KUMEKUCHA, Mramba amtaja Mkapa!

Phillemon Mikael,

Niliposoma hoja zako tu nilielewa wazi kwamba wewe ni mdini... Issue inazungumzia Mramba haya maswala ya dini yanatoka wapi.
Imesemekana katajwa Mkapa, Kikwete na Uislaam unatoka wapi kuwakinga Lowassa, na Karamagi ambao ni Wakristu!
Hizi chuki zenu kwa Kikwete kwa sababu ni Muislaam ni utumwa wa kufikiri..Watu kama wewe wanamfuata Yesu kwa sababu ni mtoto wa Mungu, nje ya hapo usingeamini Biblia!..Pole sana.


wewe wasema....!

kuna watu ambao wakishindwa kazi wakiambiwa kweli wanakimbilia mwavuli wa udini...,mtu anaweza kunichukia mimi kama mimi kutokana na utendaji wangu..sio lazima iwe kwa ajili ya dini yangu!!!
 
Hapa Petu,
Mkuu unajua sisi wadanganyika wepesi sana kubadilisha kauli za watu wengine. mathlan Mramba kasema alipata Order toka IKULU, watu tayari wameisha jenga hoja kuwa Ikulu ni pamoja na baraza la Mawaziri wakati msemaji mkuu ni Mramba ambaye pia alikuwa baraza hilo hilo na anafahamu nini IKULU na nini Baraza la Mawaziri.lakini hapa JF limepindishwa pindfdishwa ili Mradi tu ionekanae kuwa maneno haya hakuyasema Mramba ila ni Kikwete na mbinu zake za kumdhalilisha Mkapa..
I Mean nashindwa kabisa kuwaelewa Wadanganyika, ni wao walia kila siku Mkapa afikishwe mahakamani, Kikwete kamstiri lakini ushahidi unapoonyesha kuwa Mkapa anahusika kwa njia moja ama nyingine wanarudi nyuma na kumlaumu Kikwete kuwa ni mbinu zake..
Hata sielewi nazidi kuchoka na Wadanganyika.

Petu hapa Kaka! kanyaga twende! tutafika tu!
 
wewe wasema....!

kuna watu ambao wakishindwa kazi wakiambiwa kweli wanakimbilia mwavuli wa udini...,mtu anaweza kunichukia mimi kama mimi kutokana na utendaji wangu..sio lazima iwe kwa ajili ya dini yangu!!!
Mkuu wala sikuchukii na sintakuchukia hata siku moja ila nakufahamisha upate kuelewa kwamba Ukumbi huu una watu wazima wenye akili zao na wanajua kupima maneno..
Wewe kufikia kuandika yale uloandika wakati issue hapa ni kile alichosema Mramba ktk kesi yake. Wewe umekuja vuta maswala ya Udini na kadhalika inatoka wapi?..Umesukumwa na kitu gani kama sio imani yako wewe ktk dini, tena basi unaamini kile kisichofundishwa na dini yako.
Ebu rudi nyuma uyasome tena maelezo yako mwenyewe kisha nambie yanahusiana vipi na kesi ya Mramba!..
 
Mie nasema hii Kesi na nnyinginezo ndugu wa hizi zitapelekwa kusikilizwa CHEMBA kwa kuficha waandishi wasiripoti tukajua utumbo wa Chama dume.

...Hey naomba bunduki yangu pls
 
Mkuu Phillemon Mikael,

Sehemu kubwa ya maelezo yako umelenga hoja mahususi, lakini sehemu kidogo uliyoteleza, inahamisha mjadala muhimu wa kauli ya Mramba mahakamani akiongozwa na wakili wake.

magazeti yameandika hii habari kuuza ..ukisoma ndani hakuna mahali alipotajwa mkapa bali imetajwa ikulu...ambayo ni taasisi ...inayojumuisha BARAZA LA MAWAZIRI..ambao wanaaapa [kwa namna yeyote kutooa siri za baraza la mawaziri]...na wanasimama kwenye [collective responsibility].........kikwete ,shein ,pinda ...et al walikuwapo kwenye baraza la mawaziri.....ndio maana tunasema hizi kesi ni za kisiasa....hasa zaidi zikichochewa na chuki ya kikwete kwa mkapa......LAKINI KESI ZA NAMNA HII HUISHIA SERKALI KUSHINDWA....KWANI HAZINA MSINGI IMARA!!!....sasa ameshataja baraza la mawaziri..whats next????

