The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Wengi tunahudhuria mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu .
Wengine tunafuatilia mitandaoni hatua kwa hatua mwenendo wa kesi nzima....
Kwa ambao hawajui au hawakumbuki au kusahau ni kuwa, kinachoendelea sasa ni kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within a trial)...
Kinachobishaniwa ni aidha maelezo ya mshitakiwa wa 1 Adamoo na wenzake waliyoyatoa polisi yapokelewe au yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashitaka...
UPANDE WA MASHITAKA, unadai yapokelewe kwa sababu yalichukuliwa kwa utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa sheria na PGO na watuhumiwa kusaini wenyewe kwa hiari yao...
UPANDE WA UTETEZI NA WASHITAKIWA WENYEWE, unapinga yasipokelewe kwa sababu unadai maelezo hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria (chini ya shinikizo la mateso makubwa kwa watuhumiwa) kama njia ya kuwalazimisha kukubali na kusaini maelezo ambayo hawajui yameandikwa na nani...!!
Hii ndiyo sababu upande wa mashitaka waliwekewa "OBJECTION" na washitakiwa (utetezi) katika hili na kuzaa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa na ndiyo inayosikilizwa sasa...
Ni katika hatua hii ya kesi hii ishu ya PGO imezuka kwa namna ya kipekee sana na watu kujua kumbe polisi wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kipolisi wa kila siku ikiwemo kukamata na kuhoji watuhumiwa, kuwasafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine nk nk kwa mujibu wa PGO...!!
Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, maamuzi yoyote ya kesi hii ndogo ndiyo yàtakayotoa uelekeo wa kesi kubwa ambayo huko mbele tutamkuta kinara anayelengwa kuangamizwa au kufungwa (mshtakiwa namba 4, yaani Mh. Freeman A. Mbowe)...
MASWALI YA KUTUONGOZA KATIKA MJADALA HUU NI HAYA;
1. Je, mpaka hatua hii kwa wote mnaofuatilia kesi hii, na kwa mtazamo wa kila mmoja based on the evidence uliokwisha kutolewa, unadhani objection ya upande wa utetezi itatoboa....?
2. Kwa maelezo ya mshtakiwa namba 1 na 2 ambao pia ndiyo mashahidi wenyewe wa kesi hii ndogo, unadhani wameweza kuishawishi mahakama kuwa ni kweli waliteswa kama njia ya kuwalazimisha kukubali maelezo waliyoyatoa polisi chini ya kiapo cha "onyo?"...
3. Ili kuthibitisha kuwa mtu fulani aliteswa, ukiachilia mbali maelezo ya mdomo kuwa nilipigwa sana na kufanyiwa hivi au vile, ushahidi mkubwa huwa ni alama za makovu ya vidonda katika mwili...
Je, mashahidi walionesha alama zozote zinazoashiria tendo la kupigwa na kuteswa lilitendeka kweli....?
Alamsiki. Karibuni kwa mjadala...