Kumbe CDM hamna Wasomi

Hao wenye CV kali wameisaidia nini nchi hii kama si kuichana chana kwa manufaa ya matumbo yao na familia zao?
 
kutokana na huu mlolongo wa watu kuweka cv za baadhi ya wabunge, imenibidi niangalie baadhi ya cv za wabunge wa chadema kweli ina tia aibu! kweli ndo mna taka kuchukua nchi?

Mbona viongozi wengi wa CCM wamesomea madarakani? Wengi wamesoma Open University na waliianzisha mahususi ili wao waweze kuneemeka. Halafu inawezekana hayo ndo matunda ya CCM madarakani miaka zaidi ya 40. We unadhani wale waliogushi vyeti geshini na geshi la bolosi wametoka wapi? Nyani aoni kundule
 
Suala hapa sio cv kikubwa hapa ni hekima,uaminifu,na kusimamia vema mali za umma na rasilimali za taifa..cv mara nyingine huwa kama pambo..
 
Haina haja ya kuumiza kichwa kwani uyo Ngumbalu hana lolote nae kama magamba wenzie tuuu! PASIPO BUSARA USHINDI HUENDA KWA MPUMBAVU!
 
nawashangaa sana cdm ,wanataka kuongoza nchi hii ,ukiangalia pale ndani utaona hamna kitu ,hivi wanafikiria wanataka kuongoza kijiji ? Ndio maana unawasikia wataunda serikali ndogo iliyo na mawaziri wachache sana,nikakumbuka pale walipoweka mgombea mwenza jamaa aliehitimi darasa la saba ,na kwa zanzibar hakuna darasa saba ,inamaana alikimbia shule. Eti watategemea washauri ,unategemea washauri wakati nao wanahitaji elimu ya juu.

Hebu tupangieni hapa safu yenu ,tuiite proposed safu ya uongozi ,ukianza na raisi labda tuseme wizara kumi mpaka kumina tano ,tuone ! Na kuwajadili au kuijadili hio safu !

this post deserve to the crapiest post of the day hongera dada!
 
Nawashangaa sana CDM ,wanataka kuongoza Nchi hii ,ukiangalia pale ndani utaona hamna kitu ,hivi wanafikiria wanataka kuongoza kijiji ? Ndio maana unawasikia wataunda serikali ndogo iliyo na mawaziri wachache sana,nikakumbuka pale walipoweka mgombea mwenza jamaa aliehitimi darasa la saba ,na kwa Zanzibar hakuna darasa saba ,inamaana alikimbia shule. eti watategemea washauri ,unategemea washauri wakati nao wanahitaji elimu ya juu.

Hebu tupangieni hapa safu yenu ,tuiite proposed safu ya uongozi ,ukianza na Raisi labda tuseme wizara kumi mpaka kumina tano ,tuone ! na kuwajadili au kuijadili hio safu !

Kama Zanzibar wameweza kuunda serikali, wakati wasomi ni hadithi ndefu, itakuwaje Chadema lincho lote hili la watu 40+ milioni wakose administrators ??
Rudi kajipange upya mwiba. Nadhani uliandika msg hii ukiwa na njaa kubwa
 
Nawashangaa sana CDM ,wanataka kuongoza Nchi hii ,ukiangalia pale ndani utaona hamna kitu ,hivi wanafikiria wanataka kuongoza kijiji ? Ndio maana unawasikia wataunda serikali ndogo iliyo na mawaziri wachache sana,nikakumbuka pale walipoweka mgombea mwenza jamaa aliehitimi darasa la saba ,na kwa Zanzibar hakuna darasa saba ,inamaana alikimbia shule. eti watategemea washauri ,unategemea washauri wakati nao wanahitaji elimu ya juu.

Hebu tupangieni hapa safu yenu ,tuiite proposed safu ya uongozi ,ukianza na Raisi labda tuseme wizara kumi mpaka kumina tano ,tuone ! na kuwajadili au kuijadili hio safu !

