Kumekucha: Wachina watinga Ludewa kuanza kazi ya madini

..tatizo watu wanafikiri wachina wa leo hii ni kama wale waliojenga Tazara.

..hawa wa sasa hivi wako zaidi kibiashara. they r just as greedy as westners.

..ukizingatia sheria zetu za madini, na aina ya viongozi wanaozisimamia, this is not the right time kwa nchi hii kusaini mkataba wowote ule wa madini.

Hawa wamekuja kufanya kile kilichomo kwenye mkataba, na wachimba madini wengi wanahcofanya ni kile kilichomo kwenye mikataba vinginevyo wangshtakiwa. Sio umeona tunavyohangaika sasa namna ya kuwasimamisha kwa vile tulishajivunga na kifundo cha mikataba.

Kosa tunafanya wenyewe halafu ndio tunaanza kulalamika, basi wekeni utaratibu mzuri wa mikataba badala ya kulalamika. Wachina wa miaka ile kama unaona walifanya vizuri ni kutokana na umahiri wa waandaaji wa mikataba walikuwa wanaweka utaifa mbele badala ya masilahi binafsi.
 
Mikataba ya madini na ufuatiliaji wa idara za serikali mara zote ni mbovu.Tufike wakati tuwe na Stop Policy ya kusimamisha shughuli zote za madini tunapo hisi umma hautendewi haki.
 
Candid Scope,

..hata wewe mwenyewe umeshindwa kusema kwamba mkataba huo ni mzuri.

..the best u have done ni kusema mkataba huu siyo mbaya kama ile tuliyosaini kwenye uchimbaji wa dhahabu.

..sheria zetu ni mbaya,viongozi wanao-negotiate mikataba hawana ujuzi na utaalamu, na zaidi hawaweki maslahi ya taifa mbele.

..Wachina wa leo hawana ubinadamu tena. wapo zaidi kibiashara na kibepari, kama mnabisha angalieni walichofanya Sudan ya Kusini na DRC.
 
Kuna mambo mawili tofauti, mikataba kama ya Mchuchuma- Ligannga na watu binafsi au kiundi kisichokuwa na malengo makubwa kitaifa ila kutafuta kinachopatikana kujinufaisha.

Hawa Wachina nawapa credit katika mambo mengi waliyofanya kuanzia ujenzi wa TAZARA, hakuna taifa lo lote la Magharaibi ambalo limefanya shughulu kubwa ya kiuchumi ukilinganisha na hawa wachina.

Kusaini mkataba wa 20% to 80% bado ni wizi tu tena mkubwa. Sijui ni vigezo vipi vilivyotumika hadi nchi kuambulia 20% tu na wageni kuondoka na mara nne zaidi ya kile ambacho nchi itaambulia, kwanini haikuwa hata 45% to 55%!?. Miaka hiyo iliyojengwa TAZARA hawa Wachina walikuwa wanatoa msaada wa kweli na siyo kama ilivyo katika miaka ya karibuni ambapo hawaingii mahali ambapo na wao kama nchi hawawezi kuneemeka.

Tanzania, China in $3bn mining deal

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ingine-wa-kijinga-liganga-na-mchuchuma-4.html
 
Jambo hili lilishajadiliwa hapa miezi michache iliyopita, na faida ambayo sisi tutapata ni bora kuliko wachimba madini wengine. Wachina ni bora kuliko hawa wa kutoka mataifa ya magharibi.

Hawa wa Magharibi baada ya muda watatafuta mbinu ya kutuletea vita ama vya wenyewe kwa wenyewe au vita dhidi ya ukaidi ili kuwatupa nje hawa wa Mashariki.
Pata habari za peace corps zinazoletwa na US huwa pia ni majasusi ambao hutayarisha mazingira ya sintafahamu huku wakitugawia vyandarua na kujifanya wanafanya kazi ya kujitolea.

Huu urafiki wetu na CHINA iko siku Wenye mali (wale waliotufanya watumwa,wale walitutawala na wale wanaotuwekea serikali vibaraka na mifumo ya uchumi inayoturudisha nyuma) watasema, enough is enough.
 
Umeona ehe, Bushi kaja juzi kujipendekeza kwa vyandalua wakati wachina wanakuja kujenga reli na kuongeza umeme kwenye grid ya taifa, ni wachimba madini gani wenye project zenye kuleta manufaa kwa taifa? Ludewa kuna uhakika wa ajira ya 8000 kwa mwaka wakti migodi mingine wanawaua wananchi kwa kutowajali.
 
Hawa wa Magharibi baada ya muda watatafuta mbinu ya kutuletea vita ama vya wenyewe kwa wenyewe au vita dhidi ya ukaidi ili kuwatupa nje hawa wa Mashariki.
Pata habari za peace corps zinazoletwa na US huwa pia ni majasusi ambao hutayarisha mazingira ya sintafahamu huku wakitugawia vyandarua na kujifanya wanafanya kazi ya kujitolea.

Huu urafiki wetu na CHINA iko siku Wenye mali (wale waliotufanya watumwa,wale walitutawala na wale wanaotuwekea serikali vibaraka na mifumo ya uchumi inayoturudisha nyuma) watasema, enough is enough.

Ahsante sana Mkuu.
 