Magazeti ni kweli yanaandika kuuza, lakini si yote yanaandika uongo na katika hili magazeti yameandika ukweli. KWa Waziri wa Fedha kusema Ikulu, hawezi kuwa anamaanisha wale walinzi wa mlangoni ama mhudumu wa Ikulu, lazima ana maana ya kuwa ni aliyemteua ndiye anaweza kumpa amri. Uandishi tasfiri unakubalika na ukiondoa hisia zako utaamini hayo.

kama si chuki za kikwete kwa mkapa ..yote yanafanyika kwa baraka zake ....mbona hakuwakamata lowassa,karamagi na ibrahim....ambao ushahidi wao waala si wa kumungunya mungunya?????????

Si ni Kikwete aliyesema "mwacheni mzee wa watu apumzike" ? Si ni Mkapa aliyemwachia JK urais na baadaye Uenyekiti wa CCM? Si ni wasaidizi wengi wa Mkapa wameendelea na JK akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Shein? Sasa hizo chuki hapo hazipo na kama zipo hazina uhusiano wowote na kauli ya Mramba kwa kuwa Mramba na Mkapa wana mahusiano ya kikazi na kifamilia kwa muda mrefu na usije shangaa Mkapa amemwambia Mramba asema hayo ili kuokoka. Mramba ndiye anayesema unayoyasema kwamba kesi zao ni za kisiasa na wanakomolewa na Kikwete, sasa hawezi kutumwa na Kikwete amtaje Mkapa.

si ndio yeye alikuwa watu wake kwa maelekezo yake walikuwa wakisimamia mkapa atukanwe kila siku magazetini?????.....then alipoona kumbe kazi ngumu akliwa songea ...akajibaraguza kwa kusema ..anaomba waandishi wamuache mkapa??

Majibu ya juu yanatosha kukwambia kwamba kwa hoja iliyopo mbele ya Mramba kuitaja Ikulu ya Mkapa, hakuna hoja kwa kuwa Mramba hawezi kutumwa na KIkwete kumtaja Mkapa.

visasi tu!!!... leo hii vinapelekea hadi chama cheti imara kama ccm kinageuzwa cha kidini.....umeona wapi ratio za uongozi chamani zimefikia unrealistic representation of the members or country demographic population kiasi huki??...LEO HII KAMATI KUU ASILIMIA 80% SITAFUNI MANENO ...NI WAISLAMU ...WHAT IS THIS MOCKERY???

SAFU ZA VIONGOZI ASILIMIA ZAIDI YA 80%....TAZAMA HADI KWENYE JUMUIA .....ZA CHAMA ........SIJAANGALIA VEMA HALMASHAURI KUU PALE...LAKINI HII HAITUPELEKI PAZURI KAMA TAIFA????...LAZIMA UONGOZI UWEKE RATIO ZETU SAWA UWAKILISHI KIDINI ,KABILA .....HATUNA KAWAIDA YA KUUONGEA WAZI...LAKINI SI WA KUUDHARAU...!....AU MNATAKA TUKIKIE KAMA KWENYA KUANZA KUDAI NAFASI ZA UTEUZI WAZI KIDINI,KIKANDA AU KIKABILA..KIJINSIA??

Hapa ndipo unapopotoka zaidi na unaungana na wale walioandika barua ya wasomaji katika gazeti la Mtanzania wakisema kwamba Umoja wa Wanawake umejaa Waislamu, na Sophia Simba ameteua Waislamu wenzake kasoro Mkiristo mmoja tu, Lucy Mayenga. Kwa mfano mdogo huo wa Wanawake, kwanza Sophia Simba si Muislamu na Lucy Mayenga si Mkiristo. Na hiyo tu inaondoa hoja ya udini kwa kuwa kwanza majina Si dini. Tuna Augustine Ramadhani, Askofu John Ramadhani ambao ni Wakiristu safi, tunao kina Gideon ambao ni Waislamu safi na kadhalika.

Lakini kama unazungumzia Kamati Kuu, rudi katika Kamati Kuu iliyopita na uangalie majina. Angalia wakati wa Mkapa na wakati wa MWinyi then urudi ujenga hoja upya. Uende na Zanzibar ujenga hoja pia.

