Kumbe ndio maana wanashikilia bango posho!!! Lo aibu!!!

dguyana

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
423
110
Polisi wakwama kumfikisha Shelukindo mahakamani
Send to a friend
Thursday, 08 March 2012 20:12
0diggsdigg

Elias Msuya na Joseph Zablon
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, juzi ililazimika kuahirisha kesi ya madai ya Dola za Marekani 20,333 (sawa na Sh 32,329,470) inayomkabili Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo kutokana na polisi kushindwa kumkamata na kumfikisha mahakamani hapo. Kesi hiyo namba 92 ya mwaka 2005, ilifunguliwa na Benki ya Azania inayodai kumkopesha mbunge huyo, Dola za Marekani 12,932 (Sh20 milioni) ambazo sasa pamoja na riba ya asilimia 14, zimefikia Dola za Marekani 20,333.

Juzi kesi hiyo ilifika mahakamani hapo ili kukazia hukumu iliyokwishatolewa kwa kumtaka Shelukindo, alipe deni hilo na Shellukindo alitakiwa kuletwa na polisi baada ya mahakama kuandika hati ya kukamatwa kutokana na kuhudhuria kesi hiyo. Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Joyce Minde alitoa hati ya kukamatwa kwa Shelukindo tangu Februari 22 mwaka huu ili aje kusikiliza kesi hiyo juzi, lakini Kituo cha Polisi Oysterbay kilichopewa hati hiyo, kilishindwa kumleta mahakamani, hivyo akalazimika kuahirisha kesi hiyo hadi mbunge huyo atakapokamatwa.

"Awali niliamuru akamatwe lakini hilo halikufanyika na juzi (jana) hakutokea mahakamani hivyo nimekazia amri yangu ya awali," alisema Minde na kuongeza kuwa shauri hilo limepangwa tena Aprili 10 mwaka huu. Mbunge huyo alikuwa akikabiliwa na kesi ya madai namba 92 ya mwaka 2005 na hukumu ilitolewa ya kumtaka alipe, lakini hadi sasa hajafanya hivyo na juzi ambapo alitakiwa kufika mahakamani, hakutokea, badala yake alifika wakili wake.

Minde alisema, amekazia hukumu yake ya awali ya kukamatwa Shelukindo ambaye anatakiwa kufikishwa mahakamani Aprili 10 mwaka huu. Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, SSP Wilbrod Mutafungwa alikiri kupokea hati ya kumkamata Shelukindo, ila akasema kuwa bado wanamtafuta.

"Ni kweli tunayo hati ya kumkamata, lakini bado tunamtafuta," alisema SSP Mutafungwa. Upande wa madai, yaani Benki ya Azania unaowakilishwa na wakili Charles Mugila ulikuwepo mahakamani wakati wa kusikiliza kesi hiyo, lakini hadi wakati wa kuingia kwenye chumba cha Mahakama, majira ya saa tano asubuhi, Shelukindo hakuwepo.

"Mara ya mwisho mahakama ilishatoa hati ya kumkamata Shelukindo, lakini nashangaa kwanini polisi hawamkamati?" Alihoji Wakili Mugila. Kwa mujibu wa hakimu Minde, "Tunachokifanya sasa ni kukazia hukumu, kwasababu hukumu ilishatoka tangu mwaka 2006. "Kama Shelukindo atafika mahakamani, nitamsikiliza kwanini ameshindwa kulipa deni hilo.

Kama hana sababu za msingi atafungwa jela kama mfungwa wa madai," alisema Minde. Kwa siku za hivi karibuni, Shelukindo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, amekuwa katika harakati za kushiriki mikutano ya Mpango wa Kujitathmini kiutawala Bora wa Afrika (APRM) ambao wajumbe wake wapo nchini kufanya tathmini ya mpango huo


Source Mwananchi.
MY Take:- Hili lilishawahi kusemwa hapa JF watu wakadhani uzushi kweli ubunge dili.
 
Back
Top Bottom