Mbunge ndio anawapokea nilidhani wangepokelewa na Mbunge pamoja na mtu wa wizara yenye dhamana ya nishati na madini ama mtu toka NDC! Yote kheri inanikumbusha makala moja niliyoisoma inayosema "From Brettonwoods to China".

hata mimi imenikumbusha hiyo habari
 
Acha kusema eti Wachina ni ndugu zako, na kamwe usijifariji eti angalau wachina, naona wewe hujafuatilia mienendo ya wachina kwa sasa, jamaa wamebadilika kuliko hata hao wazungu,

kawaulize watu wa Zambia kwenye shaba kabulahawajampata SATA wao, jamaa hata mfagia ofisi wanamtoa kwao, na subilini mtaona migogoro ya arthi huko Ludewa, si kwa sasa kumetulia, angalieni sehemu kama Shinyanga,Tarime, Manyara, Arusha na kwingineko kwenye madini, napia Filikunjombe asipende kujiingiza kwenye kashifa ya badaae kwani ilishathibitika kuwa hata mkataba wenyewe umejaa ufisadi, mimi nawaomba sana muwe waangalifu na rasilimali za nchi yetu, na msiwatukuze wachina sana kwani siku hizi nitofauti na zamani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watatafuta namna ya kuiba madini haya na kuyapeleka kwao. Nchi nyingine mwekezaji anaambiwa alete labda 5% tu ya Wataalamu na wengine wote wawe ni local experts lakini kwetu inakuwa ni vice versa si ajabu wakati mwingine hata 100% ya wataalamu ni wageni!!!! Angalia kule Barricks kwa wachimba dhahabu.

Ndio maana hamuendelei. Nenda kayachimbe wewe ulikuwa wapi siku zote?
 
Ndio maana hamuendelei. Nenda kayachimbe wewe ulikuwa wapi siku zote?

Tumethubutu kufanya usanii tumeweza na sasa tunasonga mbele na usanii wetu. Kama unategemea kupata maendeleo kwa mikataba ya 3% to 97% au 20% to 80% utasubiri sana. Ni bora rasilimali zetu ziendelee kubaki ardhini kuliko kuingia mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanganyika. Dhahabu yetu ilianza kuchimbwa miaka 11 iliyopita (2000) kaangalie maeneo yenye dhahabu yalivyo bado nyuma kimaendeleo wakati shareholders wa Barrick na makampuni nyingine wanazidi kuneemeka kwa rasilimali za Bongo. Weye pia ulikuwa wapi kuchimba hiyo dhahabu au kule Mchuchuma?

Huyu Deo Filikunjombe hapa anawakodolea macho wachina kiulimbukeni balaa. Hamna tofauti na Chifu Mangungo. Safari yetu kwa kweli bado ni ndefu!

DSCF5515.JPG
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huyu Deo Filikunjombe hapa anawakodolea macho wachina kiulimbukeni balaa. Hamna tofauti na Chifu Mangungo. Safari yetu kwa kweli bado ni ndefu!

View attachment 44077
mkuu kweli huyu Filikunjombe kama hatakuwa makini atakuja kuibuka na bonge la kashfa. Wabunge wamegeuka kuwa watendaji au ndio kuonyesha kuwa kuna ombwe. Manake nilitegemea Mbunge awe oversight na siyo kuonekana yeye ndiyo yuko bega kwa bega na wanyonyaji no wawekezaji hao.
 
Hosea akiamua kumpigia mbizi kiuhakika sidhani kama huyu jamaa atapona!
 
mambo mengine bwana mbona siyaelewi. Mbunge.aliwapokelea wapi hao wageni? Mimi nlidhani aliwapokea na kuwapeleka ofisini kwake lakini pichani naona kama aliwapokelea bar manake naona vinywaji vikali aina ya safari vipo kabatini na vingine vimeishagidwa? Mambo yetu bwana tunayaongelea bar tena tukiwa tunakunywa unadhani tutapata tija kwa mtindo huu. Hayo ndiyo yanayotokea wajumbe wakienda kufanya makubaliano huko ughaibuni; wanapokelewa bar wanakunywa na kusakiziwa mabinti ambao wanawaahidi kuonana nao kesho yake. Unapangwa muda ambao jamaa atakuwa anajadiliana basi jamaa akianza tu kujadili anapigiwa simu na binti anaacha kujadili anapiga mkwaju ili amuwahi binti! Baadaye anakuja kugundua kwamba.amesaini mkataba ambao serikali itapata 3% ya mrahaba! Mambo ya baa hayo!
 
Jambo hili lilishajadiliwa hapa miezi michache iliyopita, na faida ambayo sisi tutapata ni bora kuliko wachimba madini wengine. Wachina ni bora kuliko hawa wa kutoka mataifa ya magharibi.
Mkuu mwizi ni mwizi tuuuu bila kujali ni Mchina au wa magharibi, wote wanatuibia na sisi tunasmile tu. Tumelaaniwa!!!!!!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi ni kweli viongozi wetu hawajatambua kwamba ukoloni tumeurudisha
mkuu tena afadhaki wakati wa mangungo masikini alikuwa hajui kusoma wala kuandika ila hawa wa sasa wanajua kusoma na kuanxikapamoja na kuhesabu lakini wanafanya mambo mabaya ambayo kama yangefanywa na akina mangungo, mkwawa, kinjeketile nk basi Tanzania isingekuwepo wala madini au wanyama. sasa hivi mangungo akifufuka atatamani atuue soe ili ahifadhi tunu za taifa.
 
Back
Top Bottom