We Know Next
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 814
- 380
Bravo viongozi wetu wa Dini. Fanyeni kazi mliyotumwa na Muumba. Hivi Tendwa ana Dini? Siamini kabisa yanayoendelea kutoka ktk kinywa chake.
Tendwa inamuuma kusikia mwaka huu pesa za mafisadi ZITALIWA bila KURA...:A S 13:
Mwaka huu mtikisiko wa wala rushwa ni mkubwa na utaacha historia katika bara la afrika. RUSHWA ni mbaya, RUSHWA ni dhambi, RUSHWA imetutenganisha watanzania na Uso wa Mwenyenzi MUNGU.
Tendwa amemjibu askofu Mokiwa kwa kusema askofu huyo kwa kauli yake ya kuwaeleza wananchi kuwa wale pesa za wagombea na kura wampe kiongozi anayefaa inamfanya askofu huyo kuwa sehemu ya rushwa.
My take here:
Askofu Mokiwa ana kosa gani kutoa elimu ya uraia hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu?
Nani anakiuka sheria hiyo ya gharama ya uchaguzi anayoisema Tendwa?
Hao wanaotoa rushwa ndio walisababisha maisha magumu kwa watu, wahujumu uchumi wakubwa, walikusanya hizo pesa na sasa wanazitumia kuwarubuni watu, tuzipokee hizo pesa, ni zetu na tuwanyime kura zetu!