Wasomi wanaogopa kushiriki mikiki ya mabadiliko na itachukua muda.Ukiangalia mtizamo wa Tanzania kwa upinzani ni uasi na hii inafanya wasomi waogope.
 
Kwanza kabisa, Nyerere hakushindwa. Lile baraza lake la kwanza la mawaziri huwezi kulilinganisha na baraza la mawaziri hamsini wa sasa wa Kikwete. Changamoto alizokabiliana nazo Nyerere huwezi kuzilinganisha na changamoto zinazokabili uongozi wa leo, kama kweli bado tuna uongozi. Umeshawahukumu CDM kuwa opportunists, huku unafumbia macho opportunism ya uongozi wa CCM ambao umetufikisha hapa tulipo. Ni uwongo mkubwa kusema kuwa CDM haijawahi kuelezea sera za kuongeza pato la taifa. Ama you have not been listening na kama ni kweli CDM hawana sera jiulize iweje leo Watanzania wa kawaida wavutiwe kwenye mikutano yao ya hadhara hata bila kupewa ubwabwa na t-shirts kama chama fulani kinavyofanya kila siku? Ndugu yangu nakuona uko kwenye denial. Miaka 10-15 mingine chini ya CCM madini yetu yatakuwa yamekwisha, tumebaki na makorongo tu na wazungu walishasepa siku nyingi kwao ulaya. Ukiniuliza mimi, hata 2015 ni mbali sana. Ningependa kuona CCM inaondolewa mamlakani mara moja.

Kaka taratibu, tanzania haitaishiwa rasilimali watu na ardhi ambazo ni muhimu kuliko zote. ( kwenye hili la ardhi bila sera na itikadi nzuri za CCM hii rasilimali muhimu ingekua mikononi mwa wageni watupu na wazawa kukosa ardhi kabisa. wewe leo bado unajivunia kununua na kuuza ardhi shukuru CCM ).

Baadhi ya wananchi wanavutiwa na CDM kwa sababu ya sarakasi zisizoisha zaa kiongozi mmoja dhaifu na si kwa sababu ya sera za mbaya za CCM au nzuri za CDM. Hizi sarakasi na vita ya ndani ya kwa ndani imedhoofisha serikali na CCM kufikia mahali CDM wanaonekana viongozi walio tayari kwa Tanzania. Kumbuka vita hii ya ndani kwa ndani ni kwa sababu ya roho na moyo wa CCM na maisha yake yajayo..kwa uzoefu na akili zao 2015 wataweka timu makini kuongoza taifa na chama. Labda kama Dhaifu, Mamvi na wenzake wanaona kua bora CDM kuliko baadhi ya watu makini CCM, hapo sawa, bila hujuma na mengineyo wananchi watapiga kura CCM na Rais na Bunge litaongozwa na CCM 2015.
 
Join Date : 23rd October 2007

Posts : 4,215
Rep Power : 1802
Likes Received: 93

Likes Given: 3

Hoja zako hazifanani na umri wako hapa JF...Na haya ndio madhara ya kukimbia shule na yatatugharimu sana watanzania tunapoelekea kwenye shirikisho la EAC.

Hata mimi nimeshangaa sana, anaonekana ni mkongwe lakini kaja na hoja dhaifu sana! Hivi anajua kuwa CDM ikichukua nchi wasomi tupo wengi sana tunao support na utendaji na uendeshaji wa serikali haitakuwa tatizo? Mleta mada umechemka! Kwani Rwanda iko wapi sasa na rasilimali kubwa iliyopoteza miaka ya 94 wakati wa mauaji ya Kimbari?
 
Kaka taratibu, tanzania haitaishiwa rasilimali watu na ardhi ambazo ni muhimu kuliko zote. ( kwenye hili la ardhi bila sera na itikadi nzuri za CCM hii rasilimali muhimu ingekua mikononi mwa wageni watupu na wazawa kukosa ardhi kabisa. wewe leo bado unajivunia kununua na kuuza ardhi shukuru CCM ).

Baadhi ya wananchi wanavutiwa na CDM kwa sababu ya sarakasi zisizoisha zaa kiongozi mmoja dhaifu na si kwa sababu ya sera za mbaya za CCM au nzuri za CDM. Hizi sarakasi na vita ya ndani ya kwa ndani imedhoofisha serikali na CCM kufikia mahali CDM wanaonekana viongozi walio tayari kwa Tanzania. Kumbuka vita hii ya ndani kwa ndani ni kwa sababu ya roho na moyo wa CCM na maisha yake yajayo..kwa uzoefu na akili zao 2015 wataweka timu makini kuongoza taifa na chama. Labda kama Dhaifu, Mamvi na wenzake wanaona kua bora CDM kuliko baadhi ya watu makini CCM, hapo sawa, bila hujuma na mengineyo wananchi watapiga kura CCM na Rais na Bunge litaongozwa na CCM 2015.
Ni kweli Tanzania haitaishiwa raslimali watu. Lakini Kikwete kishaanza kutupiga bei kwa wawekezaji. Watu wanahamishwa kiholela ili mwekezaji (mzungu) apewe eka 800,000 za kulima mazao ya genetic. Sisi, raslimali watu, tutakuwa manamba tu wa kuchota maji na kukata kuni kwa mzungu. Nimesoma mahali kuwa population ya Tanzania katika miaka 50 ijayo itakuwa double ya population ya sasa (millioni 90) lakini kwa kasi ambayo serikali ya Kikwete/CCM inavyogawa ardhi yetu kwa "wawekezaji" kwa mikataba ya miaka 90, tutajikuta tukiwa landless in our own societies. Ukitizama mkataba wa Kisarawe ambapo mzungu kapewa ardhi kujizalishia biofuel, si kwa manufaa yetu bali kwa manufaa yake, uende Mvomero ambako kuna mvutano leo kati ya raia wa asili na mwekezaji wa kigeni, halafu Arusha ambako kaburu kapewa mashamba ambayo sasa anayakodisha kwa wananchi, unajiuliza tunakwenda wapi? Ndizo sera za CCM hizo unazosifia?
 
Yaani hao CCM, hizo Degree zao za PASS, Ualimu wao wa UPE, Masters walizopata uzeeni kwa kuungaunga na vyeti feki ndio vinawapa jeuri, wanajiona wako juuu, wasomi wamekaa kimya hawajishaui, mlioshindwa shule, mkaishia kuforge vyeti na wale waliomaliza levels mbalimbali za elimu kwa kubahatisha, chabo na wizi wa mitihani, na kuishia kuwa na elimu cheti, wakati kichwani hawana lolote, bado wanathink kama watoto wanaocheza kombolela, ndio mnajifanya mko juu sana kielimu, unaweza ukawa una vyeti vizuri kweli kigrade but ability yako kudo, kuwork kwa kiwango kile cheti chako kilivyokuelezea, ni zero, kumbe ni vyeti vinavyotokana na chabo na rushwa katika elimu, kuhonga waalimu!
Wasomi wa CCM wameifikisha wapi CCM na nchi kwa ujumla? Mwenyekiti wenu mchumi wa chuo kikuu hajui kwa nini nchi anayoiongoza ni maskini!

Wasomi CDM wako wengi sana, tofauti ni kuwa wengi wao ni vijana wadogo na professionals wenye shughuli zao. Unataka wote tuvae magwanda kwenda maofisini ndio mjue kuna wasomi kiasi gani! 2015 ndio utaona ninachozungumzia leo.
 