MAANA KENYA NDIO WAMEFIKA HAPO...HAWAMPI RAIS FURSA KUTEUA KIUTASHI ..AKIJIUZULU KIONGOZI ..KAMA ALITOKA NYANZA ...KESHO YAKE WAZEE WA NYANZA WANAENDA IKULU NA MAJINA YA VIJANA WANAOWATAKA MMOJA WAO NA KUMPA RAIS ....NA INABIDI ATEKELEZE..! WAMEFIKA HAPO BAADA YA WANASIASA KU ABUSE ...FURSA YAO YA KUPANGA SAFU ZA UONGOZI KWA USAWA!![/B]

[/QUOTE]

Hoja za juu zimepunguza nguvu ya hoja yako hapo juu.
 
Phillemon Mikael;

Tukirudi kwenye kauli yako kuhusiana na kesi ya Kina Mramba. Nakubaliana na wewe kesi hizo hazina maana yoyote na wengi humu wamejadili hilo katika mada nyingine kwamba wangepelekwa mahakamani kina KAgoda, MEremeta, Tangold, Rada tungeelewa kwamba hizi ni kesi makini, lakini huwezi kuwashitaki kina Mramba kwa matumizi mabaya ya madaraka ukawaacha kina Lowassa na Karamagi (Richmond) na huwezi kuwashitaki kina Jeetu Patel na Maranda ukawaacha kina Rostam Aziz na Manji (Kagoda), huwezi kuwaacha Masha na kina Rutabanzibwa na Chenge (Deep Green/rada). Tunaambiwa Jeetu Patel ni mshirika wa karibu wa Mkapa, na Maranda anahusiana na mwanasiasa mwingine wa zamani wa wakati wa Mkapa pia, lakini Kagoda, Deep Green na Richmond haigusiki.
 
Rais wa awamu ya tatu B.W.Mkapa atajwa kuhusika na kwenye tuhuma zinazomhusu Mramba na Yona,Nipashe ya agosti 4,2009.
 
Ametajwa kwamba amefanya nini? Usiweke habari iliyokaa mithili ya hadith, hadith...
 
Mtandao unasumbua kuposti habari hiyo,ila imeelezewa kuwa Mkapa aliuidhinisha ule msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stuwart iliyosababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja (11 bilion).
 
of course; kama vile Kikwete alivyoidhinisha mkataba wa Richmond na Dowans! Nadhani wakati umefika kwa DPP kuifuta hii kesi and the illusion of justice has already been achieved..
 
Kwani Ikulu ni Rais? Mbona wazito wengi tu wana ofisi zao pale. Kama aliagizwa na Rais si angesema tu?

Amandla.....
 
Kwani Ikulu ni Rais? Mbona wazito wengi tu wana ofisi zao pale. Kama aliagizwa na Rais si angesema tu?

Amandla.....

wakisema Ikulu imesema ina maana authority ya Rais ndiyo imefanya hivyo; Unaweza kumtenganisha Rais na Ikulu yake? Yaani kama US President na White House? Nilidhania ofisi zote zilizoko Ikulu ziko chini ya Rais ama?
 
Halisi na ungana na wewe, hizo kesi tumezoea hakuna jipya. Waandishi wa hizi habari wako walio na uchungu na naandikwa kwa kufuata maadili na wako wenye njaa. Wako waandishi safi ama wamepoteza kazi au kutishiwa maisha na watuhumiwa. Mtu kama Rostam Azizi ana share kwenye magazeti so what do you expect, ni sawa na jambazi kuown kituo cha polisi.
 
Hawa wote ni wasanii tu!! Mwisho ya yote hawa wote wakina Mramba, Yona , Mgonja na mafisadi wengine wataachiliwa. Serikali hii ingekuwa serious isingemuachia Mgonja mpaka astaafu ndio imfungulie mashtaka; kwa kufanya hivyo walihakikisha kuwa ingawa ni fisadi lakini sisi walipakodi tutaendelea kumlipa pension yake!! Kama alivyosema Lowassa mbele ya bunge wakati anajitetea juu ya Richmond " SISI WOTE NI WANASIASA TUKIANZA KUUMBUANA HAKUNA ATAKAYEBAKI". Ni kwa misingi hiyo Kikwete atamlinda Mkapa na atakayekuja atalinda uoza wa Kikwete !! Wapambe wao nao watalindwa hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom