Kukosolewa. . . .

Ni hulka ya wengi sana wanapenda kuendelea kusifiwa kila wafanyapo jambo lolote hata kama jambo hilo sio jema kihivyo
Yaani wanataka waonekane wako sawa wakati wote
 
mimi naona unavyonishambulia kama vile wanichukia.......................msema kweli ni kipenzi cha Mungu............lakini ni adui wa mwanadamu pia............................ukweli ni kuwa kukosoa itategemea na jinsi unavyomkosoa mwenzio...................kuna mahali hata umediriki kusema ya kuwa umeamua kuwa ....."mkali kidogo" kwa umombo........hata nimesahau................something like "sarcastic".................hivi hata huyo unayemkosoa lengo kweli ni kumsaidia au kumdhalilisha kwa kumuumbua..................but I love you dear because if i do not the love of CHRIST is not in me........................

aaaawwwww that's so cute!

:D :D :D
 
Nimetoa changamoto watu ambao hukwazika pale wakosolewapo wajitaje na mpaka sasa hakuna hata mmoja aliyejitaja. Sasa kweli ina maana sisi wote tuliochangia humu huwa hatukwaziki jamani?

Au ndo yaleyale ya nyani (no pun intended) haoni kundule?
 
Hahahaha!!!

ndo hivyo,we ukiona umemkosoa mtu afu anakuangalia tu,hakujibu kitu ujue yameingia kulia na kutokea kushoto..ila anaekasirika na kutukana ujue yamefika mpaka kwenye vyumba vya ndani kabisa vya moyo wake na huyu ndo anauwezekano mkubwa sana wa kuufatilia ushauri wako baadae..
 
Ni hulka ya wengi sana wanapenda kuendelea kusifiwa kila wafanyapo jambo lolote hata kama jambo hilo sio jema kihivyoYaani wanataka waonekane wako sawa wakati wote
upo wewe mkuu wewe ni mfano wa kuigwa hapa bongo huna ubishi wa kiboya boya mkuu
 
Bado nasubiri...nani kati yetu atakuwa wa kwanza kukubali kukwazika na mikosoo ya watu!!!! Manake binadamu bana...tu ma hodari sana wa kuona kasoro za wengine.
 
Mie hukwazika sana, tena ukizidi nikosoa naweza lia mbele ya PC yangu.
Na siku nikikufahamu ntakugonga hata na baskeli yangu

Nimetoa changamoto watu ambao hukwazika pale wakosolewapo wajitaje na mpaka sasa hakuna hata mmoja aliyejitaja. Sasa kweli ina maana sisi wote tuliochangia humu huwa hatukwaziki jamani?

Au ndo yaleyale ya nyani (no pun intended) haoni kundule?
 
Back
Top Bottom