Kumbe St. Augustine University of Tanzania (SAUT) ni moto wa kuotea mbali

hii mada ya vyuo ilishafungwa hapa jamvini, tanzania kuna vyuo viwili tu. UDSM NA SUA: vilivyobakia ni longolongo tu, hamna kitu ndo maana unasifu wanasiasa kazi ambayo inaweza kufanywa vizuri sana hata na muhitimu wa darasa la saba. Unapaswa kufahamu kuwa kazi ya siasa haina ubora kama kazi ya ualimu katika rank za great thinkers. Ualimu ni professional na siasa ni usanii tu.
vingine nn?
 
sasa hyo robo 3 ya product za UDSM na SUA inayoongoza serikali na mashirika ya uma imeifanyia nini nchi zaidi ya kufanya ufisadi na kuifilisi nchi?
 
Senetor;nyie mngekua wastaarabu mngeleta mada mfu ka hii hapa jf??,yan m2 kuwa mwanasiasa 2 tayar ushaona chuo alchosoma kiko nondo,ndugu yangu siasa ni uwezo wako wa kuongea facts 2 zkakubalika kwa wa2 na c kuwa nondo kichwan,mbona ce wa udsm na sua 2cjcfie kwa kutoa wabunge na watendaji weng wa serikal na mashirika,au hujui kuwa zaidi ya robo tatu ya watendaj wa hii nchi ni products za udsm na sua,?ebu shkeni adabu na vyuo vyenu hvo vya uchochoro.ebooh

Senetor, mie kuchangia mada na kukukosoa haina maana mie nimesoma SAUT na hivyo vyuo unavyosema vya uchochoroni. Mtu yeyote anayetoa mada ya kulinganisha chuo alichosoma na vingine namuona kama ana utoto na ufinyu wa fikra. Ungejuwa nimesoma vyuo gani na niko wapi wala usingetoa comment kama hiyo hapo juu. Si vema kuvibeza hivyo vyuo vichanga na kuviona kuwa havitowi watu walio na mchango katika jamii, na haina maana wewe ni bora zaidi ya hao wanao soma hivyo vyuo unavyovibeza.
 
udsm zamani cio leo mdingi badirika wewe usiishi kwa historia, bora ata Sua hadi leo,angalia idadi ya maprofesa wa vyuo vya private.
 
udsm zamani cio leo mdingi badirika wewe usiishi kwa historia, bora ata Sua hadi leo,angalia idadi ya maprofesa wa vyuo vya private.
maprofesa gani wako vyuo vya private mkuu?
 
sasa mkuu hata hii udsm ya leo unataka kuifananisha na chuo cha kipuuzi kama saut?
Kama kweli saut ni chuo cha kipuuzi kwanini why did Higher education board commission it? i bet huwezi kumlinganisha graduate wa saut na udsm. ni kama ardhi na mbingu mkuu. saut iko juu-kubali yaishe babu
 
Senetor
;sasa mkuu hata hii udsm ya leo unataka kuifananisha na chuo cha kipuuzi kama saut?

Senetor, kama umesoma hujastarabika. Kwako wewe Saut ni chuo cha Kipuuzi? Kama umesoma UDSM, na chenyewe hakikuwa hivyo kilipo katika umri wa SAUT. Kwa hiyo wewe unajiona ni bora zaidi ya wale waliosoma vyuo vingine tofauti na UDSM? Jiangalie maisha yako, na utendaji kazi wako, je ni bora zaidi ya hao waliyosoma vyuo vingine? Acha kubeza SAUT ndugu, sema ni chuo kidogo bado kinakuwa.

mwambie mkuu. ubora wa chuo sio majumba but the products
 
zilizofanywa na hao wanaoandika proposal kila siku kuomba pesa toka nje zimetufikisha wapi or zimetusaidia nini kuondokana na umasikini/matatizo yetu? what???
Research ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote hapa duniani,suala la implentation ya research findings ni muhimu pia lakini pande hii ufanywa na mtu au kikundi kingine cha watu,hivyo kama chuo kikuu kimefanya research nyingi na hazikufanyiwa kazi basi hilo si kosa la chuo kikuu bali ni kosa la sehemu iliyotakiwa kutumia hizo findings kutatua matatizo mbalimbali.Swali la msingi bado lipo palepale wamefanya research ngapi?jibu swali acha polojo!na kama wewe ni product ya chuo hicho basi wewe ni by-product kwa kuwa huendani na hadhi ya chuo hicho,huwezi kujibu maswali ya msingi,uliwezaje kumaliza chuo?
 
Vyuo vikuu vya umma vina changamoto kubwa manake walimu wazuri wengi wanakimbilia vyuo binafsi, lakini hili linasababishwa na serikali kutokuwajali watumishi wake..

si kweli, hapo nakupinga mpaka asubuhi...walimu wanaokimbilia private sector ni wa sekondari na ngaz nyingine na sio vyuo vikuu, infact hata walio private universities wanataka waje public universities.
 
Kama kweli saut ni chuo cha kipuuzi kwanini why did Higher education board commission it? i bet huwezi kumlinganisha graduate wa saut na udsm. ni kama ardhi na mbingu mkuu. saut iko juu-kubali yaishe babu
Kichekesho!unajidanganya mkuu!!!angalia rank ya vyuo vikuu vya Afrika utapata ukweli!!au kama una vigezo vingine zaidi ya hivyo vilivyotumike tafadhali tupatie ili nasi tuweze kuelimika zaidi!!
 
Siku za nyuma nilidhani chuo kikuu cha mtakatifu Augustine (SAUT) kilichopo mkoani Mwanza hakina uwezo wa kuzalisha vijana na wasomi wenye kuweza kulisaidia taifa katika kusukuma gurudumu la maendeleo, Nilidhani ni vyuo vikuu vya umma kama vile UDSM ndio vinaweza kudhalisha viongozi bora wa taifa hili lakini sasa hivi nimeamini kuwa SAUT nacho ni moto wa kuotea mbali katika kuandaa viongozi pengine na watumishi watakao sukuma gurudumu la maendeleo mbele. Mpaka sasa chuo cha mtakatifu Augustine (SAUT) kimezalisha wabunge watatu machachali walioingia bungeni kupitia vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita. Wabunge hao ni Ezekiah Wenje, Moses Machali, na Felix Mkosamali. Mbali na hao mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Heche pia ni mhitima wa SAUT. jana nilisikiliza michango ya Moses Machali na Wenje katika kujadili bajeti ya waziri mkuu kwa kweli nilivutiwa na jinsi vijana wale walivyokuwa wamejipanga wakati wakitoa hoja zao. Wabunge hao walitoa michango yao huku ikiambatana na nukuu "quotations" kutoka kwa wasomi mbalimbali. Hatua hii imenifanya sasa niamini kuwa kumbe SAUT ni moja ya vyuo makini vionavyozalisha viongozi na wataalamu makini katika taifa hili.
Hata Vicky Kmata ni product ya SAUT
 
Nimegundua kwamba UDOM ni maarufu na iko juu kwa sasa ndio maana hamchoki kuizungumzia.
Tofautisha umaarufu na ubora!mbona shule za kata ni maarufu sana kuliko shule nyingine?lakini vipi ubora wa elimu!!
 
udsm zamani cio leo mdingi badirika wewe usiishi kwa historia, bora ata Sua hadi leo,angalia idadi ya maprofesa wa vyuo vya private.
Tofauti ya Udsm ya zamani na ya leo ni nini?Tutumie njia gani kupambanua ubora wa chuo?mimi najaribu kutoa chache na wewe utatoa zako:
*Idadi ya walimu wanaokidhi vigezo(PHD holders from reputed or recognised universities)
*Alama za masomo kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma(Mfano unaweza kukuta chuo kimoja kinachukua cream zote na kingine kikaambulia mabaki,sote tunafahamu hapa tanzania kuna special schools kama vile Tabora boys,Iriboru,Mzumbe,Msalato na kadharika,huwezi kulinganisha na shule nyingine hasa kwa sifa za kufauli ambazo wanafunzi uingia nazo).
*Maktaba na vitabu vinavyoendana na wakati
*Uzoefu wa walimu wake katika kufundisha na kufanya tafiti.

Malizia na nyingine mkuu!!!!
 
Napita tuu, nina safari zangu
 
Back
Top Bottom