Nikuonavyo unapingana na mawazo yako mwenyewe, sitoshangaa siku moja nikikuona unapoteza muda wako bure kwa kufikiria vitu usivyoweza kuvijua kama 'asili ya mungu' kwamba alitokea wapi. Uwezo wa akili ya mtu huishia kufikiri yale aliyojifunza, mpumbavu hutaka kujua asiyojifunza. Suala la CDM na cabinet yake sio priority ya chama kwa sasa ukizingatia kwamba kwanza wako wachache sana bungeni na wao sio serikali ama back up yake. Subiri gari na,
namba T2015 CDM liungurume then upime uzito wa engine yake.
Na ndio nikasema nimewapa ushindi wa yote hayo,kwayo yataendeleza Tanzania ,na ni nani hao watakao endeleza ushindi huo ,maana nikiangalia ndani siwaoni, Inawezekana wizara nilizohitaji ni nyingi na hamuwezi kuzitosheleza kutokana na kutokuwepo wenye sifa za kuongoza nafasi hizo nyeti za uongozi.
 
Wasomi wa CCM wameifikisha wapi CCM na nchi kwa ujumla? Mwenyekiti wenu mchumi wa chuo kikuu hajui kwa nini nchi anayoiongoza ni maskini!

Wasomi CDM wako wengi sana, tofauti ni kuwa wengi wao ni vijana wadogo na professionals wenye shughuli zao. Unataka wote tuvae magwanda kwenda maofisini ndio mjue kuna wasomi kiasi gani! 2015 ndio utaona ninachozungumzia leo.
Mtoa mada hapa anataka umutoe Shaka Kwamba CDm ni zaidii ya uwazili wa akina sugu,vicent,lema...... Mi naona it's a right time kuvaa gwandaz iLi hofu Itoke...............
 
Kuna watu mnatafutiaga wenzenu Ban tu.. sasa huko ccm hao wasomi ndio wepi? Kina Lukuvi?
 
mm nadhan ndugu hauhitaji kuwa na woga kuhusu CDM kuongoza nchi kimafanikio. Chadema ina wasomi makinisana na kwa bahati nzuri ni vijana na wazee ni wachache. ukitaka kujua ukweli watafute marafiki na wapenzi wa chama cha CDM
 
nothing to wish..facts are facts. Chademu will make excuse about everything hata kama ukweli upo dhahiri, tabia ambayo wameiga kutoka kwa masahiba zao Magamba.

Fact zipi CCM wangekuwa na wasomi wa kweli sio wa kununua vyeti au waliosoma kweli na kusimama katika principles za usomi na sio kupamba ukuta kuwa nao wana shahada pia Tanzania pamoja na raslimali zote ilizonazo ingekuwa hapo ilipo? Elimu sio lazima uingie darasani ukapate shahada ya uzamili elimu ni ufahamu wa kujua mambo ya kuyatawala mazingira ukatoka katika hali duni na kwenda hali nzuri zaidi. ufahamu huo haujalishi uliupata wapi, kwa njia zipi na katika mazingira yapi ili mradi ufahamu huo unao na umeuonyesha watu wakaona kama ambavyo CHADEMA wameonyesha.

Mfano Kikwete kasoma shahada ya uchumi lakini kiuchumi kathibitisha ni mtupu kiasi kwamba kazidiwa maarifa ya kiuchumi na Mkapa ambaye alisoma habari kwa maana hiyo Kikwete pamoja na kuwa alimaliza shahada ya uchumi shahada yake inaonekana ni ya kupamba ukutani zaidi maana ufahamu wake katika uchumi ni mdogo kulinganisha na Mkapa ambaye hatujui yeye ufahamu wake katika uchumi alipata wapi ili mradi alionyesha ni zaidi ya Kikwete maana elimu haijalishi uliipata wapi na katika njia zipi ili mradi umethibitisha unaweza.

