Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 666
Muonekano wako ndo kila kitu. Ndio unaamua watu wengine tukuchukuliaje. Ndio unaamua watu wakuheshimu haraka au la. Muonekano wa nje upo juu yako kabisa. Unaweza kuubadili muda wowote na ukaufanyia kazi. Wala usisingizie kitu. Unaweza kujiweka utakavyo. Hivyo usipuuze hilo ukabaki kujisemea 'sina mvuto'. Hapana. Jitahidi upendeze na ujiweke msafi. Usipuuze muonekano wako kamwe.
Usipendeze ili umpate mwanamke fulani. Au ili fulani akuone. Hapana. Bali kwa ajili ya furaha yako mwenyewe.
Japo ni sawa kujiweka vizuri ili wengine wakuone (sote tunataka kuonwa) lakini sio ndo iwe kipaumbele chako sana, mpaka ukajibadilisha na kuwa usivyotaka.
Pia mwonekano wako unaamua utakaye mvutia. Sio wanaume wala wanawake. Wote. Ukiwa na mwonekano wa kitapeli. Utavutia matapeli na wanaotapeliwa. Ukiwa na mwonekano wa kiofisi. Utavutia mabosi na wafanyakazi aina hiyo.
Hata kama ni kwa sehemu ndogo usipuuze. Usije ukasema 'ah naenda hapo tu, haina haja'. Ujue umepunguza maksi zako mbele ya macho ya watu. Pendeza na Ufurahie Siku yako.
Siku Njema.