Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,707
- 41,460
Jamani mnapoteza kujadili kitu kilicho wazi. Makamu wa kwanza na wa pili wa Rais wa Zanzibar, kwa hapa bara si chochote, ni raia wa kawaida wa kutoka Zanzibar. Katiba ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, haina kabisa vyeo hivyo. Katiba ya JMT inamtambua Rais wa Zanzibar na Waziri kiongozi wa Zanzibar kama viongozi wa juu wa sehemu mojawapo ya Mwungano. Kwenye serikali ya JMT Rais wa Zanzibar hadhi yake ni kama ya waziri - yeye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la JMT.
Hao Makamu mnaowataja kamwe hawatambulika na hawatatambulika kwenye serikali ya JMT mpaka katiba ya JMT itakapotamka hivyo. Ukweli kikatiba kumfananisha Maalim Seif na Mkuu wa Wilaya kwa JMT ni kumkweza. Kikatiba, kwa JMT yeye ni Raia wa kawaida kama tulivyo sisi wengine, anachofanyiwa ni mchezo wa kuigiza wa kumsadikisha kuwa naye ni kiongozi anayetambulika katika JMT wakati siyo kweli. Serikali ya JMT na CCM wanalijua sana hilo ila sina uhakika kama Maalim Seif na CUF wanautambua ukweli huu.