Pia tukumbuke kuna viongozi wamekuwa na kiwango cha elimu cha darasani kidogo sana lakini wameonyesha wanaweza maana wanaufahamu mwingi wanajua wao walikoupata ingawa walikomea madarasa ya chini darasani mfano Jacob Zuma darasa la nne, Lula Da Silva Rais wa zamani wa Brazil darasa la saba, Omar Bongo Certificate, John Major waziri mkuu wa Uingereza Diploma, na wengine wengi. kuhusu wabunge kuwa na elimu ya kawaida haina shida kabisa ili mradi wanakubalika kwa wananchi na wanajua wafanyalo ndio maana CDM inataka mawaziri wasiwe wabunge ili wachaguliwe professionals kushika wizara na sio wanasiasa kama Ngeleja, Maige, Nkullo na Mponda ambao uwezo ni mdogo pamoja na elimu zao za darasani na matokeo ni kuliibia taifa.
 
cdm ina madaktari, wachumi, wanasheria, mawakili, maprofesa, mainjia, yan kila fani muhimu ktk kuongoza nchi
 
Fact zipi CCM wangekuwa na wasomi wa kweli sio wa kununua vyeti au waliosoma kweli na kusimama katika principles za usomi na sio kupamba ukuta kuwa nao wana shahada pia Tanzania pamoja na raslimali zote ilizonazo ingekuwa hapo ilipo? Elimu sio lazima uingie darasani ukapate shahada ya uzamili elimu ni ufahamu wa kujua mambo ya kuyatawala mazingira ukatoka katika hali duni na kwenda hali nzuri zaidi. ufahamu huo haujalishi uliupata wapi, kwa njia zipi na katika mazingira yapi ili mradi ufahamu huo unao na umeuonyesha watu wakaona kama ambavyo CHADEMA wameonyesha.
Chademu walisimamisha mgombea mwenza wa Urais darasa la saba, ilhali wao hivi sasa wameshasahau na kuanza kuwakejeli akina Prof. Maji Marefu. Sioni hoja yako ni nini? au kwa nini unajibu post isiyohusu.. #goingincycles

Mfano Kikwete kasoma shahada ya uchumi lakini kiuchumi kathibitisha ni mtupu kiasi kwamba kazidiwa maarifa ya kiuchumi na Mkapa ambaye alisoma habari kwa maana hiyo Kikwete pamoja na kuwa alimaliza shahada ya uchumi shahada yake inaonekana ni ya kupamba ukutani zaidi maana ufahamu wake katika uchumi ni mdogo kulinganisha na Mkapa ambaye hatujui yeye ufahamu wake katika uchumi alipata wapi ili mradi alionyesha ni zaidi ya Kikwete maana elimu haijalishi uliipata wapi na katika njia zipi ili mradi umethibitisha unaweza.
Mkapa did though hatch grand theft and corruption, sijui nayo alisomea wapi? au ndo uchumi wenyewe? recipe ya maendeleo naona bado hujaijua.

Pia tukumbuke kuna viongozi wamekuwa na kiwango cha elimu cha darasani kidogo sana lakini wameonyesha wanaweza maana wanaufahamu mwingi wanajua wao walikoupata ingawa walikomea madarasa ya chini darasani mfano Jacob Zuma darasa la nne, Lula Da Silva Rais wa zamani wa Brazil darasa la saba, Omar Bongo Certificate, John Major waziri mkuu wa Uingereza Diploma, na wengine wengi. kuhusu wabunge kuwa na elimu ya kawaida haina shida kabisa ili mradi wanakubalika kwa wananchi na wanajua wafanyalo ndio maana CDM inataka mawaziri wasiwe wabunge ili wachaguliwe professionals kushika wizara na sio wanasiasa kama Ngeleja, Maige, Nkullo na Mponda ambao uwezo ni mdogo pamoja na elimu zao za darasani na matokeo ni kuliibia taifa.
Umuhimu wa kuwa viongozi wenye elimu na ufahamu wa kutosha hauwezi kuwa overemphasized zaidi ktk nchi yetu kwa sababu mfumo wetu unawapa hawa madaraka ya kuamua mambo yote ya msingi. Japo binafsi sipendezewi na utaratibu huo lakini ndio hali halisi. Kama SA na wengine waliweza, wamebahatika pengine, lakini hatuwezi kushusha standards kwa visingizio vyovyote vile. Mwakilishi wa wananchi kuanzia ubunge na kuendelea lazima awe amefuta ujinga walau ktk ngazi ya stashahada au shahada, hiyo haikwepeki tena ktk zama hizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom