Kumbe kuna salamu maalumu ukikutana na mtu usiku mzito? Usiku wa leo mbio ndiyo zimeniokoa

Hao ni either wahuni ,sungusungu au Walinzi wa eneo hilo, wamejiwekea password yao. Ili kuto hitarifiana wao kwa wao na watu wa kitaaa kwao.
Bro ukakosea Password . Ila umekuwa mwepesi kujiongeza, ndo maana unaambiwa don't be Fat daddy
hitarifiana ❌ hitilafiana✔️
 
Iliwahi kutokea mwaka jana, kuna dada alishushwa na boda kama saa saba usiku, ghafla sungu sungu wakafika na kumwambia "usikuuuu" dada kimyaaa! Ghafla akajikuta chini ya ulinzi na ikabidi apekuliwe kwenye mkoba wake kama ana silaha au chochote kibaya, humo wakakuta Ky, vipodozi na vyupi vya akiba.

Alipoulizwa unakwenda wapi alisema ni kwa mpenzi wake na ni nyumba ya tatu kutoka hapo, jamaa akafuatwa na kuamshwa akakiri huyo ni mgeni wake na ni amani kabisa, dada akaonywa kutembea usiku na kuachiwa.

Pia hii ilichangiwa na sungu sungu mmoja alimfahamu huyo dada kuwa hana tatizo lolote na ana mume wake ambae yupo kikazi Dodoma, ila dada hakumjua huyo sungu sungu.
 
Umeamua kuwatisha wanaume walio kikazi Dodoma 🤣🤣 anyway....USIKU..
 
Kuna knowledge ndogo sana ila ni za muhimu sana,
Usiku wa leo Mida ya saa nane hivi nilikua napita kwenye chocho fulani hivi, Ilikua ni njia ndefu iliyonyooka, upande wa Juu/ kulia ni ukuta mrefuu, chini/ kushoto ni mto wenye vichaka chaka.

Kuanzia mwanzo wa ukuta mpaka mwisho ni kama 500M hivi maana ni karakana ya reli kwa ndani.

Kwa mbele kuna mtu anakuja, ni giza kali naona weupe wa shati kidogo na ile mikwaruzo ya kiatu. Wala sikuwaza chochote..

Nikasikia Sauti Kubwa "USIKU" mimi sikuelewa anamanisha nini, akasema tena "USIKU" nikiwa sina uhakika anaongea na mimi, Maana walikua wawili.
Nikajibu kwa Sauti "USIKUU"

Khaaaa, ghafa nasikia Mvurugano ya Vichaka, "kwacha kwacha kwachaaa" na mtu kama kaingia kwenye Maji, ghafa sione ule weupe wa shati, Nikiwa sielewi nini kinaendelea, kulipita upepo unafanya kuvuma sikioni kwangu, kumbe ni jiwe, nilishtuka baada ya kutua ukutani.

Hapo ndio nikajua hapa hakuna usalama, nikazima simu fasta tusionane, mbele nilikokua naelekea ndio pafupi, nyuma parefu mno.

Nikatoka kwenye kale ka njia, nikajibana upande wa chini wenye kichaka, nasikia tu mtu anatembe kwenye maji, Mara nikasikia Washa tochi.

Aaaaaaaah, hapo ndio walipoharibu, kule nyuma nilikokua naona ni mbali sijui nilifikaje, ninachokumbuka tuu kuna washakaji wawili walikua nyuma yangu, mmoja alivyoona nimempita kwa speed naye nyuma akaunga kunifuata, wa pili hakusubiri nimpite kaona/sikia mtu anakuja kwa kasi akageuza.

Kituo changu ilikua ni huku karibu na Tazara ushapita Mchicha, maana ilibidi nirudi nyuma huku, wale washkaji sijui waliishia wapi, ila ni kama walikunja kushoto kama wanaelekea njia ya vingunguti, Anyeifahamu kiwalani vizuri ashafahamu chocho ninayoizungumzia.

Kufika home naelezea naambiwa, Nilitakiwa niseme "MCHANA" , ndio nikashangaa? How comes?

Anyway mimi niliyokua najua ni mtu akikuambia "SALAMA?" unajibu "SALAMA"

Tupeane tips kama kuna ishara au salamu nyingine za siku, haya maisha ya kuishi kwa mbio, sio siku zote utashinda.
Watoto wa 2000 mtajulia wapi haya🤣🤣🤣
 
Hahah hapana mkuu, ila yule Sungu sungu anaemjua ndiye aliyetupa ushuhuda huku akilalamika na roho ikimuuma kama kafanyiwa yeye
Aumie yanamuhusu, anajua huko Dodoma hiyo mbaba analalaga wapi? Mwambie sungu sungu aendelee na doria ahakikishe usalama upo.
 
Kuna knowledge ndogo sana ila ni za muhimu sana,
Usiku wa leo Mida ya saa nane hivi nilikua napita kwenye chocho fulani hivi, Ilikua ni njia ndefu iliyonyooka, upande wa Juu/ kulia ni ukuta mrefuu, chini/ kushoto ni mto wenye vichaka chaka.

Kuanzia mwanzo wa ukuta mpaka mwisho ni kama 500M hivi maana ni karakana ya reli kwa ndani.

Kwa mbele kuna mtu anakuja, ni giza kali naona weupe wa shati kidogo na ile mikwaruzo ya kiatu. Wala sikuwaza chochote..

Nikasikia Sauti Kubwa "USIKU" mimi sikuelewa anamanisha nini, akasema tena "USIKU" nikiwa sina uhakika anaongea na mimi, Maana walikua wawili.
Nikajibu kwa Sauti "USIKUU"

Khaaaa, ghafa nasikia Mvurugano ya Vichaka, "kwacha kwacha kwachaaa" na mtu kama kaingia kwenye Maji, ghafa sione ule weupe wa shati, Nikiwa sielewi nini kinaendelea, kulipita upepo unafanya kuvuma sikioni kwangu, kumbe ni jiwe, nilishtuka baada ya kutua ukutani.

Hapo ndio nikajua hapa hakuna usalama, nikazima simu fasta tusionane, mbele nilikokua naelekea ndio pafupi, nyuma parefu mno.

Nikatoka kwenye kale ka njia, nikajibana upande wa chini wenye kichaka, nasikia tu mtu anatembe kwenye maji, Mara nikasikia Washa tochi.

Aaaaaaaah, hapo ndio walipoharibu, kule nyuma nilikokua naona ni mbali sijui nilifikaje, ninachokumbuka tuu kuna washakaji wawili walikua nyuma yangu, mmoja alivyoona nimempita kwa speed naye nyuma akaunga kunifuata, wa pili hakusubiri nimpite kaona/sikia mtu anakuja kwa kasi akageuza.

Kituo changu ilikua ni huku karibu na Tazara ushapita Mchicha, maana ilibidi nirudi nyuma huku, wale washkaji sijui waliishia wapi, ila ni kama walikunja kushoto kama wanaelekea njia ya vingunguti, Anyeifahamu kiwalani vizuri ashafahamu chocho ninayoizungumzia.

Kufika home naelezea naambiwa, Nilitakiwa niseme "MCHANA" , ndio nikashangaa? How comes?

Anyway mimi niliyokua najua ni mtu akikuambia "SALAMA?" unajibu "SALAMA"

Tupeane tips kama kuna ishara au salamu nyingine za siku, haya maisha ya kuishi kwa mbio, sio siku zote utashinda.
Pole sana Mkuu..kuna baadhi ya Maeneo Usiku unatembea kwa code
 
Back
Top Bottom