Kumekucha: Wachina watinga Ludewa kuanza kazi ya madini

Jambo hili lilishajadiliwa hapa miezi michache iliyopita, na faida ambayo sisi tutapata ni bora kuliko wachimba madini wengine. Wachina ni bora kuliko hawa wa kutoka mataifa ya magharibi.
Hamna kitu hawa Wachina ni wanadharau sana wanachapa mpaka viboko wafanyakazi pili wanaleta mpaka mtu wa chini ambaye mtanzania wa kawaida anaweza kuifanya hiiyo kazi mfano grader operator,dumper nk,pili wanalipa mishahara midogo sana tena kwa unyanyasaji wanaongoza kampuni kama BARRICK au kusini kwa Waaustralia huwezi kulinganisha na Wachina sana sana huko Watz wanakimbila kidebe cha mafuta halafu Kwa Mchina hata security ya kazi hakuna cha HR yaani hata fundi mekanika anaweza kukufukuza kazi yaani hao hakuna kabisa hata safety ni ziro utasikia watu watakavyo kufa au kuathirika na mgodi na sijui sheria zetu zinatulinda vipi ukimuuliza huyo Filikunjombe sidhani kama anajua hilo asifurahie kuja kwa Wachina baadae watz wa Ludewa waje wamlilie
 
I will keep these picture kwani kesho huyuhuyu deo anaweza kuja kulalama bungeni kwamba wachina wanaiba rasilimali zetu, ingawa leo anawababikia kama mabwana zake
 
Sioni cha kufurahia hapo, mie nilitumaini kwamba chuma kitakochimbwa hapo kingetumika hapahapa nchini kwa ajili ya 'heavy industrialization' kumbe kinakwenda kuwanufaisha wachina na sisi kuambulia uchafuzi wa mazingira na mishimo mikubwa.

Nini kinahamasisha uanzishwaji wa viwanda hapa nchini iwapo hakuna mali ghafi. Madini hayo ni moja na chanzo cha viwanda nchini kwa vile mradi huo una lengo la kujenga viwanda vya kuprocess madini hayo hapa hapa na kitakachosafirisha ni kutoka viwandani na wala si kutoka machimboni.

Kwa nini makampuni mengi yaliogopa kuchimba madini kule Mchuchuma na Liganda? Madini ya chuma na makaa ya mawe si kama dhahabu na Tanzanite ambayo unaweza kuiweka mfukoni au kwenye handbag. Ni matani ambayo hata kuiba ni vigumu, ndio maana wachina wanaanzisha viwanda vya kusafisha chuma hapa hapa, na pengine hata utengenezaji wa mataluma ya reli ukafanyka hapa kisha bidhaa ndizo zisafirishwe,

Tuwe tunaona mbali badala ya kulalamika tu, tunachosha nyongo mwisho zitapasuka wakati wenzetu wako tayari kutusaidia kufikia malengo.
 
Hamna kitu hawa Wachina ni wanadharau sana wanachapa mpaka viboko wafanyakazi pili wanaleta mpaka mtu wa chini ambaye mtanzania wa kawaida anaweza kuifanya hiiyo kazi mfano grader operator,dumper nk,pili wanalipa mishahara midogo sana tena kwa unyanyasaji wanaongoza kampuni kama BARRICK au kusini kwa Waaustralia huwezi kulinganisha na Wachina sana sana huko Watz wanakimbila kidebe cha mafuta halafu Kwa Mchina hata security ya kazi hakuna cha HR yaani hata fundi mekanika anaweza kukufukuza kazi yaani hao hakuna kabisa hata safety ni ziro utasikia watu watakavyo kufa au kuathirika na mgodi na sijui sheria zetu zinatulinda vipi ukimuuliza huyo Filikunjombe sidhani kama anajua hilo asifurahie kuja kwa Wachina baadae watz wa Ludewa waje wamlilie

Wachina hawa tunacho walichokwisha kifanya ambacho wanatokea kifua mbele kujivunia. Jiulize ni taifa gani limefanya makubwa katika maendeleo hapa Tanzania? Miradi mkubwa ninayoifahamu ni Wachina na Wajapani. Wazungu longo longo nyingi na kutafura miradi ambayo madini yake ukichimba ni rahisi kuyaficha mifukoni kuliko miradi mikubwa kama hii. Nipe hoja ya kupinga utetezi wangu huu ambao wazungu tangu tupate uhuru kama wamejenga reli, viwanda na barabara, ila wachina na Wajapani.
 
