KUMEKUCHA, Mramba amtaja Mkapa!

mmmhh!!!..hapa kazi ipo..kwanzaaa ndo muvi limeanza..kuna maadui na mastering...lets wait and watch..but it'l b very very interesting

I Just hope it's not an Indian Movie - wanalia na kuimba or rather Nigerian Movie - wanarogana, wanasali, wanaokoka...
 
picha la Kihindi linaaanza starring anakufa kwenye maua...patamu hapo..
 
Jamani mramba nasikia atagombea ubunge tena na campain za chinichini zimeanza rombo,mh! Hawachoki na kuridhika?
 
Ni wakati muafaka sasa Mkapa akajibu tuhuma zake kwani kujificha si dawa ni bora kujitokeza kuomba radhi kuliko kukaa kimya maana watanzania wataona ni dharau.
 
Kisheria ukiiangalia kesi hiyo kiaraka haraka unaona mpaka mwisho wake. Nisingependa kujadili sana kwa sababu shauri bado lipo mahakamani . Lakini Serikali kuthibitisha mashtaka yake ni vigumu sana labda wavunje sharia ( ya kutoa siri za balaza la mawaziri) na vile vile Bila Mkuu wa baraza la mawaziri kusimama kama mtuhumiwa au shahidi upande wa Serikali basi kesi hiyo ni mchezo wa kuigiza.


haya sie yetu macho.
 
Hakika Kazi ndio hiyo, Hizi zote ni kesi za danganyatoto maana hakuna cha kuweza kutofauti na maamuzi ambayo hata mzee wa nyumba naye alikuapo wakati ule, tutasikia mengi sana katika kipindi hiki maana ndio kesi za Uchaguzi
 
Kweli kuna kazi. Kusoma kote kwa Mramba amecheza mchezo mbaya kwa sababu Mkapa amemtosa kwa sababu there was nothing in writing from the State House therefore, how comes that he says it is Mkapa ? It might be anyone from the State House. Poor chap. Mramba na elimu yote anashindwa to tell Mkapa to have a small note from him ??? Haya ngoma nzito !!! Sasa kwa Mramba, hizo hotel ya Arusha ya nani kama sio zake ? Unajua hawa wenzetu wana weka watu wa vuli kama mali yao kumbe kuna wakubwa nyuma yao.

Sisi wananchi tunataka haki itendeke na wote hawa kufilisiwa kabisa kwa sababu ni pesa zetu na watoto wetu. Tunataka kuona wamefungwa
 
Kimbembe cha bi kilembwe kimeanza..sasa watu wameanza kuathirika na unga wa dengu Giningi itawaka moto muda si mrefu...tukae mkao wa kula na wenye sauti na wasikike
 
Hakuna cha kesi hapa bali ni kupotezeana muda na wakati. Toka lini mwizi akamkamata mwizi mwenzake?. Hii yote ni kuwadanganya watanzania wapumbavu ili kuwapa kura tena mwakani.

Serikali imeoza imejaa wizi, ufisadi, kulindana na ukiritimba.

Dawa ni kutembeza bakora na mapanga mpaka kieleweke, kwani tumetawaliwa na wakoloni weusi.
 
Nilisema hizi kesi, ni kesi si kesi ili mradi kuurudisha umaarufu wa mpenda sifa. Ukipenda sana kusifiwa, utakuwa tayari kufanya lolote ili mradi nyimbo za mapambio ziendelee kurindima.

Niliposema serikali has a very weak case against them in the eyes of law, watu walinisakama sana. Nasubiri kesi ianze nithibitishe maneno yangu.

Hata ile kesi ya BOT, akipatikana mwanasheria makini, atathibitisha we have defective law systeam inayokiuka haki za binaadamu.

Masikini Liyumba na Mzee wetu wa Kanisa, Mzee Kweka, wanawaonea bure!. Time will tell ninachoshukuru, hii kesi itafanya badhi ya bad laws kuwa scraped from the book of laws!.

Aisee Hii hatari..
 
Back
Top Bottom