Kumbe nacheza uwanja mmoja na baba

Pamoja mkuu nitajaribu kumuanzishia figisu figisu huyu beki 3 Ili atimuliwe tu.

Beki tatu kakosa nini?
Wewe na baba yako tamaa zenu ndiyo chanzo cha kumsababishia matatizo house girl!
Dogo endelea na maisha yako! Mwache mzee aendelea kutoa mastress zake ,unaweza kuta mama yako ndiyo chanzo mshua kikimbilia kwa Beki Tatu.

Usimharibe mtoto wa watu maisha-ila kwa ustaarabu muonye awe makini na tabia ya kuwachangaya mtu na baba yake akome!


Vipi Mama naye anakula misele wapi?
 
Ukionja asali na mzinga unachonga. Usikute huyo baba ana michepuko kibao huko nje.
 
Acha kula chakula cha baba yako!!!wewe umedandia treni mwache mzee atafune hiyo kitu,hata wewe utatafuna muda wako ukifika.
 
Kijana si vizuri kutembea na Mama yako mdogo chakufanya tupatie number yake huyo baki tatu tukusaidie kulipiza kisasi.
 
Hapa mi naona hakuna ambaye hana kosa. Wote mnazini. Wote. Sio baba sio wewe sio house girl. Kwahivyo huwezi kujustify nani awe na house girl au nani alianza.

Ila house girl ndo kabisa hajielewi. Kwa sababu anajua anatembea na wote wawili lakini anakubali.

Sijui uhusiano wako na mzee/baba ukoje? anaingilika? unaweza kuongea naye? huwa mnapiga story? usikute ni wale wazee hawaongei na watoto wao. Kama anaingilika na nyie ni marafiki unaweza kumwambia mzee kijanja kwa maneno yako kutokana na jinsi anavyoingilika. Labda "mzee naona tumbo la dada ni kubwa, sijui mjamzito. Asije akawa mjamzito na mimi sijapata kazi." Hapo ujumbe utakuwa umefika.

Ila Kikubwa msichana wa kazi ni wa kumwondoa tu. Yaani hapo mwondoeeni tu kwa uzuri wa familia. Kwa sababu mwisho wa siku mzee au wewe mtampa mimba. Sasa huyo mtoto sijui utamwita nani? Halafu sasa hivi!! kiburi kitaanza. Ishara kubwa sana ya baba analala na msichana wa kazi huwa ni dharau na kiburi kwa mama.
 
Ninachokushauri dingi hajafanya kitendo kizuri kabisa.kutembea na beki 3 Nyumba hiyo hiyo na mkewe akiishi hapo.
Je unategemea cku hiyo ingelikuwa ni mama ndo kamwona anatoka kwa dingi lazima mmoja angekufa cku hiyo.
Hako kamchezo dingi yako hatakaacha amekolea kwa huyo beki 3.
Nakushauri wewe ni mtoto WA kiume hii kitu iwe siri yako mama asiijue.ila kaa na mshua mwambie alichofanya, mshua akifahamu kuwa umewagundua atamrudisha beki 3 kwao lakini pia hata akija baki 3 mwingine dingi anaweza akawa nawoga WA kumlamba asije akagundulika kwamba karudia kosa
 
Ila house girl ndo kabisa hajielewi. Kwa sababu anajua anatembea na wote wawili lakini anakubali
Sisemi kwamba house girls hawana haki ya kupenda au kupendwa. Ila ukweli mchungu ni kwamba wadada wa kazi wengi wanajikuta kwenye mahusiano na watoto wa kiume na mababa wenye nyumba sio kwa kupenda, wengi hawapendi ila wanajikuta tu wanakubali ili kulinda "vibarua vyao". Mdada hajiwezi, na anawaza je nikikataa nikafukuzwa, ntafanyaje na haya maisha.

Afu hawa wadada wa kazi ni kama watoto wa familia husika, mkatongozage huko nje jamani. Familia nyingine ptuuu, ndo madomo zege au kuonea tu mabinti za watu? Huwa mnakuwaga na nia za kuwaoa kweli, au kusuuza tu mirungu yenu. Hawa hata wakisema huyu mdada afukuzwe, akija mdada mwingine watamtongoza tu kama kawaida yao. Solution ni wao wenyewe kuanza kujiheshimu na kuwaheshimu hao madada. Muwe na aibu, muwe na Utu
 
Mweleze baba yako kuwa anachokifanya sio kizuri na akiendelea mtishie kumwambia mama yako
 
Mfanyie zengwe beki tatu atimuliwe...

Mnaweza weka houseboy..kama na huyo msure wako akimMendea basi kunatatizo hapo:D:D:D

fursa kwa mama ............. hii ndio inauma zaidi, jamaa atajinyonga ,bora hivyo hivyo tu.
 
ndiyo maana ukishafikisha miaka 18 hupaswi kabisa kukaa nyumbani kwenu, hata kama pako poa kiasi gani unapaswa uondoke uende kupanga tofauti na nyumbani,
hivyo ndivyo tunavyofanya watoto wa kiume,
ukishakua unasepa, siyo mnabanana home masaa yote.
we unadhani ungekua umepanga haya yangetokea????????????????

Umeona sasa, jambo moja mwambie Mother au Mdingi akupe Punga ufanye Business akikupa unakwenda kupanga, halafu unaanza Moja.

Mtoto wa kiume sifa kubwa ni kutokuwa Muogopa kwa lolote lile.
Ondoka nyumbani hapo, ukiendelea utaleta balaa,
we subiri house girl apate mimba ndiyo utajua nasema nini.


Poa mkuu Ila si unajuatena nimemaliza Chuo na Kama miezi 5 hata channel bado hazija set frsh, Ila kujikataa maskani nitajikataa tu b'se hata Mimi napenda niwe huru zaid.
 
Kwani wewe pamoja elimu yako ya chuo unadhani wewe ndio mwenye haki ya kufanya mapenzi na beki3 enu eeeeh. Tamaa zenyu hizi zitakuja kuwaua bule. Kumbuka ni laana kula sahani moja na dingi ako. Kwa kuwa sasa umejua basi wewe jitoe kimyakimya kisha mbio kacheki ngwengwe mapema kama ulienda mwinyi mpeku ili ujue status za HIV.


Ila kinga nilikua natumia kiongozi, maana nilikua nahofia Sana HIV na Mimba pia.
 
Back
Top Bottom