Rasilmali zako na nani? rasilmali zako unazo mwenyewe.

Mwenyeezi Mungu kaweaka haya madini huku chini ya ardhi kwa maana zake. Wewe umewekewa lakini huna ujuzi wa kuyachimbuwa, mwenzako kapewa ujuzi lakini hana hayo madini, na huyo anaeyachimbuwa anategemea ataeyatumia. Hivyo ndivyo inavyokuwa. Na usifikiri yanakwisha au yanapotea, la hasha, yanatumika na yanapatikana kwa vipimo vilivyokadiriwa. Na yana umuhimu kwa wakati wake tu na si kila siku. Wacha roho dhaifu.

Wameacha kina fiauni itakuwa wewe? wameacha kina Suleiman, itakuwa wewe? wewe kama unauwezo kachimbe tumia, ukiondoka wenzakao watayakuta amma umeshayachimba au hujayachimba.

Tena nikuambie, hao wababe bora ukae nao mezani mkubaliane kwani ukijidai kuwanyima, unayakalia tu, yatakukuta yaliyowakuta wengi tu. Mwenye macho haambiwi tazama.

kama hizi ndo akili za wana ccm, cshangai kwa nn leo tumefika hapa!
 
Kutusaidia?

Yes, maana wenyewe tumeshindwa ila maneno mengi bila vitendo. Tumesomesha watu tangu mika 50 iliyopita hakuna cha maana wanachofanya ila longo longo tu, sasa tunawalaumu wachina wanaoonyesha utendaji badala ya wasomi wetu wanaoanika elimu yao kwenye makaratasi bila utendaji. Hatujaamka, labda wakiendelea kunyofoa utajiri wetu ndio tutaamka, tumekalia utajiri tukiwa maskini bila kutumia utajiri huu kujikwamua kutoka umaskini.
 
Mkuu naona akili yako imekaa ki-kusaidiwa saidiwa. Ni kama vile umeshakubali kushindwa. Kama hayo ndo mawazo unayotaka tuendelee kuwa nayo basi ina maana tutaendelea kulala kwa miaka 400 mingine. Nachangia!
 
NDC walikabidhiwa mradi huo miaka zaidi ya 20 na hakuna cho chote kilichofanyika licha ya kupewa bajeti kila mwaka. Wameshindwa hata kuchimba kidogo kwa uwezo wao kulisha viwanda vya kutengeneza nondo vya pale Dar na Tanga. Sasa utetezi wako uko wapi kama si ubishi? Hata chuma cha kutengenezea nondo za kujengea tunaagiza nje wakati tuna madini nje nje yametanda wilaya nzima ya Ludewa na wala hayahitaji kuchimbwa mahandaki kuyaibua, ni mawe ya chuma na makaa juu juu tu, utetezi wako dhaifu. Bora tukubali tu mabingwa wa nadharia wakati tu dhaifu wa vitendo.
 
[h=3]KANISA LAWATAKA WABUNGE BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
KUIGA MFANO WA MBUNGE FILIKUNJOMBE
[/h]
DSCF5314.JPG
DSCF5315.JPG
DSCF5317.JPG

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ludewa mjini limewaanya wabunge wa bunge la Jamahuri ya muungano wa Tanzania kuwa iwapo wataendelea kugeuza ubunge ni sehemu ya kujilimbikizia mali na kujinufaisha wenyewe kuwa ubunge wao utakuwa wa kipindi kimoja pekee na wataendelea kuchukiwa na wananchi daima.

