Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,230
- 13,415
Wakuu najua kwa namna moja ama nyingine mmepata usumbufu wa takribani dakika 120 na ushee hivi kwa kukutana na ujumbe ambao huenda haukueleweka kwa wengi na ulikuwa si mzuri.
Kuna mtu kajaribu kufanya alichofanya na kukifanikisha kwa muda mfupi huo amewatumia emails walio wengi na kuambatanisha link anayodai haina virus hata kama inaelekea ina virus. Ukweli link hiyo si salama kabisa!
TAHADHARI: Usibonyeze link hiyo (DO NOT CLICK IT) kwani si salama. Haijatumwa na uongozi wa JF na wala hatuombi michango kwa njia ya barua pepe!
Aidha, namshukuru mkuu Fidel80 kwa kunifahamisha juu ya kilichokuwa kinaendelea na kusababisha nigeuze gari haraka na kurudi ofisini kuchukua hatua haraka.
Tunaomba endapo wanachama mnakumbana na jumbe ambazo hazieleweki tuwasiliane aidha kwa njia ya barua pepe ama kwa simu moja kwa moja ili hatua za haraka na za makusudi zichukuliwe kushughulikia tatizo.
Tatizo hili limetatuliwa na tunaahidi kuhakikisha halitokei tena na kuomba ushirikiano wenu katika kutufahamisha juu ya matukio kama haya. Poleni kwa usumbufu uliojitokeza na nirudie kuwatahadharisha kutobonyeza links zozote zilizoambatana na email ya awali.
Tutawaandikia email baadae lakini kwa uungwana tumeona ni vema kuwafahamisha kuwa tatizo tumeliona na kulichukulia hatua na kuwaomba radhi kwa usumbufu pia kuwahadharisha na kubonyeza link iliyoambatanishwa kwenye barua pepe hiyo.