Kulima kwa kutumia trekta

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,553
3,070
Habari,

Jamani naomba kuuliza hivi kujua kulima kwa kutumia trekta kunahitaji utaalam mkubwa? Nahitaji kwenda kozi? Au mimi naweza kujifunza kwa kuangalia na kufuatilia kama kuendesha gari?

Nafikiria nijue siku nyingine niwe nasonga mwenyewe front-line au hata kama natoa maelekezo na mimi nijue nini kinaendelea.

Naomba maelezo wandugu.
 
Unaweza kujifunza mwenyewe ukiwa shambani Unatakiwa uwe mvumilivu sana kwani trecta linarusha sana na unaka muda mrefu kwenye kiti vumbi juwa mvua na mtikisiko wa trecta vyote vinakusubiri cha msingi uwe mvumilivu tu. issue kubwa ni kuweza kubalance tairi kwenye mstari na adjustment ya jembe liwezi kurusha udongo umbali wa kawaida usifukie majani
 
mkuu unawez jifunza kwa dreva wa hilo trekta, lakini unatakiwa kwanza ujue kuliendaha vizuri kabisa kabla ya kuanza kujifunza kulima nalo, Kama unaweza kuliendesha bila tatizo unaweza kuwa unajifunza taratibu utaelewa na haitaki papara,
Kuna kuua Trekta mkuu hasahasa kwenye Hydroric ya jembe au kupasua brock,
 
HAPANA! KULIMA KWA TREKTA UNAHITAJI UJUZI! Suala si kuendesha trekta, ni pamoja na kujua aina ya udongo, kiwangocha unyevunyevu kwenye udongo, level of compaction, na hivyo ujue angle ipi unaingiza majembe ndani ya udongo, hesabu ya ulaji wa mafuta kwa aina fulani ya udongo, na mambo mengine.Ukitaka kufanya vizuri ni bora uende shule usifanye mambo kikanjanja! FINITO!

Back
Top Bottom