Kumradhi wakuu...

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,196
13,187
Wakuu najua kwa namna moja ama nyingine mmepata usumbufu wa takribani dakika 120 na ushee hivi kwa kukutana na ujumbe ambao huenda haukueleweka kwa wengi na ulikuwa si mzuri.

Kuna mtu kajaribu kufanya alichofanya na kukifanikisha kwa muda mfupi huo amewatumia emails walio wengi na kuambatanisha link anayodai haina virus hata kama inaelekea ina virus. Ukweli link hiyo si salama kabisa!

TAHADHARI: Usibonyeze link hiyo (DO NOT CLICK IT) kwani si salama. Haijatumwa na uongozi wa JF na wala hatuombi michango kwa njia ya barua pepe!

Aidha, namshukuru mkuu Fidel80 kwa kunifahamisha juu ya kilichokuwa kinaendelea na kusababisha nigeuze gari haraka na kurudi ofisini kuchukua hatua haraka.

Tunaomba endapo wanachama mnakumbana na jumbe ambazo hazieleweki tuwasiliane aidha kwa njia ya barua pepe ama kwa simu moja kwa moja ili hatua za haraka na za makusudi zichukuliwe kushughulikia tatizo.

Tatizo hili limetatuliwa na tunaahidi kuhakikisha halitokei tena na kuomba ushirikiano wenu katika kutufahamisha juu ya matukio kama haya. Poleni kwa usumbufu uliojitokeza na nirudie kuwatahadharisha kutobonyeza links zozote zilizoambatana na email ya awali.

Tutawaandikia email baadae lakini kwa uungwana tumeona ni vema kuwafahamisha kuwa tatizo tumeliona na kulichukulia hatua na kuwaomba radhi kwa usumbufu pia kuwahadharisha na kubonyeza link iliyoambatanishwa kwenye barua pepe hiyo.
 
shukrani mkuu make nilisnhangaa lakini bahati yangu hiyo email iliingia kwenye spam folder so nikai delete straight.
 
Mimi nilishtukia kuwa kanyaboya kutokana na lugha katika hio message,English utata, tafsiri ya kiswahili ndio uozo kabisaa!
 
Kuna mtu kajaribu kufanya alichofanya na kukifanikisha kwa muda mfupi huo amewatumia emails walio wengi na kuambatanisha link anayodai haina virus hata kama inaelekea ina virus. Ukweli link hiyo si salama kabisa!
Aiseee hiki kijamaa hata mie kimenitumia.....nishakihisi kwa ile english yake ya ugoko....inabidi watu wapewe shule ya bure juu ya hizi link ambazo tunatumiwa....
 
Wacheni woga ,si unakong'oli tu ,maana zama za kutishana zimepitwa na wakati ,mi huwa nafungua kila kitu ,na kwa vile system yangu iko ngangari kinoma ,akuna kidudu kinachoweza kupenya bila kuvutwa ukosi na kuwekwa pembeni,mambo yakizidi naformat alafu navuta backup narudi tena uwanjani na porogaramu zangu zote zinakuwa uptodate. Kwa ufupi kila mwisho wa wiki nafanya backup ya pc na kuweka pembeni.
 
Hata mi nishakijua tena kimo humu ndani!!
 
Aiseee hiki kijamaa hata mie kimenitumia.....nishakihisi kwa ile english yake ya ugoko....inabidi watu wapewe shule ya bure juu ya hizi link ambazo tunatumiwa....

Nitaigalagaza kompyuta yako...wewe subiri tu
 
Wacheni woga ,si unakong'oli tu ,maana zama za kutishana zimepitwa na wakati ,mi huwa nafungua kila kitu ,na kwa vile system yangu iko ngangari kinoma ,akuna kidudu kinachoweza kupenya bila kuvutwa ukosi na kuwekwa pembeni,mambo yakizidi naformat alafu navuta backup narudi tena uwanjani na porogaramu zangu zote zinakuwa uptodate. Kwa ufupi kila mwisho wa wiki nafanya backup ya pc na kuweka pembeni.

