Kumbe Katiba ya Tanzania Haitumiki Zanzibar! - Pinda akiri Utata!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni asubihi hii, imedhihirika kumbe Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, haitumiki Zanzibar hata katika uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Muungano!

Tanabahi hiyo, imetolewa na swali toka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, na kuuliza kwa nini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeipa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEK), uwakala wa kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge, lakini ZEC inatumia sheria ya uchaguzi ya Zanzibar badala ya ile ya Muungano?. Mhe. Hamad Rashid akauliza endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ya ubunge wa Muungano, kesi hii itaamuliwa kwa sheria gani?.

My Take.
Kumbe zaidi ya zile kero za muungano zilizokuwepo, bado kero zinazidi kuibuliwa kila kukicha, hivi kuna tatizo gani kwa Tanzania na Zanzibar kuufumua huu muungano na kuufuma upya tukianzia na katiba mpya sio tuu, kuunda muungano thabiti, imara na madhubuti bali pia kutengeneza level playing ground kwenye medani za siasa?.

Waziri Mkuu Pinda alikiri hilo ni tatizo na ufumbuzi wake utapatikana endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ambayo haijawahi kutokea, atasubiri busara za mahakama kwenye hili.

Mwanasheria Mkuu wa JMT alikuwepo huko Bungeni au hakuwepo? Swali kama hilo Waziri Mkuu hakutakiwa KABISA kujaribu kulijibu!! Siyo kila swali analoulizwa afikiria analo jawabu.
.
Q&A ni ya PM tuu. Ila pia Pinda, amekiri kuwa hili ni gumu, wanachoweza kufanya, ni kusubiri siku Wizara ya Sheria na Katiba itakapowasilisha makadirio yake, kambi rasmi ya upinzani iliweke hili kwenye maoni ya upinzani.

Tukubali tusikubali, structure ya Muungano wetu ina matatizo. Zanzibar ni jeuri, inatumia jeuri ya uwepo wa katiba yake kuendesha kila kitu Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hata kwenye mambo ya Muungano. Ukizama sana kwenye hili, unaweza kuta kumbe hao wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT sio legitimate MPs kwa sababu hawakuchaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT!.

Kimfumo, Tanzania ni nchi moja, Union, na Katiba ya JMT ndio sheria mama, supreme, na Katiba ya Zanzibar ni subordinate tuu, sasa hii ZEC imepata wapi mamlaka sio tuu ya kuitumia sheria ya Uchaguzi ya ZEK kwa wabunge wa Muungano, bali pia kui-sideline/ignore Sheria mama ya Uchaguzi ya NEC?.

Natamani kuiona hand-over note YA NEC iliyodelegate powers kwa ZEC kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge kama wakala wa NEC lakini kwa kutumia sheria ya ZEC.

Wakati ni delegete, delegete hawezi ku delegate. Sijapata kusikia wakala anaepaswa kutekeleza majukumu ya aliyemtuma kwa, akitekeleza kwa kujiundia sheria zake, badala ya sheria za aliyemtuma.

Naomba tusizame zaidi kwenye hili, tukizama sana humu, tutarudi kule kule kwenye malumbano ya uhalali (legality) ya huu Muungano wetu.
Pasco
 
Pinda is not serious!

Tatizo lipo - Ufumbuzi wake mpaka itokee kesi - na uamuzi wa kesi utategemea busara za mahakama!
 
Waziri Mkuu Pinda alikiri hilo ni tatizo na ufumbuzi wake utapatikana endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ambayo haijawahi kutokea, atasubiri busara za mahakama kwenye hili.

Du! bongo bana, sasa huko mahakamani si wanasema mambo ya siasa ni bungeni, huyu mkuu anatwambia tena otherwise. Inakuwaje Lol.................
 
Nimelisikia swali, lilikuwa la akili sana na inaonyesha kweli kuna problem kubwa ya Kikatiba kwenye suala hili. Inaelekea CUF wana orodha ndefu ya matatizo ya kikatiba katika set up ya Muungano na wanatyoa issues kidogo kidogo. Nawashauri wangeandaa dossier kuhusiana na matatizo haya ya kikatiba ambayo wataitumia kupush agenda ya kuandikwa kwa katiba mpya
 
Waziri Mkuu Pinda alikiri hilo ni tatizo na ufumbuzi wake utapatikana endapo kutatokea kesi ya uchaguzi ambayo haijawahi kutokea, atasubiri busara za mahakama kwenye hili.

Halafu tunasema tunae waziri mkuu!
Busara ya mahakama ni kutokuingilia/kutoamua mambo ya kisiasa hivyo ishu hii ikitokea mahakama itairudisha bungeni kama ilivyofanya kwenye ishu ya mgombea binafsi!
 
Mwanasheria Mkuu wa JMT alikuwepo huko Bungeni au hakuwepo? Swali kama hilo Waziri Mkuu hakutakiwa KABISA kujaribu kulijibu!! Siyo kila swali analoulizwa afikiria analo jawabu.
 
Mwanasheria Mkuu wa JMT alikuwepo huko Bungeni au hakuwepo? Swali kama hilo Waziri Mkuu hakutakiwa KABISA kujaribu kulijibu!! Siyo kila swali analoulizwa afikiria analo jawabu.

Hii wameiiga ile "PMQ" ya kila Jumatano kule Uingereza. Majibu yote anayatoa WM tu. AG hakuwepo leo lakini hata angekuwepo asingejibu.
 
Mwanasheria Mkuu wa JMT alikuwepo huko Bungeni au hakuwepo? Swali kama hilo Waziri Mkuu hakutakiwa KABISA kujaribu kulijibu!! Siyo kila swali analoulizwa afikiria analo jawabu.
.
Q&A ni ya PM tuu. Ila pia Pinda, amekiri kuwa hili ni gumu, wanachoweza kufanya, ni kusubiri siku Wizara ya Sheria na Katiba itakapowasilisha makadirio yake, kambi rasmi ya upinzani iliweke hili kwenye maoni ya upinzani.

Tukubali tusikubali, structure ya Muungano wetu ina matatizo. Zanzibar ni jeuri, inatumia jeuri ya uwepo wa katiba yake kuendesha kila kitu Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hata kwenye mambo ya Muungano. Ukizama sana kwenye hili, unaweza kuta kumbe hao wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT sio legitimate MPs kwa sababu hawakuchaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT!.

Kimfumo, Tanzania ni nchi moja, Union, na Katiba ya JMT ndio sheria mama, supreme, na Katiba ya Zanzibar ni subordinate tuu, sasa hii ZEC imepata wapi mamlaka sio tuu ya kuitumia sheria ya Uchaguzi ya ZEK kwa wabunge wa Muungano, bali pia kui-sideline/ignore Sheria mama ya Uchaguzi ya NEC?.

Natamani kuiona hand-over note YA NEC iliyodelegate powers kwa ZEC kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge kama wakala wa NEC lakini kwa kutumia sheria ya ZEC.

Wakati ni delegete, delegete hawezi ku delegate. Sijapata kusikia wakala anaepaswa kutekeleza majukumu ya aliyemtuma kwa, akitekeleza kwa kujiundia sheria zake, badala ya sheria za aliyemtuma.

Naomba tusizame zaidi kwenye hili, tukizama sana humu, tutarudi kule kule kwenye malumbano ya uhalali (legality) ya huu Muungano wetu.
Pasco
 
.
Q&A ni ya PM tuu. Ila pia Pinda, amekiri kuwa hili ni gumu, wanachoweza kufanya, ni kusubiri siku Wizara ya Sheria na Katiba itakapowasilisha makadiria yake, kambi ya upinzani iliweke kwenye maoni ya upinzani.

Tukubali tusikubali, structure ya Muungano wetu ina matatizo. Zanzibar ni jeuri, inatumia jeuri ya uwepo wa katiba yake kuendesha kila kitu Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hata kwenye mambo ya Muungano. Ukizama sana kwenye hili, unaweza kuta kumbe hao wabunge wa Zanzibar sio legitimate MP kwa sababu hawakuchaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Kimfumo, Katiba ya JMT ndio sheria mama, na Katiba ya Zanzibar ni subrdinate tuu, sasa hii ZEC imepata wapi mamlaka sio tuu ya kuitumia sheria ya Uchaguzi ya ZEK kwa wabunge wa Muungano, bali pia kui-sideline/ignore Sheria ya Uchaguzi ya NEC.

Natamani kuina hand-over note YA NEC iliyodelegate powers kwa ZEC kuendesha uchaguzi wa rais na wabunge kama wakala wa NEC.
Sijapata kusikia wakala anaepaswa kutekeleza majukumu ya asliyemtuma kwa kujiundia sheria zake!.

Tukizama sana humu, tutarudi kule kule kwenye malumbano ya uhalali (legality) ya huu Muungano wetu.

Mh. Rashid naye si mbunge wa JMT? sasa yeye mwenyewe hatma yake ni ipi?. Ninavyoelewa kule ZNZ kuna Wawakilishi ambao nadhani ndio wabunge halali wa huko. Hawa wabunge wanaokwenda DOM kama MH. Rashid wanaweza kujikuta hawana pa kwenda maana maamuzi mengi kuhusu kero za muungano huwa yanatolewa na Baraza la Wawakilishi!!
 
Hivi hii serikali ya CCM ina matatizo gani, kwanini hawataki kuwa pro-active?
Yaani kweli PM anakiri na kusema solution itatokea pale tatizo litakapotokea!!! Huu muungano ni zimwi tusilolijua litatula mpaka twishe!!!

Shame on the government!!
 
Back
Top Bottom