Kauli hiyo ilitolewa na mchungaji wa kiongozi wa kanisa Kilutheri usharika wa Ludewa Ebron Misitu wakati akimpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi (CCM)Deo Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano katika jimbo hilo na mkoa wa Iringa katika kutekeleza ahadi zake kwa wakati na kuwataka wabunge wengine kuepuka kutumia nafasi ya ubunge kujilimbikizia mali.

Mchungaji huyo alitoa kauli hiyo wakati wa ibada ya sikukuu ya Krismas iliyohudhuriwa na mbunge huyo Filikunjombe ambaye pia alipata kutimiza ahadi ya mchango wake kiasi cha shilingi milioni 1 kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa kanisa hilo.
 
I personally respect the workmanship of our Chinese peers and remain optimistic with the task ahead of them.
 
I personally respect the workmanship of our Chinese peers and remain optimistic with the task ahead of them.

Unao upeo pekee kuona pande zote mbili za coin, vinginevyo tutaendelea na kinogaubaga, hakuna chema tunachokiona ila malalamiko yasiyo na tija kwa kila kitu, je tutaendelea kwa mtindo huu?
 
Heee mara sifa zimekuwa za mbunge Filikunjombe? watu wamepiga kelee wee bungeni kuhusu matatizo ya Umemem nchini mara imekuwa mradi wa mbunge?...Haya lakini kitu kimoja tu nami naongezea. Kwa utawala tuliokuwa nao sasa hivi mradi huu utakuwa namadhambi makubwa kuliko hata Barricks na athari zake hazihesabiki maana tunacheza na nuklia bomb sasa hivi.. Watu watakufa na maradhi ya ajabu ajabu, Ludewa kutakuwa hakioti kitu, maji hayatanyweki yaani naogpa sana kusikia mradi huu unafanywa na wawekezaji ambao wapo nchini kutengeneza FAIDA...

Inshaalah Mwenyezi Mungu akituweka haki ten yrs from now tutayazungumza tena sijui ktk kijiwe gani lakini myakumbuke maneno yangu. Kweli kabisa tunahitaji uwekezaji huu na muhimu sana lakini nachelea kusema kwamba mtoto wetu kaanza uhuni mapema...
 
Ahsante sana Mkuu.
 
Vitisho vya nini? Hili bomu la nuklia lingewezekana wangeshaliona mapema kwani wale wa 10% hulichangamkia sana, sasa hawa jamaa wanaofuata haki tupu wakawakwepa na kuendelea na danadana, hadi upenyo ulipopatikana Jairo yuko nje mambo yamenyooka na bila ila ya 10%.

Wengi wanaopinga hili ni wale wafuasi wa 10% ulaji umewapita kisogoni na mambo yanaendelea mdundo. Kama una ndugu wapeleke kule Ludewa maana tumehakikishiwa ajira ya 8000 soon, sasa nini mnataka kama yale ya barricks yasiyo na ajira? Kama barricks wangetoa ajira kwa raia vita visingekuwepo, na hii itajidhihirisha kule kwa wachina Ludewa. Wa 10% wakijiingiza wajue namna ya kujitetea kungfu na karet, ndo wachina hao hawana longo longo.
 
Nawapa pole sana, maana mpaka kuzoea! Ila kama mradi ni 50 kwa 50 hongera Mh Njombe ila kama kuna wizi nadhani wanajombe watakuja wakudunde mawe!
 
Kuendelea kufumba macho hakutusaidii maana pamoja na utajiri mkubwa tuliokuwa nao katika rasilimali mbali mbali wanaofaidika ni wageni na sisi tukibaki bila maendeleo ya kweli.
Wa Tanganyika mumelala usingizi Amkeni jamani lohhhhhhhhhhhhhh MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wa Tanganyika mumelala usingizi Amkeni jamani lohhhhhhhhhhhhhh MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO.

