Kumiliki akaunti ya fedha nje ya nchi

ral

Senior Member
Dec 30, 2009
133
37
Wadau wa JF salaam,
naomba kujuzwa maana labda mie nimesahau, nakumbuka katika nchi yetu kuna sheria ilikuwepo sijui kama ilishaondolewa au la, sheria yenyewe ni kuwa inakataza mtanzania aliyepo nchini kumiliki akaunti ya fedha nje ya nchi. Je hii sheria ilishafutwa au bado ipo? Natanguliza shukurani
 
Mwanakiji tunaomba ufafanuzi wa hili suala la watu kumiliki Vijisenti (a.k.a Chenge) nje ya nchi, kuna sheria ihusuyo jambo hilo?
 
sheria zakijamaa hazina ishu

Ujasoma shule vizuri ukagunduwa faida na hasara zakuweka fedha mtu binafsi nje ya nchi. Nilazima ujuwe kwa kadiri mtu anapokuwa na fedha ya halali na kuiweka bank anaiongezea bank uwezo wa kukopesha tena ata kuwa na uwezo wa kuikopesha serikali. Na hili lipo ktk money loundering act if i'm not mistake. Israel wazir alijiuzulu ktk kashifa kupokea fedha kutoka nje. What about us wale wanapeleka ktk ma bank ya nje?
 
Wadau wa JF salaam,
naomba kujuzwa maana labda mie nimesahau, nakumbuka katika nchi yetu kuna sheria ilikuwepo sijui kama ilishaondolewa au la, sheria yenyewe ni kuwa inakataza mtanzania aliyepo nchini kumiliki akaunti ya fedha nje ya nchi. Je hii sheria ilishafutwa au bado ipo? Natanguliza shukurani

Kama nakumbuka vizuri miezi michache iliyopita Governor wa BoT Ndullu alidai sheria hii bado ipo, lakini ipo kiushahidi shahidi tu maana Watanzania wengi tu hasa Viongozi wa juu Serikalini sasa hivi wengi wana bank accounts za nje ya nchi katika nchi nyingi tu. Na hata yule Mzee wa Vijisenti na Idrissa Rashid mapesa yao ya ufisadi wa ununuzi wa RADA waliyaweka katika bank ya nchi za nje.
 
Ujasoma shule vizuri ukagunduwa faida na hasara zakuweka fedha mtu binafsi nje ya nchi. Nilazima ujuwe kwa kadiri mtu anapokuwa na fedha ya halali na kuiweka bank anaiongezea bank uwezo wa kukopesha tena ata kuwa na uwezo wa kuikopesha serikali. Na hili lipo ktk money loundering act if i'm not mistake. Israel wazir alijiuzulu ktk kashifa kupokea fedha kutoka nje. What about us wale wanapeleka ktk ma bank ya nje?
!!!..?
 
Na kwa kuongea mi ninavyojua Chenge na Idrissa hawajawahi kufanya biashara zaidi ya kusubiri tarehe 25 ya kupokea mshahara ndipo nao wapate vijisenti vyao na pia hawajawahi kufanya kazi nje sasa hivyo vijisenti vyao walivyovificha huko ughaibuni wamevipataje?tena hivyo visenti vimeingizwa kwenye hizo account sambamba na malipo ya rada,sasa mpaka hapo Takukuru,usalama wa Taifa,tume ya maadili ya viongozi sijui hivyo vyombo vinafanya kazi gani?kwa hayo tu hawa jamaa walitakuwa wangekuwa wanashinda pale Kisutu na akina Mramba,lakini ajabu hawaguswi eti,jamani hii serikali imejishusha hadi chini kwa kuwanyenyekea watu wachache huku maslahi ya wengi yakipuuzwa
 
Sidhani kama kuna hiyo sheria, ili mradi kuna sababu halali za kutoa hela nchini, mimi nina account nchi mbili right now na sijawahi kuulizwa lolote na benki yangu.
 
Back
Top Bottom