vitenge
vya Zaire wanavyopitisha wale kinamama niliokuambia! ?"
"Darling na wewe ! Si nilishakwambia wakipitisha tena
we chukua tu pea mbili halafu uniambie tu mimi
nitakupa pesa?!"
" Asante ! Na vile viatu je ?"
"Darling sasa unataka kuniudhi ! Nimeshakuambia kuwa
sio lazima uniombe ruksa kila kitu ! We chukua halafu
unaniambia..
 
Nitajitahidi nisiwe hivyo, yaani mimi nitakuwa malavudav mwanzo-mwisho.
 
wakwangu nitamwita darling, sweetheart, hny mpaka mwisho wa dahari

Habadilishwi m2 jina hapa!! Ni sweetie/darling kwa kwenda mbele...... wa kwangu nikimuita kwa jina lake halisi anajua kuna ishu ameitibua cos sio kawaida yangu!
 
nafikiri haya mambo ukitaka yaendelee, yataendelea tu, ni jinsi wewe mwenyewe unavyomuhandle jamaa.
wanawake msiwe mnagombeza gombeza waume zenu, mna wa put off!
we ongea naye taratibu hata kama anakuuzi, atalainika mwenyewe.
 
mh lakini neno darling/swt kuyarudia rudia kwa mtuu huyo huyo yanachosha, inafika siku especialy akitokea darling mpya unakuwa hulitamki tena labda ukituma msg ulimi unakuwa mzito kulitamka.
Kwenye ndoa mnavyopata mtoto mama anahamishia hayo maneno baby, darling... kwa mtoto so na baba inabidi utafute pa kuyahamishia ili muende sawa...lol
 
Huenda wenzetu nchi hizoooo..baadhi yao hufanya mahusiano haya kuwa ni mkataba wa kipindi fulani
hofu na mashaka ni kuogopa kufikia hapo ktk mizozo,kuchukiana n.k
 
hahahaaa...!!. safi sana, nimeipenda hii. ukiona hivyo ujue penzi limekuwa mature hamna mchezo tena, ukikosea kofi ukileta mzaha kwenu.hapo kubali ukatae utakuwa mpole tu. Mia
 
aliniambia ' baby siku izi hunitumii tena sms nzuri nzuri' nikamwambia mi sio mtunzi wa mashairi kutunga tunga visentensi kama ivyo. am not good in that.
 
nimegundua kitu,hata mama pia kabadilika jamani tusiwalaumu tu wanaume,nimejaribu kufuatilia lugha ya mama na yenyewe sio ile lugha ya miaka ileee akiwa mchumba,mama kasalimiwa "hujambo" kajibu sijambo,za kazi" ili nimtetee mama alitakiwa ajibu"sijambo mume wangu,za kazi darling,au honey au baby au sweet au vyovyote kama wenyewe walivyozoea.Hapa inaonesha wote washakua butu,mmoja akirudi nyuma mwenzake anatakiwa amvute mwenzke mbele kwa kumuonesha upendo utakaofanya akumbuke jinsi ilivyokua raha wkt mnapendana sasa baba kabadilika anajibu kijeshi na mama naye anapokea kimwanamgambo kwanin baba asinaswe na lugha tamu za nyumba ndogo.Sisemi baba anafanya vizur lkn kwa vile ndiye anayelaumiwa hapa ilibidi mama ndio aoneshe mfano mzur.
 
wa kwangu namwita mamayoyoooo kwisha kazi.
utawanyenyekea utaweza?kajaribu kwenda serengeti ukapande mgongoni mwa tembo kisa uliona india wakiwapandia uone kichapo yake.
punda wa ulaya haya bakora hawazijui.
 
mh lakini neno darling/swt kuyarudia rudia kwa mtuu huyo huyo yanachosha, inafika siku especialy akitokea darling mpya unakuwa hulitamki tena labda ukituma msg ulimi unakuwa mzito kulitamka.
Kwenye ndoa mnavyopata mtoto mama anahamishia hayo maneno baby, darling... kwa mtoto so na baba inabidi utafute pa kuyahamishia ili muende sawa...lol


sawa na avatar yako
 
Back
Top Bottom