MziziMkavu you are right!

Malalamiko hayatatuondolea umaskini, bali utendaji. Tulikuwa tunalalamikia wasomi, sasa tunao mambo ndio yanaharibika zaidi afadhali tulipokuwa hatuna wasomi, malalamiko haya tuyaelekeze kwa wasomi na serikali badala ya kuwalalamikia hawa wawekezaji, kwani tulitangaza tenda, na kama we unayepinga ulikuwa na uwezo kwa nini hukuchukua tenda halafu leo ulalame kwamba tunaibiwa? Walionyesha uwezo wa kuchukua tenda kadiri ya masharti ya tenda, kama kosa ni sisi tuliowapa tenda na wala si wageni wanaochukua tenda.
 
Vitisho vya nini? Hili bomu la nuklia lingewezekana wangeshaliona mapema kwani wale wa 10% hulichangamkia sana, sasa hawa jamaa wanaofuata haki tupu wakawakwepa na kuendelea na danadana, hadi upenyo ulipopatikana Jairo yuko nje mambo yamenyooka na bila ila ya 10%.

Wengi wanaopinga hili ni wale wafuasi wa 10% ulaji umewapita kisogoni na mambo yanaendelea mdundo. Kama una ndugu wapeleke kule Ludewa maana tumehakikishiwa ajira ya 8000 soon, sasa nini mnataka kama yale ya barricks yasiyo na ajira? Kama barricks wangetoa ajira kwa raia vita visingekuwepo, na hii itajidhihirisha kule kwa wachina Ludewa. Wa 10% wakijiingiza wajue namna ya kujitetea kungfu na karet, ndo wachina hao hawana longo longo.
Mkuu ningekuomba tu unisome between the lines.. Nacho maanisha ni kwamba mradi huu una madhara makubwa sana sawa na bomu la nuklia kwetu.. Mafuriko yaliyotokea Dar nchi hizi ni sawa na bomba la maji jikoni..Simtishi mtu isipokuwa lazima tuweke tahadhali..

Mpango huu umepita jaitro akiwepo unachozungumza nini haswa... Rais na mawaziri wote mnaowaona wabovu ndio wamewezesha mradi huu kwa hiyo msitake kuwapa sifa watu wengine wakati wale wale wa 10% ndio wameweka saini..Hilo wala sii neno kwangu na wala halinitishi isipokuwa kikubwa zaidi kwangu ni UFISADI uliopo kwa mradi huu utagharimu maisha ya watu na mazingira kwa sababu kuchimba makaa ya mawe sio sawa na kuchimba Tanzanite wala dhahabu..

Inatakiwa makni ya hali ya juu sana maana hata Ulaya mwenyewe ipo miradi mingi yamakaa ya mawe imefungwa kutokana na madhara ya miradi hii...Hivyo kweli tunahitaji makaa ya mawe lakini Je, tumejiweka vema kukabiliana na madhara yake maanake hatuna tabia ya kudhibiti usalama wa wananchi..Meli zinazama hatuna mpango wa kuhakikisha haitokei tena, hiyo malaria tu tumebambikwa vyandarua na show za clouds..samahani Joe na Ruge wangu watanisamehe!

Jamani mnafanya mchezo na maisha ya watu nyie! sijui tumejiandaa vipi kuhakikisha madini yatokanayo na makaa ya mawe yanadhibitiwa vizuri na kuhakikisha vyanzo vya maji havipati madini hayo...Hao waajiriwa 8000 how long wataishi na Je, ikitokea maisha ya watu wa Ludewa wanakufa na maradhi yasiyojulikana hizo ajira zitalipa vipi?

Tumeshidnwa kuleta umeme wa dharura mega watts hazifiki hata 300 kwa mji mmoja tu for the past 6 years na bado tunahesabu siku na miaka, leo mnataka kunambia waamuzi wale wale wa mipango ile wataweza haya makubwa ?..
 
Back
Top Bottom