Mkuu PC yako iko ngangari, je za wengine unafikiri ziko kama ya kwako? Watu lazima wachukuwe tahadhari.......acha ku-discourage watu linapokuja suala la safety/security.
 
Wacheni woga ,si unakong'oli tu ,maana zama za kutishana zimepitwa na wakati ,mi huwa nafungua kila kitu ,na kwa vile system yangu iko ngangari kinoma ,akuna kidudu kinachoweza kupenya bila kuvutwa ukosi na kuwekwa pembeni,mambo yakizidi naformat alafu navuta backup narudi tena uwanjani na porogaramu zangu zote zinakuwa uptodate. Kwa ufupi kila mwisho wa wiki nafanya backup ya pc na kuweka pembeni.
Acha Ubishi wewe ukiambiwa kitu, Kila siku unakuwa mbishi sana
 
Wacheni woga ,si unakong'oli tu ,maana zama za kutishana zimepitwa na wakati ,mi huwa nafungua kila kitu ,na kwa vile system yangu iko ngangari kinoma ,akuna kidudu kinachoweza kupenya bila kuvutwa ukosi na kuwekwa pembeni,mambo yakizidi naformat alafu navuta backup narudi tena uwanjani na porogaramu zangu zote zinakuwa uptodate. Kwa ufupi kila mwisho wa wiki nafanya backup ya pc na kuweka pembeni.

Hayo ni wewe unaweza kurisk na kufanya hayo unayofanya, si wote tunasystems na utalaam ulio nao.......so ni bora tuchukue tahadhari kabla madhara hayajatupa kama wakuu wanavyotushauri!
 
Huyu jamaa aliiteka JF kwa muda jana..ilikuwa nikifungua site nakumba na ujumbe. Kumbe link ilikuwa kirusi mbaya. Duh..
Tunashukuru Max kwakutuhabarisha.
 
Hata miye niliyaona!, nikapata kigugumizi kidogo, nikahisi labda ya bcstimes.com yameingia hapa (yaani JF no basi tena)! Nilijipa moyo na ile link nikawa naishuku tu.

Kwa kiasi kikubwa mimi nahisi ni hao miungu watu wa tz (yaani ma fisadi), ambao wanajaribu kurusha makombora yao:confused:
 
Wacheni woga ,si unakong'oli tu ,maana zama za kutishana zimepitwa na wakati ,mi huwa nafungua kila kitu ,na kwa vile system yangu iko ngangari kinoma ,akuna kidudu kinachoweza kupenya bila kuvutwa ukosi na kuwekwa pembeni,mambo yakizidi naformat alafu navuta backup narudi tena uwanjani na porogaramu zangu zote zinakuwa uptodate. Kwa ufupi kila mwisho wa wiki nafanya backup ya pc na kuweka pembeni.
mwiba kuwa muangalifu, mdudu akiwa latest antivirus unakuta saa ingine haikamati mpaka wamtafutie suluhisho
juzi bosi wetu katupa kompyuta tano mdudu alishambulia network
 
Jamani sasa sisi tulio-click tukizani tunasaidia JF tufanyaje?maane nili-click kiroho mbaya sio mara moja au mbili tu!nisaidieni kuokoa kakompyuta kangu!
 
Pole man, labda tuanze kukuchunguza wewe mwenyewe.
ULipo-click ile link uliona athari gani ktk computer yako??? au ilifunguka page gani???

Ushauri wa bure tu, jaribu ku-update Antivirus yako unayotumia then Scan full system.

Next time epuka sana ku-click link ambayo mtumaji humjui, jengine ile link ina extension ya .exe (ina-maana ulipo-click kuna kitu ume-install ktk pc yako)

Jioni njema
 
mm nimeifutilia mbali kwa kua najuwa tangazo lolote la michango na ghasia zinazohusu JF nitazikuta hapa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom