Kumekucha, wachezaji wawili wote leo ndiyo wamebeba 'Majini na Hirizi' za Kuzibeba timu zao kwa Mkapa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,651
109,041
Na nawaombeni leo kabla ya Mechi kuanza kuweni makini kuangalia nini Watafanya au Kitafanyika ila Mpira ukianza tu watakuwa Wanakwepana.

Pia kuna uwezekano mkubwa Wote wakafunga Magoli kwa Timu zao ila Kuumia kiasi kwa Mmoja wao au sana ni kwa 85% kutokana na Mizigo ya HATARI ya Kishirikina waliyoibeba.

Akianza tu Kufunga Goli Mzanzibari Minywele jua Timu yake itashinda Goli kuanzia 3 ila akianza Kufunga Goli Mzanzibari Mrembuaji Macho na Mjilamba Midomo jua Mechi itaisha kwa 1 kwa 0 au Sare ya 1 kwa 1.

Kwa Siku za karibuni tumeona Vitendo vya waziwazi vya Kishirikina katika NBC Premier League ila kwa taarifa ambazo GENTAMYCINE nimepenyezewa kutoka ndani kwa pande zote mbili ni kwamba leo kuna Uchawi wa Kufuru umefanyika na mwingine utamalizika kufanyika pale pale Uwanjani.

Haya TFF iandaeni mapema ile Kamati yenu ya Kutoza Faini kutokana na Vitendo vya Ushirikina Viwanjani / Uwanjani kwani leo Ndumba itafanyika wazi wazi kwa Mkapa na wala Wahusika hawatojali Faini zenu japo najua Ndumba za leo zitawatajirisheni mno na najua hamtokosa hata Makosa ya Faini za kufikia Shilingi Milioni 25 hata hadi Milioni 50 hivyo hakikisheni 10% yangu haikosekani baada ya kuwapeni huu Mchongo wa kupiga Hela zisizokuwa na Kazi za Tajiri Tapeli Dhulumati Mkwepa Kodi na Tajiri Mkimya Mstaarabu Msaidia Watu ambaye Kabarikiwa na Mola.
 
Screenshot_20240317-162613.jpg
Screenshot_20240317-162613.jpg
 
Ukitaka kujua kuwa watu wengi wamebeba vichwa vyao kama water dispenser ya mate, wape nafasi ya kuongea n kuchangia hoja critically.

Hizi tuhuma ni upuuzi uliotukuka.
 
Ukitaka kujua kuwa watu wengi wamebeba vichwa vyao kama water dispenser ya mate, wape nafasi ya kuongea n kuchangia hoja critically.
Hizi tuhuma ni upuuzi uliotukuka.
Kuna mahala popote pale umelazimishwa Kuusoma huu Uzi? Idiot.
 
Na nawaombeni leo kabla ya Mechi kuanza kuweni makini kuangalia nini Watafanya au Kitafanyika ila Mpira ukianza tu watakuwa Wanakwepana.

Pia kuna uwezekano mkubwa Wote wakafunga Magoli kwa Timu zao ila Kuumia kiasi kwa Mmoja wao au sana ni kwa 85% kutokana na Mizigo ya HATARI ya Kishirikina waliyoibeba.
Mchawi katika ubora wako
 
Back
Top Bottom