Kumbe nacheza uwanja mmoja na baba

kaa kimya wewe acha tu Mungu atamuumbua kwa wakati wake atakaoutaka yeye
 
Yupo beki tatu aliangamiza familia nzima, na walikuja jua source in beki tatu, wakati wakiugua.

Na hao 'Bar-Maids" wa mzee huko nje mama atajikinga nao vipi!?
Bwana mdogo ashauriwe ajiweke pembeni. ..ukimwambia mama yako akikasirika ataachia ngazi na beki tatu ndiyo atakamata usukani na wewe ndiyo utajua kuwa maharage ni mboga au kiungo cha kande!?
 
Usije ukamueleza mama yako,mchane beki3 na utafute muda uongee na mzee umwambie anachofanya sicho. Pia jitahidi kujishuhulisha ushakua kijana saivi unapaswa kujishuhulisha nawe uwe na vyako,mahusiano na huyo dada acha
 
Wasalam wakuu,

Ni wiki ya tatu sasa tangu mama asafiri kwenda kwenye msiba huko nyumbani kwao, nyumbani tumebaki mimi, baba na mfanyakazi wetu wa ndani.

Kwa vile mimi nimeshamaliza chuo na muda mwingi huwa nashinda nyumbani (sina kazi) nimejikuta nikiingia katika mahusiano ya mapenzi na huyu msichana waa kazi.

Juzi usiku kama kawaidayangu nilienda chumbani kwake ila sikumkuta ikabidi nitege mingo ili nijue huyu msichana kaenda wapi, baada ya kama lisaa 1 nilishtuka kuona mlango wa kwa baba unafunguliwa na yule msichana wa kazi kakatoka na kwenda chumbani kwake.

Niliumia sana kuona kile kitendo si kwa wivu wa mapenzi bali kwa kile kitendo alichofanya baba na ukizingatia anamke wa ndoa (mama yangu).

Wadau naombeni busara zenu kuwa anachokifanya sio kizuri au nimwambie na bi mkubwa?

ndiyo maana ukishafikisha miaka 18 hupaswi kabisa kukaa nyumbani kwenu, hata kama pako poa kiasi gani unapaswa uondoke uende kupanga tofauti na nyumbani,
hivyo ndivyo tunavyofanya watoto wa kiume,
ukishakua unasepa, siyo mnabanana home masaa yote.
we unadhani ungekua umepanga haya yangetokea????????????????

Umeona sasa, jambo moja mwambie Mother au Mdingi akupe Punga ufanye Business akikupa unakwenda kupanga, halafu unaanza Moja.

Mtoto wa kiume sifa kubwa ni kutokuwa Muogopa kwa lolote lile.
Ondoka nyumbani hapo, ukiendelea utaleta balaa,
we subiri house girl apate mimba ndiyo utajua nasema nini.
 
Wasalam wakuu,

Ni wiki ya tatu sasa tangu mama asafiri kwenda kwenye msiba huko nyumbani kwao, nyumbani tumebaki mimi, baba na mfanyakazi wetu wa ndani.

Kwa vile mimi nimeshamaliza chuo na muda mwingi huwa nashinda nyumbani (sina kazi) nimejikuta nikiingia katika mahusiano ya mapenzi na huyu msichana waa kazi.

Juzi usiku kama kawaidayangu nilienda chumbani kwake ila sikumkuta ikabidi nitege mingo ili nijue huyu msichana kaenda wapi, baada ya kama lisaa 1 nilishtuka kuona mlango wa kwa baba unafunguliwa na yule msichana wa kazi kakatoka na kwenda chumbani kwake.

Niliumia sana kuona kile kitendo si kwa wivu wa mapenzi bali kwa kile kitendo alichofanya baba na ukizingatia anamke wa ndoa (mama yangu).

Wadau naombeni busara zenu kuwa anachokifanya sio kizuri au nimwambie na bi mkubwa?
Kwani umejuaje katoka kuchakachuliwa? Na Mzee ndani? Labda alikuwa anapanga vitu chumbani huko
 
Kwani wewe pamoja elimu yako ya chuo unadhani wewe ndio mwenye haki ya kufanya mapenzi na beki3 enu eeeeh. Tamaa zenyu hizi zitakuja kuwaua bule. Kumbuka ni laana kula sahani moja na dingi ako. Kwa kuwa sasa umejua basi wewe jitoe kimyakimya kisha mbio kacheki ngwengwe mapema kama ulienda mwinyi mpeku ili ujue status za HIV.
 
Aisee!
Nyamaza kimya kabisa funga hilo bakuli!
Familia ndo hiyo hiyo na umeikuta usije jifanya mjuaji.
 
Jichanganye mtaani fanya kazi yyt ya halali pasipo kubagua utapata njia ya kutokea, utapanga chumba chako then utajitegemea, kaushia hiyo ossue ikimfikia mama itakusumbua maisha yako yoote yaliyobaki
 
Back
Top Bottom